WANANCHI WA ZANZIBAR WAMETAKIWA KUWA NA UTARATIBU WA KUJICHUKUZA SARATANI YA MATITI
Na Maryam Nassor
WANANCHI wa Zanzibar wametakiwa
kuwa na utaratibu wa kupima Afya
zao mara kwa mara ,kutokana na
kuongezeka kwa Ugonjwa wa saratani ya
matiti nchini Tanzania.
Wakizungumza na waandishi wa Habari , katika kambi ya
Matibabu huko katika Ukumbi wa Kariakoo Mjini Unguja Afisa kutoka Kitengo Shirikishi cha Afya ya Uzazi na Mtoto kutoka Wizara ya
Afya Zanzibar Mwanafatima Ali Mohamed
Amesema , Wimbi la
wagonjwa wa saratani ya matiti linaendelea kuongezeka nchini Tanzania, huku
wataalamu wa afya wakionya kuwa idadi hiyo inaweza kuongezeka zaidi iwapo jamii
haitachukua hatua za mapema za uchunguzi na kinga.
Amesema kuwa, takwimu za ugonjwa huo Duniani zinaonesha kukuwa katika wagonjwa 10 wakipimwa
afya zao watano wanagundulika na Saratani hiyo.
Amesema kutokana na mwezi huu ni mwezi wa kutoa uwelewa kwa
wananchi wameandaa kambi mbali mbali za Matibabu katika Wilaya ya Magharibi ‘A’
Unguja na wamewapima watu zaidi ya mia mbili
( 200) na Chumbuni waliwapima
watu 170 na bado wanaendelea kutoa huduma hiyo katika shehia nyengine.
“ Kwa upande wa
saratani ya matiti tumewapima watu wengi
lakini pia tuliwakuta wanawake zaidi ya 20 wanadalili za ugonjwa huo na
mwanamke mmoja alikuwa ameathirika na
ugonjwa huo “ amesema .
Aidha amesema kuwa,
tokea waanze kazi hiyo mwaka jana June
2024 mpaka sasa jumla ya wananchi 740,000
tayari wameshawapima kupitia kambi hizo za Matibabu Unguja na Pemba.
Daktari huyo ,
amesema idadi ya wagonjwa wa saratani ya matiti imeongezeka kwa kasi katika
kipindi cha miaka ya hivi karibuni hali inayochangiwa na mabadiliko ya mfumo wa
maisha, lishe duni na kuchelewa kufanyiwa uchunguzi
Amesema sababu nyingine ni uelewa mdogo wa jamii kuhusu
umuhimu wa uchunguzi wa mapema wa saratani ya matiti, na bado kuna hofu
miongoni mwa wanawake wengi kwenda hospitalini wakihisi uvimbe au maumivu.
“Wengi
wakiona dalili za awali, hufikiri ni mambo madogo kama mabadiliko ya homoni au
maumivu ya kawaida ya kifua. Wengine wanaogopa matokeo ya uchunguzi, jambo
linalosababisha kuchelewa kupata tiba sahihi,” aliongeza.
Miongoni mwa waliopitia changamoto hiyo ni Subira Ali Hamza, mkazi wa Matemwe mkoa wa
Kaskazini Unguja, ambaye kwa sasa ni mnusurika wa saratani ya matiti. amesema
aligunduliwa kuwa na ugonjwa huo baada
ya kupuuza dalili kwa zaidi ya miezi sita.
Alisema kwa mara ya kwanza, alienda hospital na kumueleza
Daktari kuwa kafanya boje akaambia ajichuwe kwa maji ya moto baada ya mwezi
akarudi tena hali bado na akaambiwa akafanye kipimo cha Utra sound na
kugundulika na ugonjwa huo.
“Nilianza
kuhisi uvimbe mdogo kwenye chuchu, lakini nilipuuzia nikidhani utapotea ,
Baadaye nilianza kuumwa na nilipoenda hospitali madaktari waliniambia nina
saratani , nilipoteza nguvu na
matumaini, lakini kwa msaada wa familia na matibabu, nilipona,” alisema kwa
hisia.
Amesema kwa sasa
anatumia uzoefu wake, kuelimisha wanawake wengine kuhusu umuhimu wa kufanya
uchunguzi wa mara kwa mara ili kugundulika mapema ugonjwa huo.
“Ninawashauri
wanawake wenzangu wajipende, wajichunguze na waende hospitalini mapema Saratani
inapogunduliwa mapema, ina tiba,” alisisitiza.
Kwa upande wake, DKT Merirose Kaya Giatus
Dokta Bingwa wa Magonjwa ya jamii kutoka Asasi ya JAPAIGO, amesema wao kama wadau wanafanyakazi na Serikali
ya Mapinduzi Zanzibar na wamejikita katika
kusaidia katika afua ya Magonjwa
yasioambukizwa .
Amesema, Katika
mwezi wa Oktoba wamewamejikita katika
kutoa elimu ya kinga na kuwajengea uwezo
wahudumu wa Afya katika uchunguzi wa kupapasa
lakini pia uchunguzi wa kina kwa kutumia shindano .
Amesema kuwa, watawawezesha pia madaktari kuweza kutoa
huduma kwa wagonjwa wa saratani ya Matiti na wao kama mradi wataendelea
kutoahuduma hizo kwa kipindi cha miaka mitano.
Aidha amesema kuwa, takwimu zinaonesha ugonjwa wa saratani
ya matiti unaongoza kwa kuuwa zaidi ukilinganisha na saratani ya shingo ya mlango
wa kizazi.
“ Na Bahati mbaya wagonjwa wa saratani ya Matiti wanaogundulika zaidi ya asilimia 50 wanapoteza maisha, ukichunguza
wanawake 10 basi watano wanapoteza maisha, kwani wengi wao
wanagunduliwa katika stage ya tatu ambao
ni vigumu kutibika “ amesema.
“Wanaume
wana nafasi muhimu katika kuwahamasisha wake zao, dada au mama zao kwenda
kupima. Saratani ya matiti si ugonjwa wa wanawake pekee, hata wanaume wachache
hupata, hivyo elimu ni ya wote,” amesema.
Aidha
amesema kuwa, kuna vichocheo vingi vinavyosababisha Saratani hiyo, ikiwemo mtindo wa maisha , vinasaba vya urithi na shida
kubwa ni jamii hawajui visababishi vya
ugonjwa huo.
Ameongeza kuwa ,serikali inaeendelea kuboresha miundombinu
ya matibabu katika hospitali za mikoa, ikiwa ni pamoja na huduma za uchunguzi
wa saratani, ili wananchi wengi wapate huduma .
Amewaomba wananchi wa Zanzibar, kuwa na utamaduni wa kujichunguza
matiti yao mapema ili wakigundulika
inakuwa rahisi kupata matibabu na kupona kwa haraka.
MWISHO

Post a Comment