WAANDISHI WA HABARI WA ZANZIBAR WAPATIWA MAFUNZO YA ULINZI NA USALAMA
NA MARYAM NASSOR
WAANDISHI
wa Habari wa Zanzibar wamepatiwa mafunzo ya ulinzi na usalama kuelekea uchaguzi mkuu
wa Oktoba mwaka, kipindi ambacho
mara nyingi huwa hatarishi kwa wandishi wa Habari.
Mafunzo hayo , ya ulinzi na usalama yametolewa August 6 na 7 , 2025 huko katika Afisi za TAMWA ZNZ Tunguu , na
mkufunzi Maryam Nassor ambaye ni mwandishi wa Habari baada ya kujengewa uwezo na Umoja wa klabu za Waandishi wa habari Tanzania ( UTPC) akimuwakilisha ToT Najjat Omar kutoka klabu ya
wandishi wa Habari Zanzibar ( ZPC).
Amesema
, waandishi wa Habari wanapaswa kuwa makini
na kuchukuwa tahadhari kwa
kujilinda wakati wote kwani ulinzi na
usalama wa mwandishi huanza na mwandishi mwenyewe.
Amesema kuwa, ulinzi na usalama wa mwandishi wa
Habari unaanza na yeye mwenyewe hivyo ni lazima kutambua mazingira anayofanyia kazi na watu
anaofanya nao kazi , ili kujihakikishia ulinzi
na usalama wake wakati akiwa
kazini.
“ Waandishi wa Habari lazima muwe makini katika kipindi hichi tunachoelekea kwani musipokuwa makini munaweza kuingia kwenye matatizo na kuhatarisha maisha yenu “ amesema mkufunzi huyo.
Aidha
amewataka wandishi wa Habari kujilinda
pia katika mitandao ya kijamii na kujiepusha kufungua viunganishi ( links) ambavyo
sio salama na hawajui vinapotoka.
Amesema kuwa, ni
vyema wandishi wa Habari kulinda taarifa zao binafsi zisifike kwa watu wasiohusika ili kuzuwia udukuzi na wizi wa taarifa.
Nao baadhi ya wandishi waliyobahatika kupata mafunzo hayo, Jesse Mikofu kutoka gazeti la mwananchi Zanzibar ameshauri ni vyema elimu kama hiyo kupewa na wamiliki wa vyombo vya Habari ili kusaidia kuwapatia vitendea kazi ambavyo vitasaidia kuwalinda.
Amesema kuwa, vyombo vingi vya Habari hawahamasishi waandishi wao, kuwa na vifaa vya kujilinda kama Press Jacket na vyenginevyo wakati wa majanga.
Nae, mwandishi Samira Abdalla kutoka Zanzibar University online Tv , ameshukuru kupatiwa mafunzo hayo ya ulinzi na usalama hasa kuelekea kipindi hichi cha uchaguzi, na kuahidi kuyafanyia kazi.
Mafunzo hayo ya siku mbili, ya ulinzi na usalama wa kimwili , kidigital na Afya ya akili kwa waandishi wa Habari yanalenga kuimarisha ulinzi na usalama kwa wandishi wa Habari kuelekea kipindi cha uchaguzi.
mwisho




Post a Comment