MICHEZO HUIMARISHA AFYA NA TIBA MUJARABU KWA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA
NA MARYAM
NASSOR,
MICHEZO ni fursa, ni ajira na huimarisha afya, inaaminika duniani kote kuwa, michezo ni tiba mujarabu kwa magonjwa
yasiyoambukizwa ambayo ni tishio kwa
afya za binaadamu.
Michezo hupunguza uwezekano wa kupata magonjwa
yasiyoambukizwa kama vile saratani, kisukari, magonjwa ya
moyo , shindikizo la juu la damu na huzuia
uwezekano wa kupata kiharusi ( stroke).
Magonjwa
yasiyoambukiza (NCDs) yanachangia takribani ya asilimia 33 % ya vifo vyote nchini, huku
takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) kwa mwaka 2020 zinaonesha kuwa
magonjwa hayo yalichangia zaidi ya vifo milioni 41 sawa na asilimia 71%
ya vifo vyote Duniani ukilinganisha na vifo
milioni 57 kwa mwaka 2016.
Waziri wa
Afya wa Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui, alipokuwa akizindua utafiti wa kitaifa wa
viashiria vya magonjwa yasiyoambukizwa,
katika ukumbi wa mikutano mjini Dodoma.
Alisema
kuwa, takwimu zinaonesha kuwa magonjwa yasiyoambukizwa, yameongezeka mara 5 hadi 9 zaidi kati ya miaka ya 80, ambapo yalikuwa ni asilimia 1 tu, kwa
watanzania waliokuwa na kisukari ni asilimia 5. lakini kwa sasa tatizo la kisukari limefikia asilimia 9 ,
wakati shindikizo la juu la damu limeongezeka hadi kufikia asilimia 25.
“Takwimu
hizo zote, tumekusanya kutoka kwenye vituo vyetu vya kutolea huduma za kiafya
nchini, ambazo zinaonesha ongezeko kubwa
sana la magonjwa hayo” amesema Waziri Mazrui.
Aidha
amesema kuwa, katika kukabiliana na
ongezeko la magonjwa hayo, Serikali inaongeza vituo vya afya na kutoa
elimu kwa jamii kuhusu namna bora ya
kujikinga na magonywa hayo Pamoja na
kuimarisha mifumo ya utoaji wa huduma za
afya nchini.
Aidha alishauri jamii kubadili mtindo wao
wa Maisha, na kujenga tabia ya kula mlo kamili na kufanya mazoezi ili kujikinga na magonjwa yasiyoambukizwa.
Nae, Makamo wa kwanza wa Rais wa Zanzibar
Mhe, Othman Massoud Othman, hivi
karibuni alipokuwa akifungua bonanza la
michezo kwa wote la Pemba Fitness
Club kwa kushirikiana na Chama cha Wandishi wa Habari Wanawake Tanzania Zanzibar ( TAMWA ZNZ) huko katika uwanja wa Gombani amewataka wananchi kufanya mazoezi
na kushiriki michezo mbali mbali ili kuipunguzia gharama Serikali ya kuagiza
dawa za matibabu ya magonywa yasiyoambukizwa, na familia katika kutafuta fedha kwa ajili ya gharama za matibabu.
“ Serikali
imekuwa ikitumia Fedha nyingi kuagiza dawa nje ya nchi, kwa maradhi
yasiyoambukizwa, hivyo ipo haja kwa jamii kubadili mtindo wa Maisha kwa kula
vyakula vyenye afya na kufanya mazoezi” ameshauri Makamo wa kwanza wa Rais.
Katika
bonanza hilo, aliwataka wanamichezo wa Club hiyo na jamii kwa ujumla kuwa na mazoea ya kufanya mazoezi,
kwani kuna athari nyingi za kutokufanya
mazoezi ikiwemo kuongezeka uzito wa
mwili na kusababisha udhaifu katika
msukumo wa damu.
Nasra Juma
Mohamed ni Naibu kamishna wa Timu ya Uhamiaji Zanzibar na kocha wa Mpira wa
Miguu, amesema ipo haja Kwa wanajamii
kushiriki michezo mbali mbali kwani michezo ni tiba.
Amesema
kuwa, mtu anae shiriki michezo afya yake inakuwa tofauti na yule asiyeshiriki
michezo, kwani michezo ni tiba kwa magonjwa mbali mbali yasiyoambukizwa.
“Sisi wana michezo tunakuwa na afya mzuri
ukilinganisha na watu wasioshiriki michezo, yale magonjwa ya mara kwa mara ya kuumwa na miguu au Presha yanatuepuka
kutokana na kuushughulisha mwili “ amesema Kocha Nasra.
Aidha ameitoa wito
kwa jamii, kushiriki michezo mbali mbali ili kuimarisha afya zao na
kujikinga na maradhi yasiyoambukiza.
Hija Mohamed Ramadhan
mshauri katika maswala ya jinsia katika michezo, katika mradi wa michezo kwa
maendeleo, unaofadhiliwa na shirika la Ujerumani nchini Tanzania (GIZ) amesema
mradi huo una lengo la kujenga viwanja saba vya michezo, vinne Unguja na vitatu
Pemba hivyo vitawarahisishia jamii kushiriki michezo.
Programu ya michezo kwa maendeleo,
inatekelezwa na TAMWA ZNZ, ZAFELA na Center for Youth Dialogue (CYD) kwa
kushirikiana na Deuth Gesellschaft fur intenational Zusammenrbeit (GIZ) shirika
la Ujerumani ikiwa na lengo la kuhamasisha waandishi wa habari kuandika habari
za michezo na ushiriki wa wanawake katika michezo.

Post a Comment