UKATILI WA KIJINSIA UNAVYOWATIA HOFU WAGOMBEA WAKIKE KUTOKA VYAMA VYA UPINZANI.
NA MARYAM NASSOR,
HUU ni mwaka
wa uchaguzi nchini Tanzania, ni miaka
mitano imepita tokea kufanyike uchaguzi wa mwisho wa mwaka 2020, lakini baadhi ya wagombea wanawake waliyo shiriki uchaguzi huo kutoka vyama vya upinzani, bado
wanauguza majeraha na vidonda visivyo poa vya kunyanyaswa na kupoteza ndugu zao wa karibu , watu wengi
waliyeruhiwa na wengine kupoteza maisha.
Halima ambae ana diploma
ya kozi ya ukarani, ni mama wa watoto watano, anaishi na mume wake
kisiwani Unguja, alianza safari yake ya siasa tokea miaka ya
1994, anaeleza jinsi alivyokutwa na
ukatili wa kijinsia wakati anagombea nafasi ya Uwakilishi mwaka 2020.
Hii, ni baada ya kutakiwa kutoka katika chumba cha kupigia kura na
watu ambao wanadaiwa kutoka vyombo
vya dola , akiwa ni mgombea wa
Uwakilishi kutoka ,Chama cha ACT
Wazalendo katika jimbo la Malindi lenye wadi mbili na shehia 11.
"Nilitolewa
katika chumba Cha kupigia kura, wakati Mimi nilikuwa ni mgombea halali wa uwakilishi katika Jimbo hilo mwaka 2020 na niliporudi
jioni kutaka kulinda kura zangu wakati niko njiani naelekea kituo vha kupigia kura alitokea askari mmoja akaniekea bunduki kifuani kwangu eti kunitaka nirudi nilipotoka," Anasimulia
Halima.
Amesema
kuwa, Wakati wa uchaguzi huo alivumilia ukatili wa kimwili , vitisho lakini
pia mara kadhaa alinusurika kupigwa
risasi na vikosi vya usalama ,“ Kiukweli wakati wa uchaguzi hapa kwetu Zanzibar
hali si shwari , vitisho ni vingi hasa kwa sisi tunaogombea katika vyama vya
upinzani,” anasema Halima .
Katika hali
kama hiyo, anasema vitendo vya ukatili
wanavyo fanyiwa wagombea wa upizani wakati
wa uchaguzi vinawavunya moyo, wanawake kurudi kwenye kinjanyanyiro' cha
kutafuta uongozi.
"Kila
nikikumbuka Jinsia nilivyotolea katika chumba cha kupigia kura, na kunyimwa
haki yangu ya kuangalia hesabu za kura zangu, na mwenzangu wa chama x akaachwa ashuhudie
kura zikihesabiwa, nilipata maradhi, " amesema Halima.
Kama Hali haitabadilika katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025, basi wanawake wengi wa vyama
vya upizani, hawatagombea kwani hali ile
inawavunjwa moyo kugombea nafasi za
uongozi, kutokana na ukatili unaowakuta wakati wa uchaguzi.
Hata hivyo,
huyo hakuwa pekee yake , ukatili wa
kijinsia kwa wanawake wakati wa uchaguzi ni suala linalowatafuna wanawake
wengi wa vyama vya siasa hasa kutoka vyama vya upizani, kama ulivyomkuta
Asiata Abubakar ( 40) .
Asiata Abubakar, ni miongoni mwa wanawake waliokumbwa na ukatili unaohusishwa na uchaguzi , ambae aligombania Ubunge katika Jimbo la kikwajuni Unguja, Kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), anasimulia ukatili wa kimwili na kisaikolojia
uliompata wakati wa uchaguzi mkuu mwaka
2020.
Anaeleza
kuwa, aliambiwa na vyombo vya dola,
atokee nje ya kituo cha kupigia kura,baada ya kushuhudia mtu anapewa
karatasi za kura zaidi ya moja." Ndipo nilipotolewa nje ya kituo cha kupigia kura, eti sijulikani kama mimi ni mgombea wa
ubunge katika Jimbo la kikwajuni "anasimulia Asiata.
Mwanasiasa
huyo, ambae aligombea ubunge katika uchaguzi huo anasema wagombea wa upizani wanapitia ukatili
na udhalilishaji kutoka kwa vyombo vya
dola , ambao wao hawahusiki na uchaguzi."Jukumu la kulinda uchaguzi ni la jeshi la Polisi na si la vyombo vya dola,
kwani wao ndio wanaovuruga uchaguzi’’ amesema Asiata.
Utafiti
uliyofanya na Taasisi ya kitaifa ya kidemokrasia -NDI ikishirikiana na Chama Cha Wandishi wa Habari
Wanawake Tanzania, Zanzibar TAMWA-ZNZ imesema
Zanzibar imekumbwa na vurugu zinazohusishwa na uchaguzi , hasa uchaguzi
wa mwaka 2020.
Ripoti,
iliyoandaliwa na Chama Cha ACT-Wazalendo, kuhusu matukio ya vurugu
zinazohusishwa na uchaguzi wa mwaka 2020, jumla ya matukio 343 ya
udhalilishaji yanayohusishwa wanaume 256 na wanawake 87 yalitokea wakati
wa uchaguzi, watu 14 walikufa na 55 walijeruhiwa kati ya Oktoba 26 hadi 30
mwaka 2020.
Tunu Juma
Kondo, ni Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) amesema
ni vyema wanawake wanaotia nia ya kugombea nafasi za uongozi, lazima wajidhatiti na wapambane katika kutafuta nafasi hizo, ili kuongeza wingi wao
hasa kugombea katika majimbo ambako huko wanawake bado wako kidogo.
“
Wanawake wanaotia nia ya kugombea nafasi
za Uongozi katika Uchaguzi Mkuu, lazima wajidhatiti na wawe majasiri ili kuingia katika nafasi za
uongozi” amesema Tunu.
Zanzibar
imesaini mikataba mbali mbali ya kumlinda mwanamke dhidi ya aina zote za
ukatili na udhalilishaji kama mkataba wa Cedaw ,Mkataba huu
umeanzishwa mwaka 1979, lengo la mkataba huo ni kumlinda mwanamke na
ukatili na Udhalilishaji unaowakuta lakini utekelezaji wa mkataba huo bado
unasuasua.
Kwa mujibu
wa ripoti ya sensa ya watu na makazi ya
Tanzania ya mwaka 2022, inaonesha kuwa
Zanzibar ina wakazi wapao milioni 1.8 kati ya hao wanaume ni 915,492 na wanawake ni
974, 281.
Hii ina maana kwamba, wanawake ni asilimia 51.6 ya wakaazi wote wa Zanzibar, lakini wingi wao huo hauonekani
katika nafasi za uongozi, kutokana na
mambo mengi lakini pia , ukatili wa kijinsia unaowakuta wanawake
kipindi cha uchaguzi.
Chama Cha
Wandishi wa habari Wanawake Tanzania
Zanzibar,(TAMWA, ZNZ) ni Taasisi isiyo ya kiserikali inayojishuhulisha
na utetezi wa haki za Mtoto wa kike, na
kuhamasisha wanawake kushiriki katika
nafasi za Uongozi Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo Dk Mzuri Issa, amesema Tume ya Uchaguzi ya
Zanzibar -ZEC inapaswa iwe na vikosi
maalumu vinavyolinda uchaguzi na viwe chini ya tume hiyo, ili kuepusha vurugu
wakati wa uchaguzi." Tumekuwa tukishuhudia vurugu na ukatili dhidi ya
wanawake wakati wa uchaguzi na kupelekea ushiriki mdogo wa wanawake katika
majimbo" amesema Dr Mzuri.
Ili kuengeza, ushiriki wa wanawake katika
nafasi za uongozi katika vyama vyote vya siasa , ni lazima tuwe na siasa safi
ambazo hazina vurugu. ‘’ Kama tunataka kuongeza wingi wa wanawake
katika nafasi za uongozi basi, ni lazima tuwe na siasa safi ambazo hazina
vurugu’’ amesema Dk Mzuri.
Mkurugenzi
waTume ya Uchaguzi Zanzibar -ZEC Thabiti Idarous Faina, amesema kuwa, tume ya Uchaguzi haina takwimu za makosa ya ukatili
na udhalilishaji unaotokea wakati wa uchaguzi,kwani takwimu hizo zinapelekwa
kituo cha Polisi." Kazi kubwa ya
tume ya Uchaguzi ni kusimamia shuhuli za
Uchaguzi, lakini haina takwimu za kesi za Udhalilishaji unaotokea wakati wa
Uchaguzi ‘’ amesema Faina.
Ziko Mamlaka
ambazo zinahusika na maswala ya ulinzi
na Usalama kwa raia na mali zao, Mkuu wa jeshi la Polisi Mkoa wa Kusini Unguja, SP Daniel Shila,
amesema jeshi la Polisi limejipanga
na litaendelea kulinda rai na mali zao
kama inavyowataka sheria ya jeshi
hilo sura ya 322.
Katika kuhakikisha wanawake wanashiriki kikamilifu katika
kugombea nafasi za uongozi, amesema kuwa
watasimamia sheria za nchi kwani hakuna mtu aliye juu ya sheria.
‘’Tutamchukulia hatua mtu yoyote ambae, atahusika na vurugu kipindi cha
uchaguzi, ikiwemo watakao toa maneno machafu kwa wagombea wanawake, hivyo
tunatoa wito kwa jamii , mgombea yoyote wakike atakaefanyiwa vurugu wakati wa
uchaguzi , aje kuripoti na tutachukuwa
hatua’’ amesema SP Shila.
Post a Comment