MGOMBEA UDIWANI JIMBO LA MFENESINI: BAHATI ALI – KIONGOZI MWENYE MAONO NA USHAWISHI WA KIJAMII
NA
MARYAM NASSOR,
“Kiongozi bora ni yule anayesimama na watu wake, si kwa maneno pekee bali kwa vitendo.” – Bahati Ali
Katika harakati za kisiasa na kijamii Visiwani Zanzibar, jina la Bahati Ali Rashid limekuwa
likibeba matumaini mapya kwa wananchi wa Jimbo la Mfenesini wadi ya Kihinani.
Ni kiongozi kijana mwenye maono mapana, anayejulikana kwa
msimamo thabiti, maadili mema, na moyo wa kujitolea kwa jamii yake.
Uongozi wake
umejengwa juu ya historia ya mapambano, changamoto, na mafanikio ambayo yamempa
sifa ya kuwa mmoja wa wagombea wanaopewa nafasi kubwa na wananchi wa jimbo hilo.
Taarifa
Binafsi
Bahati Ali alizaliwa katika familia yenye misingi ya utu na
mshikamano wa kijamii huko Kawe wilaya
ya Kinondoni mkoa wa Dar es salaam.
Ambapo alipata elimu yake ya msingi mwaka 1986 na sekondari
katika shule za serikali za jijini humo
kuanzia mwaka 1992. Na mwaka 1996 akamaliza masomo yake ya
Sekondari
kisha akaendelea na
masomo ya elimu ya juu ambapo alijikita zaidi katika masuala ya utalii,
maendeleo ya jamii na uongozi.
Tangu akiwa mwanafunzi, alionesha ari ya kuongoza na kupaza
sauti kwa ajili ya wanyonge, jambo lililomjengea heshima kubwa.
Uzoefu
wa Kisiasa na Uongozi
Bahati Ali amejiunga na siasa mwaka 2000 akiwa kijana
kupitia umoja wa vijana wa chama chake cha Mapinduzi (CCM) , akipitia ngazi
mbalimbali za uongozi.
Amewahi kushika
nafasi za juu katika jumuiya za vijana, kuwa katibu wa kamati za maendeleo, na
mshauri wa miradi ya kijamii katika jimbo la Mfenesini kwa nyakati tofauti.
Kupitia nafasi hizo,
amepata uzoefu wa kiutawala, uwezo wa kushirikiana na makundi mbalimbali ya
kijamii, na ujuzi wa kushughulikia changamoto zinazowakabili wananchi.
Mgombea huyo, wa udiwani jimbo la Mfenesini wadi ya
Kihinani amesema katika uongozi wake uliopita
akiwa kateuliwa katika kamati ya
utekelezaji ya Jumuiya ya wazazi wilaya hiyo mwaka 2020/ 25 aligombea
nafasi ya ubunge lakini kura hazikutosha na akatokea nafasi ya tatu.
Amesema kuwa, katika mambo anayojivunia katika uongozi wake uliyopita akiwa katika nafasi hiyo ya kuteuliwa katika jimbo hilo alifanikiwa
kushughulikia ujenzi wa ofisi za Chama ya wazazi .
Ushawishi
wa Kijamii na Maadili
Miongoni mwa sifa zinazomtambulisha Bahati Ali ni ushawishi
wake wa kijamii. Ni mtu anayekubalika kwa vijana, wazee, wanawake na watu
wenye ulemavu.
Awamu iliyopita
alikuwa kateuliwa katika
Kamati ya Utekelezaji ya Wilaya ya
ya jimbo la Mfenesini wadi ya Kihinani, ambapo amekuwa mstari wa mbele kushirikiana na
vikundi vya kijamii katika shughuli za maendeleo, kusaidia wahitaji, na
kusimamia miradi ya mazingira na afya ya jamii.
Amesema kuwa, katika
kipindi hicho,alishirikiana na viongozi
wenzake kufanya mambo mengi lakini pia
walifanikiwa kujenga ofisi nzuri ya chama ambayo wanaitumia katika shughuli
zao
“ Naamini kuwa
kiongozi bora lazima awe na maadili, uwajibikaji na uwazi kwa wananchi wake
lakini ajishushe kwa wananchi kutafuta changamoto zao na kuzifanyia kazi “
amesema .
Changamoto
za Uongozi na Mafanikio
Safari ya kisiasa ya Bahati Ali haijakosa changamoto.
Ameshuhudia upungufu wa rasilimali za kusaidia miradi ya kijamii, changamoto za
ajira kwa vijana, na wakati mwingine kukabiliana na upinzani wa kisiasa.
Hata hivyo,
changamoto hizo zimekuwa nguvu ya mafanikio yake. Amefanikisha
kuanzisha miradi midogo ya ujasiriamali kwa vijana na wanawake.
Aidha amesaidia kuboresha huduma za kijamii kama
maji safi na elimu, na pia kushirikiana na taasisi mbalimbali kuendeleza
maendeleo ya jimbo hilo .
Mitazamo
ya Kijinsia
Bahati Ali ni kiongozi anayetetea usawa wa kijinsia.
Anaamini kuwa wanawake ni nguzo muhimu katika maendeleo ya jamii na hawawezi
kuachwa nyuma.
Ameunga mkono
kuanzishwa kwa vikundi vya akina mama vya kiuchumi, kutoa nafasi sawa za
uongozi, na kushirikisha wanawake katika maamuzi ya kijamii na kisiasa.
Pia amekuwa bega kwa
bega na vijana wa kike kuhakikisha wanapata fursa sawa katika elimu na ajira.
Bahati Ali si mgombea tu wa udiwani wa Jimbo la Mfenesini,
bali ni taswira ya matumaini mapya kwa jamii yake. Uadilifu
wake, uzoefu wa kisiasa, mshikamano wa kijamii, na mtazamo wa kijinsia
unamfanya kuwa kiongozi anayeweza kuunganisha wananchi kwa maendeleo ya pamoja.
Ingawa amekumbana na changamoto kadhaa, mafanikio yake na
maono yake ya baadaye yanamfanya aonekane kama chaguo sahihi kwa wananchi wa
Mfenesini.
Watu wanaomfahamu mgombea huyo wanamzungumziaje.
Machano Othman Said ni Mgombea nafasi ya Uwakilishi jimbo
la Mfenesini anamzungumzia Bahati Ali Rashid ambae ni mgombea udiwani wa jimbo
hilo kama ni mwanamke mwenye ushawishi kwa jamii na anakubalika.
Amesema kuwa, katika kipindi kilichopita wakati Bahati
alikuwa katika Kamati ya kuteuliwa ya Jumuiya ya Wazazi, alifanya kazi
kwa mashirikiano mazuri na wakatekeleza miradi mingi ya maendeleo katika
jimbo hilo.
Ashura Yunus, mkaazi wa Mfenesini wadi ya Kihinani amesema
mgombea huyo ni mchapakazi anajitoa kwa wananchi lakini pia ni mtu ambaye hana
makundi katika chama.
“ Kwa kweli mgombea huyu
tunamkubali kwani ana maono makubwa na ni chaguo sahihi kwa wannchi wa kihinani “
amesema mwanchi huyo.
Mwisho

Post a Comment