JAMII IMETAKIWA KUHAMASISHA USAWA WA KIJINSIA KATIKA ELIMU NA MICHEZO
NA MARYAM NASSOR
JAMII
imetakiwa kutilia mkazo watoto katika kushiriki michezo mbali mbali ili kukuza ujuzi wa stadi za maisha katika kukabiliana na vikwazo mbali mbali kama ukatili na udhalilishaji wa kijinsia.
Hayo
yameelezwana wadau katika kongamano la riadhaa la siku ya motto wa Afrika, kwa
wanafunzi wa skuli mbali mbali za Unguja
yaliyoandaliwa na chama cha wandiishi wa
habari wanawake Zanzibar(TAMWA ZNZ) kwa kushirikiana na chama cha wanasheria wanawake Zanzibar
(ZAFELA) shirika la Ujerumani nchini
Tanzania (GIZ) na kituo cha majadilianao
ya vijana (CYD) kwa lengo la kuhamasisha usawa wa jinsia katika michezo.
Akizungumza kuhusu juhudi za kuimarisha usawa wa kijinsia na kuhamasisha michezo, Dk Mzuri Issa Ali Mkurugenzi wa TAMWA ZNZ, alisisitiza umuhimu wa kuwa mfano mzuri kwa jamii ili iwe hamasa kwa watu wengine kuingia katika michezo.
‘’ Tuwe mifano mizuri ya kuigwa kwa kuwa na heshima katika jamii, kwasababu sisi tuna nafasi ya kupata mawaidha sehemu mbali mbali ya stadi za maisha , hivyo tuna kila sababu ya kuhamasisha michezo kwa wote’’ alisema.
Kwa upande
wake Wanu Ali Makame , meneja idara ya
mitaala na vifaa kutoka wizara ya Elimu na mafunzo ya amali Zanzibar , alisema
kuwa katika kutilia mkazo umuhimu wa
michezo kwa maendeleo , wizara imeweka somo maalum linaloelezea masuala ya
michezo.
‘’ Tuna somo
maalumu linaloelezea masuala ya michezo , tunaweza tukacheza na tukasoma kwa
salama na Amani bila ya kuathiri mila na
tamaduni zenu’’ alisema.
Hija
Ramadhan kutoka shirika la GIZ aliongeza kuwa jitihada za kutengeneza usawa wa
kijinsia ni pamaoja na kuhakikisha wadau wanashirikiana kuwalinda watoto na
wanawake dhidi ya ukatili.
Katika hafla
hiyo, wanafunzi walipata fursa ya kushiriki mbio fupi na washindi kuzawadiwa
zawadi mbali mbali ikiwemo medali ,madaftari na bahasha.
Mashindano hayo yaliyoandaliwa na Tamwa ZNZ,
yamewaleta pamoja wadau mbali mbali ikiwemo wanafunzi kutoka skuli mbali mbali
za Unguja, wanamichezo walimu na wadau wa maswala ya jinsia yakiambatana na
kauli mbiu’’ WAKATI NI SASA ‘’ wekeza katika elimu na michezo kwa watoto wote
ikiwa ni chombo muhimu ambapo michezo itatumika kama chombo cha kuleta
maendeleo na usawa katika michezo.
MWISHO
Post a Comment