UKOSEFU WA UFADHILI LIGI YA WANAWAKE BADO CHANGAMOTO

 


NA MARYAM NASSOR

UKOSEFU wa ufadhili katika ligi za mipira ya wanawake imetajwa kuwa ndio chanzo cha timu nyingi kufa.

 Akizungumza na mwandishi wa Habari hizi,  huko katika uwanja wa mazoezi Saateni, Unguja kocha  wa timu ya warrious  Haji Hamdu Nahoda.

Alisema , timu nyingi za mpira wa miguu za wanawake hazina ufadhili ukilinganisha na timu  za wanaume.

Alisema kuwa, kuna timu nyingi zimeshindwa kushiriki ligi kuu Zanzibar msimu huu, kutokana na ukosefu  wa rasilimali fedha na nyengine kufa kabisa.

 “ Kwa sasa ligi ya wanawake imesimama kutokana na kuwa haina mfadhili, wachezaji wanajitowa vya kutosha hawana hata posho’’ alisema.

Alisema kuwa, wadau mbali mbali wajitokeze kuwasapoti kwasababu hamasa ni kubwa ukilinganisha na hapo awali kulikuwa hakuna  timu za wanawake.

 Aidha alisema kuwa,  soka ni ajira kama ajira nyengine hivyo,  lakini tatizo kuwa  hakuna wafadhili wakuwashika mkono  ili kuendeleza vipaji vya  wachezaji hao.

 Nao, baadhi ya wachezaji katika timu ya  warrious, walisema   kuwa wana ndoto za kufika mbali katika soka ya kuichezea simba guens na nyenginezo .

Walisema kuwa, lakini   wanaiomba Serikali ya Mapinduzi Zanzibar  kama mdau nambari moja kuendelea kuwapigania wapate ufadhili  katika ligi za wanawake kutokana na kuwa wanacheza katika mazingira magumu.

“ Sisi hapa tunapenda kucheza mpira lakini ligi yetu bado ina changamoto kuwa kwa upande wa ufadhili” walisema.

 

MWISHO

No comments

Powered by Blogger.