WATOTO WA KIKE ITUMIENI MICHEZO KAMA NJIA YA KUJILINDA- TAMWA ZNZ.
NA MARYAM NASSOR
WATOTO wa kike na wasichana wametakiwa kuitumia michezo kama njia moja wapo ya kujikinga na kujilinda na vitendo vya Ukatili
na Udhalilishaji wa kijinsia.
Wito huo, umetolewa na Afisa wa mradi wa
michezo kwa maendeleo kutoka chama cha wandishi wa habari wanawake Tanzania
Zanzibar, ( TAMWA ZNZ) Hairat Haji huko katika ukumbi wa Bima mipirani Unguja,
katika madhimisho ya siku 16 za kupinga udhalilishaji.
Akisoma
ripoti ya majumuisho ya vitendo vya
ukatili wa kijinsia kutoka January hadi
oktoba mwaka huu 2024, alisema zinaonesha hali ya kutisha, kwa kuongeza kwa vitendo hivyo kati ya kesi 1,582 za ukatili wa kijinsia ziliripotiwa na waathirika watoto walikuwa 1,337 kati ya
hao, wasichana walikuwa ni 1,095 na wavulana 242.
Aidha Afisa
huyo, alisema kuwa kesi 693 zilihusisha
watoto wa umri kati ya miaka 15 hadi 16
huku akitanabahisha kuwa, vitendo hivyo hufanyika kati ya saa 9:00 jioni na saa tatu usiku. Wakati muda huo watoto
wengi wapo mazingira ya nyumbani ambapo kuna usalama.
Aidha alisema kuwa, kauli mbiu ya mwaka huu ni ‘’kuelekea 2030: Tuungane kutafakari na kuchukua hatua kumaliza Udhalilishaji dhidi ya wanawake Zanzibar’’ ikiwa ni miaka 6 kutoka sasa, hivyo ipo haja ya kuunganisha nguvu ili kumaliza vitendo hiv
Nae, Mgeni
Rasmi katika maadhimisho hayo, Mwatima Issa Rashid amesema kuwa, katika siku hizo 16 za kupinga
udhalilishaji,wad kwa kushirikiana na
Serikali kuendelea kuzitumia katika kupinga
vitendo hivyo, kwani vinaonekana bado vinaongezeka.
Amesema
kuwa,siku hizo, zitumike katika kujenga jamii iliyo bora, ambayo haijihusishi
na vitendo vya ukatili na udhalilishaji dhidi ya wanawake na watoto.
Aidha,amesema
kuwa, ripoti iliyotolewa na Afisa Hairat
kutoka Tamwa, inaonesha ipo haja ya kushirikiana kwa pamoja wadau na Serikali
katika kupinga vitendo hivyo vya udhalilishaji kwani hali bado inatisha.
Nae, naibu kamisheni ya uhamiaji na Kocha wa mpira
wa miguu, Nasra Juma Mohamed amesema, michezo inasaidia watoto kujiepusha na vitendo vya
udhalilishaji duniani, kote takwimu zinaonesha hivyo.
Amesema
kuwa,kila kwenye watoto watatu basi mmoja kakumbwa na vitendo vya udhalilishaji,
hivyo ipo haja kuitumia michezo kama njia ya kujikinga na vitendo hivyo.
Jesse Mikofu, ni mwandishi wa habari mkongwe katika tasnia ya habari, alishauri kuwa wazazi kuvuja ukimnya kwa watoto wao, kwani watoto wanahitaji sehemu salama ya kueleza madhila wanayopitia , kwani kimnya kinazidi kuwawatesa na kuendelea kuwafanya wathirika wa vitendo hivyo.
Madhimisho hayo, ya siku 16 za kupinga vitendo vya udhalilishaji yameandaliwa na TAMWA ZNZ, na kuwashirikisha wandishi wa habari na wadau mbali mbali ili kutafakari na kutafuta ufumbuzi, yakiwa na kauli mbiu ‘’ KUELEKEA 2030: TUUNGANE KUTAFAKARI NA KUCHUKUA HATUA KUMALIZA UDHALILISHAJI DHIDI YA WANAWAKE ZANZIBAR.
Mwisho

Post a Comment