“NCCR–Mageuzi Yazindua Kampeni, Yaahidi Kurejesha Mitaji ya Wajasiriamali Walioathiriwa na Mikopo Kaushadamu”


NA MARYAM NASSOR,

MGOMBEA Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha NCCR Mageuzi – Leila Rajab Khamis,  amesema kama akipata ridhaa ya kuiongoza Zanzibar atarudisha mitaji kwa wajasiamali waliochukuwa mikopo ya kaucha damu na kuuwa mitaji yao.

Ameyasema  hayo, huko katika viwanja vya Kibanda Maiti mkoa wa Mji Unguja  katika ufunguzi wa kampeni za chama hicho.

Amesema ,  katika mazingira ya Zanzibar  eneo moja la kukuza uchumi ni kuweka  mazingira wezeshi kwa wajasiriamali na kukuza  mitaji yao bila ya kujihusisha na mikopo umiza.

 Amesema kuwa, masoko yamekuwa yakijengwa lakini wafanyabiashara wadogo wamekuwa wakisahauliwa na badala yake wanachukuwa mikopo ya kausha damu na kuuwa mitaji yao.

“ Sote tumekuwa tukishuhudia  wafanyabiashara wa kibanda Maiti wametolewa  Mjini na kuletwa hapa ambapo mvua zikinyesha soko linageuka bwawa la kuogelea lakini mukinipa ridhaa nitalijenga soko hili ndani ya siku 100 za utawala wangu “ amesema mgombea  huyo.

Ameeleza kuwa, ameona jitihada za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ya kujenga Mahospital lakini bado changamoto ya Afya iko pale pale Madaktari hakuna.

Amesema kuwa, Moja ya kipaumbele chake katika chama chao ni kuboresha huduma za afya na atahakikisha anawapeleka wanafunzi wa kada ya afya kusoma nje ya nchi na kila mmoja ataajiriwa karibu na sehemu anayotoka .

“ Nitachohitaji  kutoka kwenu nyinyi wazanzibar wenzangu ni kunipa ridhaa ya kuwatumikia ili kuhakikisha naimarisha kila sekta muhimu kwa jamii yetu “ amesema.

Nae, Mgombea Mwenza wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Everiny Munis  akimnadi  mgombea huyo amesema , wanataka uongozi kwa sababu wamejipanga  kuleta mageuzi ya kila sekta ikiwemo  kwenye  siasa,  afya  na kiuchumi nchini.

Amesema kuwa, Zanzibar ni tajiti na imejaaliwa utajiri wa kutosha unaotokana na Bahari na Uchumi wa buluu lakini hakuna anaonufaika nao.

“Tunataka kuleta mageuzi  kwa  kuwa na Uvuvi wa kisasa na Uchumi jumuishi  kila mmoja afaidike kutokana na  utaalamu alionao , suala la ajira halitokuwa tatizo endapo mutaichagua NCCR Mageuzi “ amesema

Nae,  Naibu Katibu Mkuu  wa chama hicho kwa upande wa Tanzania bara, Martin Bernad amesema kwa mujibu wa Msajili wa vyama vya siasa nchini Tanzania vyama vyote 19 ni halali kugombea na kushinda.

Amesema kuwa, akimnukuu Rais wa kwanza wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania  Mwalim Julius  Kambarage Nyerere amewahi kusema kuwa, nchi inahitaji mambo manne ili iendelee.

Akiyataja mambo hayo, la kwanza amesema ni watu,  la pili ni ardhi, la tatu ni siasa safi na la nne ni uongozi bora , baadhi ya mambo hayo yapo lakini siasa safi na uongozi bora utapatikana endapo wananchi watakichagua chama hicho.         

Aidha akiwanadi wagombea Ubunge, Uwakilishi na Udiwani wa Chama hicho amesema watanzania kama wanataka kuchagua wanataka muungano wa namna gani basi  wakichaguwe chama hicho.

“ Sote tunajua suala la Muungano wetu haliwezi kuwa ni maamuzi ya chama  Fulani ni muhimu wananchi wenyewe tuamuwe muungano wa namna gani tunautaka hivyo hayo yatafikiwa endapo mutakichaguwa chama chetu “ amesema  Naibu Katibu Mkuu huyo.

                                 Mwisho

No comments

Powered by Blogger.