Mashindano ya ladies first kwa mara ya kwanza yamefanyika Zanzibar.
NA MARYAM NASSOR
KAMISHNA wa baraza la
michezo Zanzibar,Mohamed Makame amesema mashindano ya 6 ya ladies First
yamefana kwa Zanzibar na kuwashukuru shirika la maendeleo la
Japan(JICA) kwa kuwakubalia ombi lao la kuja kuyafanya hapa Zanzibar.
Ameyasema hayo, huko katika Uwanja wa Amaan complex,
alipokuwa akizungumza na wandishi wa habari, mara baada ya kumaliza mashindano
hayo.
Amesema, mashindano hayo ya ladies first lengo lake ni kuhamasisha wanawake kushiriki
katika michezo, hususani katika michezo ya riadhaa.
“Mashindano haya ya ladies first ni mara ya sita kufanya kwa
Tanzania bara, lakini kwa hapa kwetu Zanzibar ni mara ya kwanza, lakini
tumefurahi yamefana sana’’ amesema.
Amesema kuwa, wachezaji kutoka Zanzibar walikuwa wakishiriki Tanzania bara, na kupata ushindi ndipo walipowaomba JICA, kuja kuyafanya Zanzibar kutokana na kuboreshwa kwa mindombinu ya michezo na viwanja vya kisasa.
‘’Tukiangalia michezo mingi wanashiriki wanaume kuliko,
wanawake hivyo, kuja kwa mashindano haya ya ladies first ni fursa kwa wanawake
kushiriki katika matamasha kama haya’’ amesema.
Nae, balozi wa Japan nchini Tanzania Yasushi Misawa, amesema mashindano hayo ni fursa kwa wanawake kushiriki, na amewashukuru wadau wote walishiriki kwa pamoja kufanikisha jambo hilo.
Amesema kuwa, anaamini
nchi ya Tanzania inakuwa kwa kasi, kutokana na kuwa inatunza rasilimali
watu, na amewataka vijana kutumia uwezo wao, katika kufanya kazi vizuri katika
Sanaa na michezo, kwani ni lazima mwanamke ashirikishwe ili kuleta maendeleo.
Nae, mshindi wa
kurusha mkuki kutoka mkoa wa magharibi ,Tuma
Makame Ali amesema amefurahi kushiriki mashindano hayo na kushinda, na
amewataka watoto wa kike kutumia fursa kama hizo zinapotokea kujitangaza na
kukuza vipaji vyao.
Mashindano hayo, maalum kwa wanawake, yamefanyika kwa lengo
la kuwahamasish watoto wa kike kushiriki michezo,hasa katika riadhaa na yameshirikisha
washiriki kutoka mikoa mitano ya Zanzibar, na mshindi katika shindano hilo ni
kutoka mkoa wa Mjini magharibi Unguja.



Post a Comment