"Wataka talaka kwa mume uliyemzoea unakwenda kwamume usiyemjua"
NA TATU JUMA
"Wataka talaka kwa mume uliyemzoea unakwenda kwamume usiyemjua"
Kauli hiyo imetokewa na Naibu Waziri wa maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee Wanawake na watoto Zawadi Amour Nassor katika hafla ya Kongamano la Ustaarabu wa Mwanamke Zanzibar iliyofanyika Ukumbi wa Golden Tulip huko Malindi Mjini Unguja.
Amesema ,mwanamke haipendezi kudai talaka kiholela kwenye ndoa kwani inapelekea hasara kubwa ikiwemo kutekekeza watoto.
Amendelea kwa kesema kuwa kuna baadhi ya wanawake hawajitambui jambo ambalo hurudisha nyuma maendeleo hivyo ameomba kushirikiana kwapamoja kutatua changamoto zinazojitokeza katika jamii.
Mbali na hayo pia amewataka washiriki wa kongamano hilo kusikiliza na kuyafanyia kazi mafuzo hayo kwa lengo la kujipatia maendeleo.
Amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inatambua kazi ya Taasisi hiyo kwani maendeleo ya Taifa haiwezekani kutoshiriki nguvu ya mwanamke katika nyanja za maisha hivyo ameomba kushirikiana pamoja katika kutatua changamoto zitakapotokezea.
Kongamano hilo la
Ustaarabu wa Mwanamke lilisheheni wanawake wafanyabiashara pamoja na
wajasiriamali mbali mbali kwalengo la kujifunza memgi ikiwemo Malezi ya
watoto,Afya,Biashara pamoja na Mahusiano.

Post a Comment