KUKOSEKANA KWA DAWATI LA JINSIA KWENYE MICHEZO , WAATHIRIKA WAPAZA SAUTI ZAO
NA MARYAM NASSOR
KANUNI na sera ya michezo ya Zanzibar
ya mwaka 2018, imetamka wazi nia njemaa
ya Serikali katika kuhakikisha uwepo wa usawa wa jinsia katika michezo.
Hata hivyo,
nia njemaa hii haifanyi kazi katika
usimamizi wa kila siku, kutokana na mapungufu ya vifaa vya michezo na ukosefu
wa dawati la jinsia ndani ya vyama vya michezo.
Umuhimu wa
dawati la jinsia ndani ya vyama vya michezo ni mkubwa, kutokana na kutamalaki
kwa vitendo vya ukatili na udhalilishaji ndani ya michezo na kuonekana ni vya
kawaida.
Waswahili wanasema lisemwalo lipo, Fatma Ali Bakari( si jina
lake halisi) mchezaji wa mpira wa miguu timu ya wanawake, akizungumza na
mwandishi wa Makala hii amesema
udhalilishaji kwenye michezo upo na wachezaji wanauchukulia ni hali ya
kawaida.
Amesema
kuwa, ni vigumu kuutambua udhalilishaji unaotokea kwenye michezo kutokana na
kuwa watendaji wa matendo hayo ni watu ambao wanaaminika katika michezo,kwani
mara nyingi anaweza kuwa kocha hakupangi
katika kikosi mpaka akutake kimapenzi.
‘’Mimi ni
muhanga wa udhalilishaji katika michezo , niliacha kucheza mpira na kuihama
timu yangu ya mwanzo kutokana na kocha kunitaka kimapenzi , nikaamua kuacha
kwenda kufanya mazoezi’’ alisema.
Saada Saidi
mchezaji wa timu ya mpira wa miguu warrious, amesema dawati
la jinsia ni muhimu mno kuanzishwa
kwenye vyama vya michezo, kutokana na kuwa wachezaji wakikumbana na
vitendo vya ukatili ndani ya michezo hawajui wapi pa kukimbia.
Alisema
kuwa, sheria iliyokuwepo ya michezo ibara ya 58 ya katiba ya fifa, inawataka
wachezaji kupeleka malalamiko yao kwenye kamati za maadili ndani ya vyama vya
michezo na kesi za michezo zisipelekwe
kwenye mahakama za kawaida.
‘’ Icho kitu
hakiingii akili vipi unaweza kumpelekea malalamiko mtu ambaye aliyekubaka,
atajihukumu vipi na wewe kweli utapa haki yako katika hali kama hiyo hatuwezi
kufika, kamati inaundwa na kocha nay eye ndio mbakaji masalani, haki haiwezi
ikapatikana’’ alisema.
Nae,
mchezaji wa timu ya mwembeladu fc timu ya wanaume, Abubakar Mohamed Sharif
amesema ni vyema kuanzishwa kwa dawati la jinsia ndani ya michezo, kwani
udhalilishaji ni mwingi na wachezaji hawajui nani wakumueleza matatizo yao
yanao wasibu.
‘’ Sisi
wachezaji hatuna sehemu maalum ya kupeleka malalamiko yetu kuhusu ukatili na udhalilishaji unaotokea
ndani ya michezo, hivyo wengine huacha ndoto zao zikapotea,tu kwasababu ya kutakiwa na makocha
kimapenzi na kesi hizo ni nyingi kwenye michezo ‘’ alisema.
Nae, kocha
wa ngumi za kulipwa Maryam Charles
amesema kuwa kama Serikali inataka vijana wengi wajiajiri kwenye michezo
ni wajibu wao kuweka mazingira mazuri na
kuiangalia kwa umakini sekta hiyo,ili
wazazi wawe na uhakiki wa usalama wa watoto wao.
Alisema
kuwa, michezo ni afya , ni fursa nia
pesa lakini pia ndio sekta yenye uhakika wa ajira kwa vijana awe kasoma au
hajasoma ilimradi tu awe anapenda michezo anaweza kufanikiwa.
Aidha alisema kuwa, ni wakati sasa wa kuiangalia sheria ya michezo na kuitafsiri nini maana halisi na kwanini kesi za udhalilishaji zinazotokea ndani ya michezo zisipelekwe katika vyombo vya sheria.
“ Nahisi
mimi maana halisi ya ile ibara ya 58 ya katiba ya fifa bado haijaeleweka
wala haijakaa sawa kwa mazingira ya sasa
inahitaji mabadiliko’’ alisema.
Makame Ameir
Mgeni, kocha wa michezo kwa maendeleo amesema
kuna kesi nyingi za udhalilishaji
ambazo zimetokea ndani ya michezo, na wafanyaji
hawakuchukuliwa hatua zozote na kupelekea kuuwa vipaji na ndoto za watoto hao.
Alisema
kuwa, kuna makocha wanabaka kwenye michezo na wengine kuwapa mimba wachezaji
lakini wachezaji hawana sehemu maalum ya kupeleka malalamiko yao, mwisho wa
siku kuacha na mpira .
‘’ Wachezaji
wanakumbana na udhalilishaji mkubwa kwenye michezo na wanakosa sehemu ya
kukimbila , hivyo kuanzishwa kwa dawati la jinsia litawapa ujasiri na kujiamini
wachezaji wetu na watajiona wako sehemu salama kwenye michezo’’ alisema.
Katibu wa
shirikisho la mpira wa miguu Zanzibar ( ZFF) Hassan Ahmada Vuai amekiri kuwa
kuna haja ya kuanzishwa kwa dawati la jinsia ndani ya michezo kutokana na
umuhimu wake.
Alisema
kuwa, kama wanataka kufikiwa ule usawa wa kijinsia ndani ya michezo basi ipo
haja ya kuanzishwa kwa dawati hilo ili
lishuhulikie vitendo vya ukatili na udhalilishaji unaotokea ndani ya michezo.
Chama cha
wandishi wa habari wanawake Zanzibar,( TAMWA ZNZ) kupitia mradi wa michezo kwa maendeleo unaofadhiliwa
na shirika la Ujerumani (GIZ) kupitia
Afisa wake Hairat Haji amewataka wandishi wa
habari kuhamasisha na kuandika
habari za michezo na changamoto zinazowakumba wachezaji ndani ya michezo
ikiwemo ukosefu wa dawati la jinsia ili changamoto hizo zifanyiwe kazi.
Nao, chama
cha wanasheria wanawake Zanzibar
(ZAFELA) kupitia Afisa wake Ruffea Juma, kimesema kuwa katika mradi wa
michezo kwa maendeleo unaodhaminiwa na
shirika la Ujerumani nchini Tanzania
,(GIZ) kimeandaa muongoz ambao utawasaidia wachezaji kujitambua na kujikinga na
udhalilishaji ndani ya michezo .
MWISHO
Post a Comment