TAMWA ZNZ KUADHIMISHA SIKU YA REDIO DUNIANI KWA KUWAKUTANISHA WADAU WA HABARI.
NA MARYAM NASSOR,
CHAMA cha
Wandishi wa Habari Wanawake Tanzania Zanzibar (TAMWA ZNZ) kimeeleza dhamira yake ya kuitumia siku ya Kimataifa ya Redio kama jukwaa la kutathimini mchango wa redio katika maendeleo ya jamii,
hususani dhidi ya mapambano ya mabadiliko ya tabianchi.
Katika kuadhimisha siku hiyo ,TAMWA ZNZ inatarajia kuwakutanisha wadau mbali mbali wa
Habari kutoka sekta ya Habari
kwa Unguja na Pemba, wakiwemo
viongozi wa vyombo vya Habari,wahariri, wakuu wa vipindi , wandishi wa
Habari na viongozi wa vyombo vya Habari kwa lengo la
kujadili nafasi ya redio katika kuelimisha na kuchochea mijadala kuhusu mabadiliko ya tabianchi.
Kwa Mujibu
wa Mkurugenzi wa TAMWA ZNZ, Dkt Mzuri Issa, kauli mbiu ya mwaka huu” Redio na
Mabadiliko ya Tabianchi” inalenga
kuhamasisha vyombo vya Habari kutumia redio kama nyenzo ya
kuelimisha jamii kuhusu athari za mabadiliko ya Tabianchi na njia za kukabiliana nazo.
TAMWA ZNZ
inasema kuwa, licha ya umuhimu wa redio katika kufikisha taarifa, tafiti zinaonesha
kuwa redio bado haijatumika
ipasavyo kuzungumzia maswala ya tabianchi , utafiti uliyofanya mwaka 2024 na chama hicho
umebaini kuwa kati ya vipindi 2,600
vilivyorushwa na ZBC na Assalam Radio ni vipindi 11 pekee (asilimia 0.9)vinavyohusu mabadiliko ya tabianchi.
“Tafiti
zinaonesha kuwa sauti za wanawake
hazipewi nafasi ipasavyo katika mijadala ya tabianchi, hivyo tunaomba redio na vyombo vya Habari vyengine kuandika zaidi kuhusu wanawake
na nafasi yao katika kupambana na mabadiliko ya tabianchi” amesema Dkt
Mzuri.
Kwa mujibu
wa TAMWA ZNZ, Redio ina nafasi muhimu katika kuelimisha jamii
kuhusu athari za mabadiliko ya
tabianchi, kuhimiza matumizi ya mbinu endelevu za kilimo, uhifadhi wa
mazingira, na kupunguza uchafuzi wa mazingira.
Mbali na
suala la tabianchi, TAMWA ZNZ inasisitiza
kuwa redio inaendelea kuwa chombo
Madhubuti cha kupigania haki za
wanawake na Watoto, usawa wa
kijinsia na ushiriki wa wanawake katika uongozi.
Katika mwaka 2024 pekee, TAMWA ZNZ ilichapisha
Habari 778 kupitia vyombo mbali mbali vya Habari zikiwemo 101 kwenye redio, Habari hizo zilihusu
maswala kama vile udhalilishaji wa kijinsia , Afya ya uzazi, wanawake katika uongozi na uhuru wa Habari.
TAMWA ZNZ
inatoa shukrani kwa vyombo vya Habari
kwa mchango wao mkubwa katika kuhakikisha jamii inapata taarifa sahihi kwa wakati, chama hicho kinapongeza
juhudi za redio kufikisha ujumbe kwa jamii, hasa katika maeneo ya pembezoni
ambapo vyombo vingine vya Habari vinafika kwa ugumu.
Siku ya
Kimataifa ya redio huadhimishwa Febuary
13 kila mwaka tangu ilipotangazwa
rasmi na UNESCO mwaka 2011 na kupitishwa
na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwaka
2013, TAMWA ZNZ inazitakia redio zote madhimisho mema na mafanikio katika mipango yao ya baadaye.

Post a Comment