RC MJINI MAGHARIBI, AITAKA SUZA KUENDELEA KUIBUA VIPAJI VYA UWANDISHI

 



NA MARYAM NASSOR

MKUU wa mkoa wa mjini magharibi Unguja, Idrissa Kitwana Mustafa , amekitaka chuo kikuu cha taifa  Zanzibar ( SUZA) kuendelea kuandaa  mashindano ya waandishi chipukizi ili  kuwapima uwezo wao katika kada hiyo.

Ameyasema hayo,  katika hafla ya  kuwatunuku  vyeti na zawadi washindi wa shindano la waandishi chipukizi  huko katika  chuo cha suza kampasi ya kiliman.

 Alisema ,  fani ya uwandishi wa habari ni kada nyeti sana, hivyo ni vyema wanafunzi wakasoma na kufanya kazi kwa bidii, kwani siku hizi kumeibuka wimbi kubwa la watu wanaojiita waandishi bila ya kuwa na sifa ya Uaandishi au bila ya kusomea fani hiyo.

“ Siku hizi kumeibuka wimbi la waandishi makanjanja na wao wanajiita waandishi wa habari wakati hawajasoma hata cheti katika habari na kuichafua kada hii kwa kwenda kinyume na maadili ya uwandishi”alisema.

Aidha alisema kuwa, kwa kupitia mashindano kama hayo, watapatikana wandishi wazuri na wajuzi wa lugha kwani ili uwe mwandishi mzuri basi , uwe na uwelewa wa lugha nyingi ikiwemo kichina ambacho kinafundishwa katika  chuo hicho.

Nae mwenyekiti wa  kamati ya majaji, Saleh Yussuf Mnemo  alisema kuwa, kazi zilizowasilishwa zilikuwa ni 40 na zote zilikuwa nzuri na zenye sifa   hivyo walipata wakati mguu kumtafuta mshindi.

Alisema kuwa, katika vipengele vilivyoshindania vilikuwa ni vipengele vitatu ambavyo ni  uwandaaji wa makala za televisheni na radio, makala za mtandaoni na utangazaji .


 Akisoma risala fupi ya chuo hicho, Khamis Juma Abdallah ambae ni mkuu wa habari na mawasiliano  chuo cha suza, alisema kuwa lengo la kuandaa mashindano hayo ni kujali mchngo  wa vijana hao na ililenga vijana  kuanzia miaka 18 hadi 35. Na sharti awe amepita  katika vyuo vya suza.

Nae, balozi mdogo wa China , anaeishii Zanzibar zheng min alisema kuwa kuna ofa kubwa ya masomo kwa wanafunzi wa Zanzibar, hivyo ni vyema wakasoma kwa bidii na kujifunza lugha ya  kichina  ili wanufaike na fursa hiyo.

  Mashindano hayo, yaliyodhaminiwa na baraza la habari Tanzania kwa upande wa Zanzibar (MCT ZNZ), chama cha waandishi wa habari (ZPC) na SUZA Washindi katika mashindano hayo, walidhawadiwa vyeti na fedha taslimu .

 

                    MWISHOO

No comments

Powered by Blogger.