WAANDISHI wa Habari nchini wametakiwa kujua madhara ya mabadiliko ya tabianchi.
NA MARYAM NASSOR;
WAANDISHI wa Habari nchini wametakiwa kujua madhara ya mabadiliko ya tabianchi, ili yanapotokea katika jamii iwe rahisi, kuyaripoti
Akizungumza katika muendelezo wa kikao cha kuandaa muongozo wa namna gani waandishi wataweza kuripoti taarifa za mabadiliko ya tabianchi, Mkufunzi kutoka Chuo kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA)Imane Duwe huko Ofisi za TAMWA Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja.
Amesema, lazima waandishi wa habari , wawe na uelewa mpana juu ya mabadiliko ya tabianchi.
"Ni vyema wakapatiwa mafunzo ambayo yanauhalisia wajambo wanaloizungumzia ili kuweza kuandika habaŕi zitakazokuwa na mvuto na uwelewa zaidi.
Amesema kuwa muongozo huo pia utasaidia waandishi kutambua jinsi gani watapata uelewa mzuri ili waweze kuleta mrejesho sahihi watakapokwenda kufanya kazi zao.
Akichanganua muongozo ambao utakaowawezesha waandishi kuuchukua na kuandaa habari mabadiliko ya tabianchi Afisa uhusiano chuo cha waandishi wa habari na mawasiliano,(IIT MADRASA) Mwatima Rashid Issa amesema nivyema waandishi wawe na utafiti mzuri ili jamii iweze kufahamu lengo halisi lililokusudiwa.
"Wandishi kuweni makini, katika mafunzo ili mupate uelewa wa kutosha ili iwe rahisi kwenu kuripoti " amesema.
Nao, wandishi walioshiriki mafunzo hayo, walisema watayafanyiakazi mafunzo hayo, ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi nchini


Post a Comment