KESI YA BANGI YAPIGWA DANA DANA MAHAKAMA KUU.
NA MARYAM NASSOR PEMBA, KESI ya kupatikana na dawa zinazoaminika kuwa ni za kulevya, iliyopo mahakama kuu Zanzibar kanda ya Pemba, imeshindwa kuendelea, baada ya shahidi namba moja ambae ni mkemia kushindwa kuchomoza mahakamani hapo, kwa udhuru wa ugonjwa wa ‘RED EYES’.
Awali , ilidaiwa mahakamani hapo kuwa,mtuhumiwa katika shauri hilo, Omar Hatibu Juma,alikutwa na misokoto mia saba yanayosadikiwa kuwa ni dawa za kulevya aina ya bangi, yenye uzito wa 2836.75g, huko machomanne wilaya ya chake chake.
Mara baada ya kufika mahakamani hapo, mtuhumiwa akiwakilishwa na wakili msomi, Zahran Said aliambiwa na upande wa mashtaka uliyokuwa ukiongozwa na mwendesha mashtaka kutoka Afisi ya mkurugenzi wa mashtaka Pemba,Mohamed Ali Juma, kuwa walikuwa wanategemea kupokea mashahid watatu.
Mwendesha mashtaka huyo, alidai kuwa kesi hiyo ipo kwa ajili ya kusikilizwa, na wamepokea mashahidi wawili kati ya watatu waliyowaita,lakini shahidi namba moja ambae ni mkemia hajafika mahakamani hapo kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa macho mekundu.
Dpp huyo,alidai kuwa kutokana ugumu wa kesi hiyo wanahitaji mtiririko mzuri wa mashahidi, hivyo hawawezi kusikiliza shahidi wengine kabla ya kuaza na mkemia.
‘’Muheshimiwa leo kesi ipo kwa ajili ya kusikilizwa lakini shahidi namba moja hajafika mahakamani, hivyo tunaomba utupangie tarehe nyengine kwa ajili ya kusikiliza mashahidi’’alidai
Mara baada ya kuusikiliza upande wa mashtaka,Jaji wa mahakama kuu Pemba, Ibrahim Mzee Ibrahim, aliuliza upande wa utetezi kuwa wanasemaje kuhus ombi la upande wa mashtaka.
Nao, upande wa utetezi ulikuwa ukiongozwa na wakili msomi Zahran Said na Massoud Juma, walisema kuwa,hawakubaliani na ombi hilo kutokana na kuwa, mteja wao ameshakaa ndani muda mrefu wanaomba wasikilizwe mashahidi ambao wamefika mahakamani.
“muheshimiwa Jaji kama ikikupendeza, basi tunaomba usikilize hao mashahidi waliofika kutokana na kuwa mteja wangu yuko ndani mudaa mrefu” alidai
Alidai kuwa, shauri hilo tokea lifunguliwe mahakamani hapo, linafika miezi sita na mtuhumiwa yuko ndani, kama ikiwezekana basi wasikilizwe hao mashahidi waliyofika hii leo.
Nae Jaji wa mahakama hiyo, alimuliza wakili wa upande wa utetezi kuwa mteja wake, ana shutumiwa na makosa mangapi kwa sababu kama kosa ni kukutwa na bangi basi shahidi namba moja ni mkemia.
Aidha alisema kuwa, mkemia ndie atakae sibitisha kuwa kile alichokiona ni bangi au laa na hapo, ushahidi utakaofuata utakuwa unasapoti.
“Hatuwezi kusikiliza shahidi wengine kabla ya mkemia, kwa sababu mkemia ndie atakae sibitisha hizi tuhuma ni za kweli au laa”alisema.
Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa,siku ya tarehe 28/07/2023 majira ya saa4:00 za usiku huko mkoroshoni, katika wilaya ya Chake chake .
Ilidaiwa kuwa,Bila ya halali mtuhumiwa huyo,alipatikana na misokoto mia saba , ya dawa za kulevya aina ya bhangi yenye uzito wa 2836.75g jambo ambalo ni kosa kisheria.
Kufanya hivyo ni kosa kinyume na kifungu cha 21 (1)(d) cha sheria za mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya Zanzibar, sheria namba 8 ya mwaka 2021 sheria za Zanzibar.
Kesi hiyo, imehairishwa mahakamani hapo hadi mach 7 mwaka 2024 ambapo itasikilizwa mfululizo na Jaji Ibrahimu,kutaka mashahidi siku hiyo wafike.
MWISHO


Post a Comment