DR. Mzuri awataka wandishi kuripoti habari za mabadiliko ya tabianchi na kuonesha nafasi ya mwanamke katika mabadiliko hayo.

 



NA MARYAM NASSOR,

CHAMA Cha wandishi  wa habari wanawake  Tanzania, Zanzibar(TAMWA  ZNZ) kimesema  wakati umefika Kwa wandishi wa habari kuripoti, habari  za mabadiliko ya tabianchi, na  kuonesha nafasi  ya mwanamke katika kukabiliana na  mabadiliko hayo.


Ameyasema hayo, mkurugenzi wa chama hicho, Dk Mzuri Issa, alipokuwa akifungua  mafunzo Kwa wandishi wa habari   kuhusu mabadiliko ya tabianchi.


Dk Mzuri, amesema kuwa wanawake ndio  viongozi katika kukabiliana na mabadiliko  ya tabianchi, lakini kazi zao hazitangazwi,  hivyo  watu wengine hawajui  wanafanya nini katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.


"Kuna wanawake wanafanya mambo makubwa, katika kukabiliana na mabadiliko  ya tabianchi, lakini hawatangazwi kupitia vyombo vya habari" amesema.


Nae, mkufunzi katika mafunzo hayo, Ali Nassor Sultan amewataka wandishi wa Habari,  kufanya utafiti zaidi ili kubaini ukubwa wa tatizo.




"Wandishi  wa habari ni lazima muende mbali zaidi ili kubaini ukubwa wa tatizo " amesema.


Afisa habari katika  mradi huo, Sophia Ngalapi  amesema    kuwa lengo la mafunzo hayo, ni kuhamasisha wanawake kuwa viongozi katika kukabiliana na tabianchi.


Amesema kuwa, wandishi wanatakiwa kuonesha nafasi ya mwanamke katika kupambana na mabadiliko ya tabianchi na wanavyo kabiliana nayo.


" Wandishi munatakiwa kuonesha nafasi ya mwanamke  katika kupambana na mabadiliko ya tabianchi "amesema.


Nao, wandishi wa habari  walioshiriki  katika mafunzo hayo, Berema Nassor  na Zurima  Maulid ,walisema ipo haja Kwa wandishi wa habari kufanya kazi ya kuelimisha jamii kuhusiana na mabadiliko ya tabianchi kwani bado jamii haina uelewa kuhusu madhara ya mabadiliko ya tabianchi.


Jumla ya wandishi wa habari 30, kutoka Unguja na Pemba wamepatiwa  mafunzo, ya siku  mbili yanayolenga kuonesha  nafasi ya mwanamke katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, kilimo Cha miti mseto ( Agroforestry) na kuhifadhi mazingira Kwa kutumia mikoko, mafunzo  hayo yametolewa na chama Cha wandishi wa habari wanawake Tanzania Zanzibar, wakishirikiana na  Taasisi  ya kutunza mazingira ya Pemba,(CFP).

No comments

Powered by Blogger.