Wanawake si wafuasi tu wa siasa, bali ni wabeba mabadiliko ya jamii – Nadhra Ali Haji.
Na Maryam Nassor
Katika historia ya kisiasa ya Zanzibar, nafasi ya wanawake
mara nyingi imekuwa haionekani
ipasavyo, Lakini kila kizazi
kimekuwa na mashujaa wake waliothubutu kuvunja ukuta wa kimya.
Miongoni mwao ni Nadhra Ali Haji, mgombea ubunge wa
Jimbo la Malindi kupitia Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC).
Ujasiri wake, uzoefu wa kisiasa na dhamira ya kuimarisha ushiriki wa wanawake
katika maendeleo ni kielelezo cha kiongozi wa kizazi kipya.
Safari yake ya kisiasa, uzoefu wa uongozi na mtazamo wa
kijinsia ni kielelezo cha namna wanawake wanavyoweza kuchangia maendeleo ya
jamii na taifa kwa ujumla.
MAISHA YAKE BINAFSI
Nadhra Ali Haji alizaliwa mwaka 1970 Mtaa wa
Vikokotoni Mjini , Unguja Zanzibar.
Akiwa mtoto wa familia yenye maadili ya heshima na mshikamano, alikulia
katika mazingira yaliyochanganya historia, utamaduni na harakati za kijamii,
hali iliyompa msingi wa mapema wa kujiamini na kujitolea.
Elimu yake ameanzia katika Shule ya Msingi Tumekuja kisha akaendelea na masomo ya
sekondari katika Shule ya Ben bembela.
Kwa wakati huo baada
ya kumaliza elimu yake ya Sekondary alikwenda kujiunga na kikosi cha Idara ya anga
ambapo elimu hiyo ilimjengea
msingi imara wa kuunganisha taaluma na vitendo katika uongozi.
SAFARI
YAKE YA KISIASA
Nadhra Ali Haji alijiunga rasmi na chama cha CUF
mwaka 1993, kipindi ambacho chama hicho kilikuwa kinapanua wigo wake
katika harakati za kidemokrasia nchini.
Safari yake ya uongozi imenza akiwa mwanachama mdogo kabisa katika chama wananchi CUF , ambapo alikuwa ni katibu katika tawi la Shangani na Mji mkongwe Unguja.
Amesema na baadae
mwaka 1995 akiwa Pemba
alihamasika kugombea nafasi ya viti
maalum kura zilifungana yeye na mwenzake
, lakini kutokana na umri mdogo aliokuwa nayo
alikuwa hajui baada ya kushinda
atakuwa nani hivyo nafasi hiyo akamuachia menziwe.
“ Najivunia sana
katika siasa mimi niliazia tawi ambapo nilikuwa
muhamasishaji mzuri wakati mwengine nilifuatwa na watu wa chama cha
Mapinduzi nijiunge na chama hicho” amesema Bi Nadhra.
Akiwa mwanachama wa mwanzo kabisa, alikuwa katibu wa tawi la
mji Mkongwe na alishiriki moja
kwa moja katika mikutano ya hadhara, warsha za mafunzo, na mijadala ya kisiasa
iliyojikita katika kutafuta misingi imara ya chama.
Kutokana na mabadiliko ya mfumo na viongozi kwa chama hicho mwaka 2024 Nadhra
alijiunga na chama cha ADC na alijipatia umaarufu mkubwa kama mwanasiasa
mwenye msimamo thabiti, aliyejenga hoja zenye mashiko na mwenye mtazamo mpana
kuhusu nafasi ya mwanamke katika siasa.
UZOEFU WAKE KATIKA KUSHIRIKI UCHAGUZI.
Kabla ya kugombea Ubunge wa Jimbo la Malindi mwaka huu,
Nadhra aliwahi kushiriki uchaguzi wa
mwaka 2010 akiwa katika
chama cha wananchi CUF, ambapo alisimama kugombea nafasi ya viti maalum katika chama hicho ingawa
hakushinda.
Aidha,
mwaka 2015 alijaribu tena kugombea nafasi ya ubunge kupitia chama
hicho, lakini hakuweza kufanikisha ushindi kutokana na changamoto za kisiasa za
wakati huo.
Hata hivyo, kushiriki kwake katika chaguzi hizi kumemjengea
uzoefu wa kisiasa, uimara wa kisaikolojia, na uelewa wa karibu wa changamoto
zinazowakabili wapiga kura wake.
MTAZAMO
WA KIJINSIA .
Nadhra Ali Haji ni miongoni mwa viongozi wachache
wanaoamini kwamba maendeleo ya kweli ya Zanzibar hayawezi kufanikiwa bila
ushiriki wa wanawake.
Amesema kuwa ,wanawake hawapaswi kuachwa nyuma katika siasa
, elimu, uchumi na afya ambapo anapigania
uwezeshaji wa wanawake kiuchumi kupitia vikundi vya mikopo midogo midogo
na mafunzo ya ujasiriamali.
Amesema kuwa, Elimu ya mtoto wa kike ni muhimu akiamini kwamba elimu ni daraja la
kumtoa mwanamke kwenye umasikini na utegemezi.
Aidha amesema kuwa, Ushiriki wa
wanawake katika uamuzi wa kisiasa, ni
muhimu huku akihimiza vyama vya siasa na
serikali kutenga nafasi zaidi kwa wanawake kwenye ngazi za uongozi.
Kupitia nafasi yake ndani ya ADC ya
Mwenyekiti wa wanawake katika chama hicho amekuwa
mstari wa mbele kuhamasisha wanachama wanawake kushiriki kikamilifu kwenye
mikutano, warsha na kampeni.
MALENGO YAKE YA BAADAE.
Iwapo atapata ridhaa ya wananchi, Nadhra ameahidi kusukuma
ajenda zifuatazo , Kwanza Kuimarisha huduma za elimu na afya kwa wanawake na Watoto
katika jimbo hilo.
Ameseme kuwa atawawezesha
vijana na wanawake kwa miradi ya kiuchumi na maendeleo kwa kuanzisha viwanda vidogo vidogo katika jimbo hilo.
Aidha kutoa
huduma ya mikopo nafuu kwa wanawake na wanaume wajasiriamali ili
kujikwamua kiuchumi.
“ Nitahakikisha nasimamia uwakilishi wa wanawake na vijana
katika nafasi za maamuzi jimboni ‘’ amesema .
WATU WANAOMFAHAMU
WANAMZUNGUMZIAJE.
Mtumwa Feisal mgombea ubunge jimbo la Chumbuni kwa tiketi ya chama hicho, amesema Nadhra Ali Haji si tu mgombea wa ubunge
ni alama ya matumaini mapya kwa Malindi.
’’ Kiukweli Nadhra ni mgombea shupavu
mwenye maono na mapenzi ya kweli kwa wananchi na mpenda maendeleo ni alama ya matumaini kwa wana Malindi” amesema.
Amesema kuwa, tangu alipojiunga na ADC , safari yake imekuwa
ni ushahidi na ujasiri wa mwanamke
anayeamini kwamba siasa ni chombo cha maendeleo ya kijamii.
Nae, Abdallah Ali mwanachama wa chama hicho amesema Mgombea
huyu anabeba matumaini ya wanawake na wanaume wa Malindi, akiwakilisha kizazi
kipya cha wanasiasa wenye nia ya dhati ya kulijenga taifa kwa mshikamano na
mshikikano wa kijinsia
Amesema kuwa, Kwa
wananchi wa Malindi Nadhra anawakilisha
siasa zenye maono siasa zinazojali
jinsia na siasa zinazolenga maendeleo
kwa wote.
“ Ushindi wake unaweza kuwa si ushindi binafsi, bali ni
ushindi wa wanawake wote wa Zanzibar wanaopigania nafasi ya kusikika na
kushirikishwa “ amesema .
Mwisho

Post a Comment