TAMWA ZNZ, CFP NA CFI YAZINDUA TUNZO YA UANDISHI WA HABARI ZA TABIANCHI ZA 'COMMUNITY FORESTS'
NA
MWANDISHI WETU
CHAMA cha Waandishi wa
Habari Wanawake Tanzania - Zanzibar (TAMWA ZNZ) kwa kushirikiana na Community
Forests Pemba (CFP) na Community Forests International (CFI) kupitia mradi
wa Zanzibar Women’s Leadership in Adaptation (ZanzAdapt), kina furaha
kuwatangazia rasmi uzinduzi wa Tuzo “Uandishi wa Habari za Tabianchi za
‘Community Forests. Yenye kaulimbiu isemayo:“Kupaza Sauti za
Wanawake katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi”.
Akizungumza na waandishi
wa habari katika ufunguzi wa Tuzo hizo, huko katika ukumbi wa Chama hicho Tunguu , Mkurugenzi wa ( CFP ) Mbarouk Mussa Omar amesema
lengo la tunzo hizo ni kutatambua
mchango wa waandishi wa habari na vyombo vya habari Zanzibar vinavyoandika,
kurusha na kusambaza habari zinazoonesha mchango wa wanawake na
uongozi katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, hususan katika eneo la
mikoko, kilimo mseto himilivu cha tabianchi (climate-smart agriculture) na
kukuza usawa wa kijinsia kupitia kazi zao.
Amesema kuwa, Kupitia tuzo hizo, TAMWA ZNZ, Community
Forests Pemba na Community Forests international zinalenga, Kukuza uandishi wa habari unaoonyesha uongozi
wa wanawake katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Amesema lengo jengine la tunzo hizo ni Kutambua
mchango wa waandishi wa habari mahiri wanaoandika habari zinazohusu wanawake na
uongozi kwenye masuala ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi
- Kuhamasisha
uandishi wa habari unaozingatia usawa wa kijinsia, ushahidi wa kisayansi
na hadithi za mabadiliko chanya kutoka ngazi ya jamii.
- Kuongeza uelewa
wa jamii kuhusu mchango na uongozi wa wanawake katika kukabiliana na
mabadiliko ya tabianchi Zanzibar.
- Kuweka
mazingira ya ushindani kwa waandishi wa habari kuandika habari zenye ubora
na athari chanya kuhusu wanawake na uongozi na mabadiliko ya tabianchi.
Kwa nini Tuzo hizi ni Muhimu:
Nae, Manager wa Mawasiliano Kitengo cha Habari
TAMWA ZNZ, Sophia Ngalapi amesema ,Licha ya wanawake kuwa mstari wa mbele na
kutoa mchango mkubwa katika shughuli za kilimo-misitu (agroforestry), uhifadhi
wa mikoko, na mikakati mingine ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwa
kutumia mbinu za asili, lakini uongozi na mchango wao bado hauonekani vya
kutosha katika vyombo vya habari na kwa jamii.
Amesema kuwa, Uwakilishi mdogo wa wanawake
katika simulizi za vyombo vya habari haupunguzi tu nafasi yao ya kushiriki na
kuongoza, bali hupunguza mwonekano wa mikakati bora ya jamii katika kukabiliana
na mabadiliko ya tabianchi.
Aidha amesema kuwa, Utafiti
uliofanywa na mradi wa ZanAdapt Juni 2024 ulibaini kwamba, kati ya habari 4,548
kutoka vyombo vya habari mbalimbali ni asilimia 1.1 tu ya habari zilizojumuisha
sauti za wanawake na wasichana, na asilimia 0.4 pekee zilizoonyesha wanawake
kama viongozi katika muktadha wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Mradi ZanzAdapt,
unaotekelezwa na Community Forests International na Community Forests Pemba kwa
ushirikiano na TAMWA Zanzibar, unalenga kuziba pengo hili kwa kuhamasisha
uandishi wa habari unaozingatia usawa wa kijinsia na kutambua uongozi wa
wanawake katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Ili kukabiliana na
changamoto hii, Tuzo ya ““Uandishi wa Habari za Tabianchi za ‘Community
Forests”.Yenye kaulimbiu isemayo “Kupaza Sauti za Wanawake katika
kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi”. imeanzishwa kutambua mchango
wa vyombo vya habari na kuhamasisha waandishi wa habari kuongeza juhudi katika
kuandika habari za wanawake na uongozi katika kukabiliana na mabadiliko ya
tabianchi Zanzibar.
Kupitia mradi wa
ZanzAdapt, waandishi wa habari 30 (20 Unguja na 10 Pemba) pamoja na wahariri 20
wamejengewa uwezo kitaaluma ili waweze kuandika habari kwa ubora,
ambapo wameweza kuandika habari zaidi 242 zinazozingatia uongozi wa
wanawake katika kukabiliana na tabianchi. Tuzo hii inakuja kuthamini,
kuendeleza na kuongeza juhudi hizo.
Tunzo
hii itahusisha kazi zilizotolewa na waaandishi wa habari katika vyombo vya
habari vya aina nne (4) kama ifuatavyo:).
1. Uandishi wa makala katika
magazeti (feature articles).
2. Uandishi wa habari wa vipindi
katika redio (radio program).
3. Uandishi wa habari katika
Televisheni (TV program).
4. Uandishi wa makala katika
mitandao ya kijamii (feature articles in social media)
Kazi
zote lazima zionyeshe masuala ya mabadiliko ya tabianchi Zanzibar na ushiriki,
sauti na uongozi wa wanawake Zanzibar.
Tuzo maalumu: Pia
kutakuwa na tuzo maalum nne ambazo ni:
1. Kutambua
chombo cha habari kilichoonyesha uwajibikaji zaidi katika masuala ya wanawake
na uongozi katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Hivyo
vigezo vitakavyotumika ni kuangalia chombo cha habari kilichoongoza kuzalisha
habari zenye ubora zilizorushwa au kuchapisha zinazohusu uongozi wa wanawake
katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, kuonyesha jinsi kinavyolenga
kuenzi na kuimarisha sauti za wanawake katika masuala ya tabianchi na uwiano wa
kijinsia kati ya wafanyakazi.
2. Tuzo
ya mwandishi wa habari kijana wa habari za mabadiliko ya tabianchi (miaka 18-30).
Vigezo kwamba mwandishi yoyote kijana, mwenye umri kuanzia miaka 18 hadi 30
anayefanya kazi katika chombo cha habari cha gazeti,television, redio na
mitandao ya kijamii ambae ameandika habari inayohusu masuala ya wanawake na
uongozi katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
3. Tuzo
ya uandishi wa habari wa mitandao ya kijamii. Vigezo ni kwamba
kazi iwe imeangaliwa na watu wengi zaidi.
4. Tuzo
kwa habari iliyoangazia kwa ukubwa nafasi ya wanawake na uongozi
katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Vigezo muhimu vya
kuzingatia:
· Habari
za Wanawake na uongozi katika mabadiliko ya tabianchi
· Umuhimu
wa kuzingatia uwiano sawa wa jinsia
Usahihi wa taarifa na unaozingatia maadili ya uandishi wa habari
· Ubora
wa uandishi wa habari kwa picha (Visual Journalism Quality)
· Simulizi
ya kipekee ya mada husika
· Ubunifu,
uchunguzi bora wa mada
· Ufasaha
na mtiririko wa lugha
· Ubora
katika utayarishaji, sauti na uwasilishaji wa mada
· Ushawishi
na ushirikishwaji wa hadhiara mitandaoni
aKipindi
cha Redio na Television kisizidi dakika 30 na pia sauti na picha ziwe katika
ubora unaostahiki.
Kwa Vyombo vya Habari Pekee:
· Dhamira ya
chombo cha habari katika mabadiliko ya tabianchi
· Program zenye
ubunifu na ushirikishwaji wa jamii
Vigezo
kwa vyombo cha habari:
Chombo
cha habari kinapaswa kuwasilisha andiko/maelezo ya kurasa mbili ikionyesha
idadi na ubora wa habari au makala zilizochapishwa au kurushwa zinazohusu
uongozi wa wanawake katika mabadiliko ya tabianchi, kuonyesha jinsi
kinavyolenga kuenzi na kuimarisha sauti za wanawake katika masuala ya
tabianchi, uwepo wa mwandishi wa habari maalum anayeshughulikia masuala ya
mazingira na tabianchi miongoni mwa wafanyakazi wake, na uwiano wa kijinsia
kati ya wafanyakazi. Vilevile, vyombo vya habari vinaweza kuweka taarifa
nyingine yoyote wanayoiona inafaa ili kuimarisha maombi yao.
Mchakato
wa Uwasilishaji na vigezo vya tathmini.
Dirisha la
kupokea kazi liko wazi kwa waandishi wa habari wa Unguja na Pemba kutoka vyombo
vya habari mbalimbali kutuma kazi zao, ikiwemo magazeti, televisheni, redio, na
mitandao ya kijamii. Kazi zitakazopokelewa ni zile zilizochapishwa au kurushwa HEWANI kuanzia
tarehe 01 Juni 2024 hadi tarehe 31 Disemba 2025, na
lazima zihusishe:
- Masuala ya mabadiliko ya tabianchi Zanzibar;
- Wanawake na uongozi katika mabadiliko ya tabianchi Zanzibar
Maombi yamefunguliwa leo
na kazi zitaanza kupokelewa kwa muda wa siku 21 kuanzia tarehe ya leo hadi
tarehe 23 Januari hadi tarehe 14 Feburuari, 2026.
Waandishi wa habari
mtatakiwa kuwasilisha kazi mbili (2) ambazo zimezalishwa, kuchapishwa na
kurushwa HEWANI kwa kipindi kilichotajwa hapo juu kupitia
kiungo/link itakayotumwa kwenye mitandao ya kijamii au kuleta moja kwa moja
Ofisi za TAMWA ZNZ zilizopo Tunguu, Unguja na Mkanjuni Chakechake Pemba.
Jopo la majaji likiwa na
wataalamu wa uandishi wa habari na jinsia,pamoja na wataalamu wa masuala ya
mabadiliko ya tabianchi litapitia kazi zote zilizowasilishwa kwa
umakini mkubwa mara tu baada ya kufungwa kwa zoezi la uwasilishaji na ukusanyaji
kazi hizo.
Kazi zote
zitakazowasilishwa zitapitia uhakiki wa awali wa jumla na majaji ili
kuhakikisha zinakidhi vigezo vya msingi vifuatavyo:
1. Lugha ya kazi iwe Kiswahili au
Kiingereza.
2. Mwandishi wa habari awe na umri
wa miaka 18 au zaidi.
3. Kazi iwe imechapishwa ndani ya
kipindi kinachokubalika kwa mujibu wa kanuni za tuzo (kuanzia tarehe 1 Juni,
2024 hadi tarehe 31 Disemba, 2025).
4. Kazi ijikite katika masuala ya
mabadiliko ya tabianchi Zanzibar.
5. Kazi ionyeshe uongozi wa
wanawake wa Kizanzibari.
6. Kazi iwe katika moja ya makundi
ya vyombo vya habari yaliyobainishwa.
7. Mwandishi wa habari au chombo
cha habari kiwe na makao yake Zanzibar.
8. Kazi ikidhi vigezo vyote vya
majaji.
Tarehe ya Tuzo:
Hafla
ya utoaji wa tuzo inatarajiwa kufanyika tarehe 28 Machi 2026,
kuanzia saa moja usiku katika hafla itakayowakutanisha waandishi wa habari,
wahariri wa vyombo vya habari, wamiliki wa vyombo vya habari, taasisi za
kiserikali, zisizo za kiserikali, za kimataifa na wanajamii.
Hitimisho:
TAMWA
ZNZ, Community Forest Pemba na Community Forest
International tunawakaribisha waandishi wa habari na vyombo vya habari vya
Zanzibar kushiriki kikamilifu katika tuzo hizi, tuzo hizi ni jukwaa muhimu la
kuonesha nguvu ya uandishi wa habari katika kuleta mabadiliko ya kijamii na
kimazingira kwa kuzingatia usawa wa kijinsia na sauti za wanawake na uongozi
katika kukabiliana namabadiliko ya tabianchi ili kujenga uelewa kwa jamii na
kuleta mabadiliko chanya.
Tuzo
hizi ambazo ni mara ya kwanza kufanyika zimeandaliwa kupitia mradi wa Zanzibar
Women’s Leadership in Adaptation (ZanzAdapt) kwa mashirikiano na Serikali ya
Canada.
Kwa maelezo zaidi, tafadhali wasiliana
nasi kupitia: info@tamwaznz.or.tz & ngalapi@tamwaznz.or.tz.


Post a Comment