WANAWAKE WANAHITAJI NAFASI ZA UONGOZI ILI KULETA MABADILIKO NCHINI,
Na Maryam Nassor
Katika jamii ambayo mara nyingi nafasi za uongozi huonekana kama ni ngome ya wanaume, si jambo jepesi kwa mwanamke
kunyanyuka na kudai nafasi yake.
Ni safari
ngumu inayohitaji uvumilivu, ujasiri na kujitolea bila kuchoka, Njia hiyo ndefu
imewafanya wengi kukata tamaa, wakihisi mzigo huo una changamoto kubwa kuliko
ndoto zao.
Hata hivyo, wapo wachache waliothubutu kusonga
mbele bila kuyumbishwa na vikwazo. Kwa uthubutu huo wameweza kubadilisha
mitazamo y a muda mrefu kwamba uongozi ni eneo la wanaume pekee, na kuonesha
kuwa nafasi hiyo ni ya wote wenye maono na uwezo wa kuongoza.
Katika taswira hiyo, Machavu Bakar Juma ameibuka kama sauti mpya
inayothibitisha kuwa uongozi si suala la jinsia, bali ni uwezo, maono na
dhamira ya kweli ya kuwatumikia wananchi.
Kupitia
Chama cha ACT-Wazalendo, Machavu ameonesha matumaini mapya kwa jamii yake na wananchi
wa Zanzibar kwa ujumla.
Machavu ambaye alizaliwa miaka ya 1965
huko Mjimbini wilaya ya mkoani Kisiwani
Pemba, katika familia ya Mzee Bakar Juma akiwa ni mtoto wa nne wa Familia hiyo.
Elimu yake ya msingi na sekondari aliipata
katika skuli ya Muembe Makumbi, kabla ya kuendelea na masomo ya sekondari katika skuli ya
Darajani, Mjini Unguja.
“Nilipokuwa skuli, ndoto yangu kubwa ilikuwa kuona wanawake wakishiriki katika
siasa si kama wapiga kura pekee, bali kama watunga sera na watekelezaji wa
mabadiliko,” amesema Machavu.
Elimu hiyo ilimfungulia milango ya ajira katika chama cha CUF ambapo alihudumu katika
nafasi ya Mwenyekiti wa Wilaya ya Mjini
na Mjumbe wa Kamati kuu ya chama Taifa.
Mwaka 1992, alijiunga rasmi na siasa kupitia Chama cha Wananchi CUF,
kilichojulikana kwa msimamo wake wa haki, uwazi na uwajibikaji. Safari yake ya
kisiasa ilianza kuchukua mwelekeo mpya .
Machavu hakupata mafanikio mara moja. Mwaka 2010 aligombea uwakilishi wa nafasi
maalum za wanawake, lakini hakufanikiwa.
Mwaka 2015 alijitosa tena kwenye nafasi ya
uwakilishi lakini kura hazikutosha. Hata hivyo, juhudi zake hazikuishia hapo na
mwaka 2020 aligombea uwakilishi wa nafasi za viti maalum na uchaguzi
ulighairishwa.
Lakini, Kupitia mafunzo aliyopata kuhusu wanawake na
uongozi kutoka Chama cha Waandishi wa
Habari Wanawake TAMWA ZNZ yalimjenga na kumfanya kuwa na ndoto kubwa ya kugombea katika jimbo .
“ Baada ya
kupata mafunzo mara kwa mara ya wanawake na uongozi kutoka taasisi mbali
ikiwemo TAMWA ZNZ, nimeshawishika kugombea kwenye jimbo na ndoto yangu hiyo
imetimia” amesema Bi Mashavu.
Mashavu ambaye ni mgombea Ubunge jimbo la
Chumbuni kupitia chama cha ACT Wazalendo,
chama ambacho amejiunga mwaka 2020 baada ya kuhudumu kwa miaka 19 katika
chama cha CUF.
Amesema, wanawake wana uwezo mkubwa kuliko
wanaume katika kuongoza kwani wanayajua madhila yanaowafika wananchi
na wana hamuya kuitumikia jamii.
Maashavu ambaye kwa sasa anakaimu nafasi ya
Katibu Mwenezi Mahusiano ya Umma Ngome ya Wanawake ACT Wazalendo Tanzania nzima , amesema ana
uzoefu mzuri wa kuongoza na kuwatumikia wananachi.
“ Kupitia nafasi nyingi nilizohudumu nimepata uzoefu mkubwa wa kuwatumikia
wananchi wezangu wa Zanzibar hivyo
najiamini kugombea nafasi hii “ amesema .
Kama kiongozi mwanamke, Machavu amekutana na changamoto nyingi zikiwemo ukosefu
wa mtaji wa kisiasa na mitandao ya muda mrefu ambayo mara nyingi hutumiwa na
wanasiasa wakongwe.
Katika mazingira ya siasa za Zanzibar, ambako
mara nyingi zinatawaliwa na mifumo dume ,
mwanamke kugombea nafasi ya uongozi si jambo rahisi .
“Wapo waliokuwa wakiniambia siwezi kufanikisha ndoto zangu kwa sababu mimi ni
mwanamke na sina uzoefu mkubwa wa siasa. Lakini niliona ni lazima kubadili
mtazamo huo kwa vitendo, si maneno,” amesema Machavu.
Kwa Machavu, siasa si jukwaa la kujitafutia heshima binafsi, bali ni njia ya
kubadilisha maisha ya wananchi.
“Siasa ni dhamana. Kila kura ya mwananchi ni ahadi kwamba nitafanya kazi kwa
niaba yao, si kwa faida yangu binafsi,” amesema.
Kwa mujibu wa Katibu Mwenezi wa chama cha ACT Wazalendo Salim Diman , anamzungumzia Mashavu kama kiongozi muelewa , mchapakazi na mpenda maendeleo ambaye amepata mafunzo ya uongozi sehemu mbali mbali ikiwemo TAMWA ZNZ.
“Machavu ni kiongozi ambaye ni mpigania demokrasia na mpenda Maendeleo anawakilisha kizazi kipya cha wanasiasa wanaoamini kwenye hoja na uwajibikaji zaidi kuliko siasa za majukwaa na kelele “ anasema Salim.
Fatma Kassim, mkaazi wa Chumbuni, anamwona Machavu kama ushahidi kwamba
wanawake wanaweza kushika nafasi kubwa za uongozi iwapo watapewa nafasi na
kuaminiwa.
“Ni mfano wa kiongozi anayechanganya
elimu, maadili na maono ya kisiasa, katika wakati ambapo jamii nyingi bado
zinahofia kuwapa wanawake uongozi,” amesema Fatma .
MWISHO

Post a Comment