TAMWA ZNZ, YAWATAKA WANDISHI WA HABARI KUTUMIA MIFUMO YA KIDIGITAL KUHIFADHI KAZI ZAO.
NA MARYAM
NASSOR
Chama cha wandishi wa
habari wanawake Tanzania Zanzibar,
( TAMWA ZNZ) kimewataka wandishi wa habari nchini , kubadilika na kutumia mifumo wa
kidigitali kuhifadhi kazi zao ili ziishi
kwa muda mrefu na zikiwa na ubora.
Akiutambulisha mfumo wa Air table,katika kikao cha wandishi wa habari na wadau huko,katika
Ofisi za Tamwa Tunguu Unguja, Afisa wa tathmini na ufuatiliaji wa chama hicho, Mohamed Hatibu Mohamed ,
amesema kuwa ipo haja kwa wandishi wa habari kuhifadhi kazi zao katika mifumo
hiyo.
Amesema
kuwa, mfumo huo ni mzuri kwa wandishi wa
habari,kuutumia kwa ajili ya kuhifadhi taarifa zao, kwani ni rahisi kuutumia na
salama kwa kuhifazia taarifa zao.
‘’ Mfumo huu wa Air table, ni mzuri na rahisi kwa matumizi yenu ya kuhifadhi taarifa zenu ikiwemo story na Makala kwani zitadumu kwa muda mrefu zikiwa na ubora ule ule ‘’ amesema Mohamed.
Nae, Afisa
habari wa mradi huo, kutoka Tamwa ZNZ, Nafda Hindi amesema miradi yote ya Tamwa
, kuanzia sasa watatumia mfumo huo, hivyo aliwataka wandishi wa habari
wanaofanya kazi nao, kuutumia mfumo huo.
‘’ Tamwa tumejipanga
kuutumia mfumo wa Air table katika miradi yetu yote, kwani ni rahisi kuutumia
lakini pia ni salama kuhifadhia taarifa zenu ‘’ amesema.
Nao, baadhii ya wadau walioshiriki katika
kikao hicho, Khamis Haroun kutoka tume ya ukimwi Zanzibar ( ZAC)
amewapongeza Tamwa kwa kutumia mfumo wa
kidigitali kwa kuhifadhia taarifa zao.
‘’ Huu mfumo ni mzuri na salama kuhifadhia
taarifa zetu hivyo, ni vyema kwa taasisi
nyengine ambazo hazijaanza kutumia mifumo
kama hiyo, kuanza kuutumia ili taarifa
zao zibaki salama’’ amesema.
Amesema kuwa, ipo haja kwa Taasisi nyingine kutumia mifumo ya kidigitali katika kuhifadhia taarifa zao, kwani dunia sasa imekuwa kijiji kutokana na maendeleo makubwa ya kimtandao.
Nao, baadhi
ya wandishi wa habari waliohudhuria kikao hicho, Berema Suleiman na Huwaida
Nassor walisema wako tayari kuutumia mfumo huo, kwani kazi zao nyingi huwa
zinapotea kutokana na kuhifadhi katika komputa na mara ikiharibika basi,
wanapoteza kumbukumbu zao.
Post a Comment