SHERIA NZURI YA HABARI NI HAKI YETU TUENDELEE KUFANYA UCHECHEMUZI -TAMWA ZNZ
NA MARYAM NASSOR
CHAMA Cha
Wandishi wa Habari Wanawake Tanzania Zanzibar (TAMWA ZNZ) kimewataka wandishi
wa Habari kuendelea kufanya uchechemuzi
wa sheria rafiki za Habari ili zipatikane kwa haraka.
Akizungumza
katika kikao cha wadau wa Maswala ya Habari na wandishi wa Habari huko katika Afisi za
chama hicho Tunguu , Afisa Programu wa
sheria za Habari kutoka chama
hicho Zaina Mzee
Amesema , ingawa mradi huo wa uchechemuzi wa
maswala ya sheria za Habari unamaliza muda wake lakini wandishi waendelee kuandika Habari na Makala ili wenye mamlaka waendelee
kusikia kilio cha wandishi.
“Mradi huu
ulikuwa ni wa miaka miwili tu na
unamalizika, ikiwa sheria hiyo haijapatikana
lakini hatua kubwa tumepigwa kwa wandishi wa Habari wamepata uwelewa na
wenye mamlaka wamesikia kilio chetu”
Amesema kuwa,
ingawa sheria hiyo haijapatikana lakini hatua kubwa imepigwa kwani wandishi wa Habari wamepata uwelewa kuhusu kutetea zao na haki za wananchi.
“ Mradi huu
unamalizika lakini umeonesha mafanikio makubwa kwani kule Pemba wandishi
wamepata uwelewa mzuri hadi kuzuia
mchele mbovu wasiuziwe wananchi “ amesema Zaina.
Amesema
kuwa, Lakini kitu kizuri zaidi
Waziri pia kasikia kilio cha wandishi wa Habari cha kutaka mabadiliko ya
sheria za Habari, kutokana na kuwa ni ya muda mrefu na ina vipengele ambavyo
vinapinga uhuru wa Habari na kujieleza.
“ Mara nyingi Waziri katika vikao vyake amekuwa akilizungumzia suala hili la sheria za Habari tunaamini amesikia kilio chetu cha muda mrefu na atalifanyia kazi “ amesema.
Nae, Mjume wa Bodi ya TAMWA ZNZ Bishifaa Said , akimuwakilisha Mkurugenzi wa Chama hicho Dk Mzuri Issa, amewashukuru
wandishi wa Habari kwa kazi nzuri
waliyoifanya ya kufanya uchechemuzi wa sheria za Habari.
Amesema
kuwa, hatua kubwa imepigwa kutokana na
mradi huo waandishi wamepata uwelewa mzuri wa maswala ya sheria zinazominya
uhuru wa Habari.
“ Mradi unamalizika lakini waandishi wanaendelea kuwepo na kufanya kazi zao, hivyo ni vizuri wazidi kufanya uchechemuzi ili sheria nzuri ya Habari ipatikane” amesema Bishifaa.
Mohamed Hatib Mohamed ni Afisa Tathimini na
Ufuatiliaji kutoka TAMWA ZNZ, amesema ,
jumla ya Habari na Makala 253 zimeandikwa katika mradi huo, 104
zikiandikwa kwa upande wa redio, 17
makala za gazeti na 132 habari za
mitandao ya kijamii na blog.
Aidha amesema kuwa, mafanikio makubwa yamepatikana lakini pia isiishie hapo wandishi waendelee kufanya kazi ili mwisho wa siku sheria hiyo ipatikane.
Nao, baadhi ya wandishi walioshiriki katika
kikao hicho Huwaida Nassor amesema kupitia mradi huo, pia imewasaidia
wandishi wa Habari kurudi vyuoni kusoma ili itakapo patikana sheria hiyo isijeikawabane kufanya kazi zao kwa kutotimiza masharti ya elimu.
MWISHO





Post a Comment