MATUMAINI MAKUBWA YA WANDISHI WA HABARI ZANZIBAR YAPO NTC


NA MARYAM NASSOR,


Wandishi wa Habari wa Zanzibar wanaendelea, kuweka  matumai  makubwa Kwa kamati ya ufundi  ya taifa (NTC).

 Akifungua mafunzo ya  sheria Kwa wandishi wa habari, Mkurugenzi wa Chama Cha wandishi wa habari  wanawake  Tanzania Zanzibar, (TAMWA  ZNZ)Dk Mzuri Issa, amesema ni zaidi ya miongo miwili sasa, wandishi wa  Habari wanadai Sheria rafiki za habari ambazo zinazoendana na wakati.

Amesema kuwa,  kwa  sasa matumai makubwa ya wandishi  wa Zanzibar , yapo Kwa kamati ya Ufundi  ya Taifa,ambayo mswada wa Sheria ya habari upo . 

Dk Mzuri amesema kuwa, ni haki ya wandishi wa Habari kupata  Sheria rafiki ambayo, itawalinda na  itaenda samba mba na maendeleo ya sayansi  na Teknolojia.

"Ni haki yetu kupata Sheria rafiki ya habari, ambayo itaendana na kasi ya mabadiliko ya sayansi na teknolojia yaliyopo sasa" amesema Dk Mzuri.

Nae, Afisa program    wa mradi huo wa  Sheria kutoka Tamwa ZNZ,Zaina Mzee amewataka wandishi wa habari kuendelea kufanya uchechemuzi wa Sheria ya Habari ili ipatikane.

Amesema kuwa, kuwepo  Kwa Sheria rafiki ya habari, kutapelekea uhuru wa kujieleza  na kuimarika huduma za kjamii na kimaendeleo Kwa ujumla.

Nae, Mkufunzi wa mafunzo  hayo,Bi Hawra Shamte amesema  Sheria kandamizi ya   usajili wa Habari  Magazeti na vitabu no.5 ya mwaka 1988 iliyofanywa marekebisho na Sheria no.8 ya 1997 ni Sheria kandamizi zinazonjima uhuru wa habari na kujieleza.

Aidha amesema kuwa, kifungu  Cha  27 (1) kinachompa Afisa yoyote wa Polisi, mamlaka  ya  kupekuwa na kukamata gazeti lolote, popote litakapo patikana, linapochapishwa kinyume na Sheria pia, kifungu hicho kifutwe hakiendani na wakati wa sasa.

"Sheria kama hizi , haziendani na wakati  huu, ni vyema kuzibadilisha" amesema bi Hawra.

Nao, wandishi wa waliopatiwa mafunzo hayo, Berema Nassor na Thuwaiba Habibu, wamesema wanataka Sheria za Habari ambazo, zitaendana na kasi ya maendeleo ya teknolojia.



Aidha, wamesema kuwa mswada huo kabla haijawa Sheria ni vyema ukarejesha Kwa wadau wa habari ili kujua kile kilio Chao Cha siku nyingi kimepata ufumbuzi.

Akijibu, maswala ya wandishi wa habari, katika kikao Cha Tathimini ya mafanikio ya miaka minne ya Dokta Hussein Mwinyi, Waziri wa Habari Utamaduni, vijana na Michezo, Tabia Maulid Mwita, amesema  mswada wa Sheria ya habari upo, katika kamati ya ufundi ya taifa (N TC) ambako unashuhulikiwa.

Katika hatua nyengine, Waziri huyo amesema kuwa anatamani mswada huo ufikishwe katika Baraza la wawakilishi hivi karibuni.

Jumla ya wandishi wa habari 15 kutoka Unguja  wamepatiwa  mafunzo ya siku mbili ya sheria kandamizi za habari zinazominya uhuru wa habari  na kujieleza nchini.

No comments

Powered by Blogger.