WAANDISHI WA HABARI VIJANA WAPATIWA MAFUNZO YA KUTAMBUA TAARIFA SAHIHI KUELEKEA KIPINDI CHA UCHAGUZI.
NA MARYAM NASSOR
WAANDISHI
wa Habari Vijana wametakiwa kuisoma
elimu ya Artificial Intellegence ‘AKILI
UNDE’ na kuielewa kwani wao ndio
kinga moja wapo ya kuhakikisha jamii haiyathiriki
na Habari za Uongo( Mis information).
Akifungua
Mafunzo ya siku moja kwa waandishi wa Habari Vijana kutoka klabu za waandishi
wa Habari wa Unguja na Pemba,
Mkurugenzi kutoka Muungano wa
Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania
(UTPC) Keneth Simbaya katika Ukumbi wa Kituo cha Huduma za Sheria
Kijangwani Mjini Unguja.
Amesema,
lengo la mafunzo hayo ni kuwaandaa
waandishi wa Habari vijana kutekeleza majukumu ya kihabari kwa weledi na umahiri katika kipindi hichi cha uchaguzi ambacho kumekuwa kukishamiri Habari za uongo
na Upotoshaji mitandaoni.
“ Kama munavyofahamu katika dunia ya sasa ambayo imetawaliwa na matumizi mabaya na
mazuri ya ‘AKILI UNDE’ hivyo lengo la
mafunzo haya kwenu ni kuona kwa namna
gani munatambua taarifa sahihi na
zisizosahihi kupitia njia mbali mbali” amesema .
Mkurugenzi huyo, amewataka waandishi wa Habari kujifunza zaidi matumizi sahihi ya ‘AKILI UNDE’ ili kuhakikisha taarifa zinazosambazwa mitandaoni kuweza kuelewa usahihi wake.
Akiwasilisha
mada juu ya namna ya kuzitambua Habari
za Uongo na Ukweli Mkufunzi wa maswala
ya kimtandao Ephraim Muchemi, amewataka waandishi wa Habari kutumia program mbali
mbali kama vile Tine eye na Google ili kuweza kutambua taarifa hizo.
Amesema ,
lazima waandishi wa Habari wasome njia tofauti tofauti za kuthibitisha Habari
za uongo na ukweli kabla ya kuzisambaza
ili kuepusha taarifa za upoteshaji zisisambae.
“ Kuna njia nyingi zinaweza kusaidia katika kuzitambua Habari za Uongo na Upotoshaji ikiwa ni picha, video au hata maelezo unaweza kuingiza kwenye program ya Google Lens, Tin eye na nyenginezo kupata kujua usahihi wa taarifa hizo” amesema Mkufunzi huyo.
Kwa upande
wake, Afisa Programu kutoka UTPC Andrew
Marawiti, amewataka waandishi wa Habari hao kuendelea kuyafanyia
kazi mafuzo hayo kwa vitendo ili yaweze kuwasaidia katika shughuli zao za kiuandishi.
“ Kuwa kwenu
hapa leo haikuwa Bahati mbaya tambueni kuwa mulikuwa wengi sana kwenye maombi ila nyinyi ndio tumeona munafaa
zaidi kutokana na maelezo yenu
mulivyojielezea , hivyo basi tunaomba sana mukaendelee kuyatumia mafunzo haya kwa vitendo ili yaweze kuwasaidia zaidi
“ amesisitiza .
Nao, Baadhi
ya waandishi wa Habari waliyopatiwa mafunzo
hayo Suleiman Tambuligeni kutoka
Zanzibar Press Club (ZPC) na Muyaba Kombo kutoka Pemba Press Club (PPC) wamesema
mafunzo hayo yamekuja muda muafaka na yatawasaidia katika kipindi hicho
cha Uchaguzi Mkuu .
Akifunga
Mafuzo hayo ya siku moja, Mwenyekiti wa
Klabu ya Waandishi wa Habari Zanzibar ( ZPC) Abdalla Mfaume amesema katika zama
hizi za Maendeleo ya Sayansi na Teknolojia kumekuwa na Habari nyingi za Uongo na Upotoshaji. Hivyo amewaomba
waandishi hao kuyafanyia kazi mafunzo
hayo hasa kipindi hichi cha uchaguzi.
Mafunzo hayo ya siku moja, yamewashirikisha Waandishi wa Habari Vijana kutoka katika klabu za waandishi wa Habari wa Unguja na Pemba, ambayo yameandaliwa na Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania ( UTPC) kwa ufadhili wa Nether land (NL).
Mwisho





Post a Comment