TAMWA-ZNZ, yazindua Tuzo ya uwiano wa kijinsia kwa Vyombo vya Habari: "Kalamu Yangu, Mchango Wangu kwa Wanawake."

NA MARYAM NASSOR

JUMUIYA ya Wanawake wenye Ulemavu Zanzibar (JUWAUZA), Jumuiya ya Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA)  Jumuiya ya Mazingira, Jinsia na Utetezi Pemba (PEGAO), na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania, Zanzibar (TAMWA -ZNZ) kwa mashirikiano na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar (WEMA wametangaza rasmi uzinduzi wa Tuzo ya uwiano wa kijinsia kwa mwaka 2025/2026 yenye ujumbe unaosema "Kalamu Yangu, Mchango Wangu kwa Wanawake."

Akizungumza na vyombo vya habari,  Tunguu mkoa wa kusini Unguja  Mkurugenzi wa Chama hicho Nairat Ali Abdullah amesema tunzo hiyo itatambua waandishi wa habari na watengeneza maudhui (content creators) wa Zanzibar wanaoandika na kuandaa maudhui ya kina yanayoangazia mafanikio, changamoto na michango ya wanawake katika uongozi pamoja na kutatambua wahamasishaji jamii waliofanya vizuri katika ngazi za wilaya kwa namna wanavyoshiriki kikamilifu katika kukuza usawa wa kijinsia na kuhamasisha jamii kupitia kazi zao.

Amesema ,Malengo yao Kupitia tuzo hiyo, JUWAUZA, PEGAO, ZAFELA, WEMA na TAMWA ZNZ,  wanalenga:

  • Kuhamasisha uandishi na utengenezaji wa maudhui unaokuza usawa wa kijinsia.
  • Kukuza na kuimarisha uongozi wa wanawake katika sekta ya elimu.
  • Kukuza sauti za wanawake katika uongozi na maamuzi kwa ujumla
  • Kutambua mchango wa waandishi, wahamasishaji jamii na watengeneza maudhui katika kuleta mabadiliko ya kijamii.
  • Kuimarisha uhamasishaji wa jamii kuhusu umuhimu wa wanawake kushiriki katika uongozi na michakato ya kidemokrasia.

Utambuzi wa Waandishi, Wahamasishaji jamii na Watengenezaji wa maudhui

Tuzo hii itahusisha kazi zilizotolewa katika makundi yafuatayo:

Vigezo Muhimu vya Kuzingatia kwa waandishi wa Habari

·       Ubora wa kazi iliyowasilishwa.

·       Upekee wa mada.

·       Umuhimu wa kuzingatia uwiano sawa wa jinsia.

·       Vyanzo vingi vya habari vilivyojitawanya.

·       Ubunifu wa mada husika.

·       Matokeo baada ya kutoka kwa habari au kampeni hiyo (impact).

·       Uwasilishaji wa mada husika.

·       Mpangilio wa mada.

·       Ufasaha na mtiririko wa lugha.

·       Kuzingatia maadili ya uandishi wa habari.

·       Uweledi na matumizi ya takwimu.

Kipindi cha Redio na Televisheni kisizidi dakika 30, na sauti pamoja na picha ziwe katika ubora unaostahiki.

Kazi zinazowasilishwa lazima ziwe zimechapishwa au kurushwa hewani katika kipindi cha kuanzia Januari 1 hadi Disemba 31, 2025.

Mchakato wa Uwasilishaji na Tathmini:

Maombi yamefunguliwa leo na kazi zitaendelea kupokelewa hadi tarehe 13 Aprili, 2026.

Kazi zinaweza kuwasilishwa moja kwa moja katika Ofisi za TAMWA ZNZ zilizopo Tunguu - Unguja na Mkanjuni Chakechake - Pemba, au kupitia barua pepe ya info@tamwaznz.or.tz pamoja na kiungo kitakachotumwa kwenye mitandao ya kijamii.

Vigezo muhimu vya kuzingatia kwa watengenezaji wa maudhui (Content Creators).

  • Ubunifu na uhalisia wa maudhui
  • Uelewa wa mada na kufikisha ujumbe kwa usahihi.
  • Ubora wa uwasilishaji maudhui kwa kutumia lugha, picha au video.
  • Uwezo wa maudhui kuhamasisha uelewa au mabadiliko chanya kwa jamii.
  • Kuhakikisha maudhui yanafuata maadili na yanatoa taarifa sahihi.
  • Maudhui yaliyosambaa na kuwafikia watu wengi.

Vigezo Muhimu vya Kuzingatia kwa wahamasishaji jamii (Citizen Brigades)

  • Kwa upande wa wahamasishaji wa  jamii tunaowatumia kuhamasisha jamii kuhusu masuala ya wanawake na uongozi katika ngazi za chini, tuzo itatolewa kwa wilaya mbili zitakazojitokeza kwa utendaji bora zaidi, wilaya moja kutoka Unguja na wilaya moja kutoka Pemba.
  • Tathmini ya utendaji wao itazingatia kiwango cha juhudi za uhamasishaji walizozifanya, kiwango cha ushiriki wa jamii,
  •  Ubunifu wa mbinu walizotumia katika kufikisha ujumbe, pamoja na
  • Matokeo  chanya yaliyojitokeza katika jamii kutokana na shughuli hizo.
  • Uwasilishaji wa ripoti za kazi zao kwa wakati.
  • Majaji wa kazi:
  • Katika kuhakikisha malengo ya tunzo hizi, kutakuwa na jopo la majaji ambalo litakuwa na watu wenye sifa za ujuzi, uzoefu, usawa na uadilifu kutoka katika maeneo yote yanayoangaliwa.

Washindi wote watatambuliwa na kupewa tuzo siku ya tarehe 02 Mwezi Mei 2026, shughuli ambayo itawashirikisha pia wadau mbali mbali wa wanawake na uongozi.

 

Aidha amesema kuwa, Huu ni msimu wa tano wa utoaji wa Tuzo hizi kupitia grogram ya kuwajengea Wanawake uwezo katika Uongozi (SWIL) inayotekelezwa kwa mashirikiano na Ubalozi wa Norway (RNE). Tuzo hizi ni mwendelezo wa jitihada za kuongeza ushiriki wa wanawake katika uongozi na kuimarisha ushiriki wa kidemokrasia Zanzibar.

Mpaka sasa, jumla ya waandishi wa habari 53 pamoja na vyombo vya habari vitatu vimetambuliwa kwa kuandika na kurusha maudhui yanayochangia kuongeza ushiriki wa wanawake katika uongozi katika kipindi cha kuanzia mwaka 2021 hadi 2024.

Kwa maelezo zaidi, tafadhali wasiliana nasi kupitia info@tamwaznz.or.tz  au ngalapi@tamwaznz.or.tz

 

 


No comments

Powered by Blogger.