MICHEZO NI FURSA KWA VIJANA KUJIAJIRI
NA MARYAM
NASSOR
MICHEZO hujenga Afya, huimarisha urafiki ni pesa ni fursa za kiuchumi lakini ndio
sekta inayoongoza ulimwenguni kutoa ajira kwa vijana.
Michezo ndio
sekta inayoongoza Duniani kutoa mishahara mikubwa Zaidi kuliko sekta yoyote.
Kwa mujibu
wa gazeti la kibiashara la nchini marekani forbes, limeorodhesha wanariadhaa
kumi wanaolipwa pesa nyingi Zaidi duniani nafasi ya kwanza akiishikilia Christiano Ronald.
Mchezaji
mwenye asili ya kireno, akilipwa pound milioni175,000 kwa mwaka sawa na bilioni
493,000 za kitanzania, sawa na mshahara wa
milioni 41,000 kwa mwezi.
Huku
mcheza gofu Jon Rahm akipanda hadi nafasi ya pili akilipwa dola milioni
218,000, wachezaji waliyodumu katika orodha hiyo ni Serena Wilium, Roger Fererer,
Tom Brady ambao wamekusha staafu.
Huko ni barani Ulaya , turudi nyumbani Afrika
bara lililosheheni kila aina ya vipaji’ waswahili wanasema mcheza kwao
hutunzwa’tuwaangalie wachezaji walitajirika kupitia michezo, tumuangalie Sadio
mane na Mohamed sallah wa nchini Misri, mchezaji kutoka Senegal Sadio Mane
akilipwa bilioni nane. kwa mwezi na Mo
Sallah analipwa milioni 18.2 na wengine wengi .
Kwa mujibu wa tarifa kutoka kwa mrajisi wa vyama vya michezo hapa Zanzibar kuna vyama 42 vya michezo vilivyosajiliwa.
Akizungumza na mwandishi wa Makala haya,
mrajisi Abubakar Mohamed Lunda amesema kwa sasa sekta ya michezo Zanzibar
imekuwa na vijana wengi wanazitumia vizuri fursa za michezo kujiajiri.
Amesema
kuwa, michezo ni sekta inayowainua vijana kiuchumi, kwani kuna michezo unatumia
roundi nne sawa na dakika 12 unalipwa
milioni tatu au Zaidi, kama mchezo wa ngumi za kulipwa(Boxing) na hapa Zanzibar
tayar zimekwisha ruhusiwa.
“ Vijana
tumieni fursa za michezo kujiajiri kwani michezo ni mingi na yote yanasaidia
kutoa ajira kwa vijana’’ alishauri.
Nae, kocha wa michezo kwa maendeleo Maryam Charles amesema michezo ni fursa hasa kwa watoto wakike kwani, wachezaji wengi wanaocheza Zanzibar wengi wanatoka Tanzania bara kutokana na hapo awali watu walikuwa wanachukulia michezo kama uhuni.
Amesema
kuwa, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imewekeza kwenye michezo ili wananchi
wanufaike na fursa zinazotokana na michezo, hivyo ni vyema wazazi wakawaacha
watoto kujiendeleza katika michezo ili wajiajiri kwani michezo ni ajira kama
ajira nyengine.
“Wazazi wasiuchukulie mpira kama ni uhuni na kukatisha ndoto za watoto wao, kwani hapa Zanzibar tunao wachezaji kama Fei toto anacheza mpira na analipwa vizuri na kuendesha maisha yake’’ alisema.
Aidha alisema kuwa, vipaji vipo katika kila
michezo ni wakati sasa wazazi kuwasaidia watoto wao kuendeleza vipaji vyao na
humo , kwenye michezo zinapatikana ajira kuliko zile za sekta ya umma au
mashirika binafsi kwani mshahara wa wachezaji
ni mkubwa kuliko muajiriwa Serikalini.
‘’ Michezo
ni fursa mimi mwenye nimesafiri sehemu
nyingi kwa ajili ya michezo, hapa juzi tu timu ya watoto chini ya umri wa miaka
15 ya wanawake imeenda Ufaransa,kwa kupitia mpira hizo ndio fursa za michezo ,”
alisema.
Nae,
mchezaji kutoka timu ya wanawake ya New Generation Hafidha Juma Ali amesema ni
kweli michezo ni ajira na fursa ya kiuchumi lakini, Serikali izidi kuwekeza katika michezo, kwani kwa ligi
za wanawake bado kuna changamoto ya ufadhili.
Amesema
kuwa, mpira wa wanawake umekuwa akimchukulia mfano mchezaji kutoka bara Clara Ruvanga analipwa hadi milioni 25 kwa mwezi ni
mfano mzuri kuona soka linalipa.
Aidha
aliiomba Serikali kama mdau nambari moja kuzidi kufanya uwekezaji ili na mpira
wa Zanzibar ufike mbali na wachezaji wanufaike kupitia michezo.
“ Michezo ni
fursa za ajira kwani wachezaji wanajiajiri kupitia soka lakini , Serikali izidi
kufanya uwekezaji ili tufike mbali na sisi wachezaji kutoka Zanzibar ‘’
alishauri.
Nae, Makame
Ameir Mgeni kocha wa michezo kwa
maendeleo, amesema michezo ni pesa hasa
katika michezo ya mtu mmoja mmoja kama ngumi za kulipwa,mpira wa wavu na
riadhaa.
Amesema kuwa
kwa hapa Zanzibar wapo wachezaji wanaojiajiri na kufanikiwa kupitia michezo
hayo kama mchezaji Dawa Haji, Asma
Omar na wengineo ambao wanaendesha
maisha yao kupitia michezo.
Katika mradi wa michezo kwa maendeleo
unaotekelezwa na shirika la Ujerumani nchini Tanzania (GIZ) umesema
mradi huo unalengo la kujenga viwanja saba vya mpira Unguja na Pemba, vikiwemo viwanja vya tenis lengo likiwa ni
kutekeleza usawa wa kijinsia katika michezo na kuinua sekta hiyo ili vijana
wajiajiri kupitia michezo.
MWISHO
Post a Comment