MGOMBEA URAIS WA CHAMA CHA ADC AMEAHIDI SHIBE KWANZA KWA KILA MZANZIBAR
NA MARYAM NASSOR,
MGOMBEA
Urais kwa tiketi ya chama cha Alliance for Democrats Change ( ADC) Hamad Rashid Mohammed ameehidi neema ya shibe kwanza kwa kila
Mzanzibar endapo atachaguliwa.
Ameyasema
hayo, huko katika Afisi za Chama hicho
Daraja bovu wilaya ya Magharibi ‘A’ Unguja.
Mgombea huyo
amesema , akipewa ridhaa na wananchi wa Zanzibar atahakikisha shibe kwanza kwa kuweka mazingira mazuri ya
upatikanaji wa Chakula.
Amesema
kuwa, kipaumbele chake Cha pili atahakikisha elimu bure kwa kila mzanzibar kuanzia chekechea mpaka chuo kikuu.
Aidha
amesema kuwa, kima Cha chini Cha
mshahara kwa kila mfanyakazi atalipwa shilingi laki sita za kitanzania
"Nawaombeni sana ndugu zangu , vipaumbele vyetu
mumevisikia na vinauzika kwa wananchi ,maamuzi mutafanya
nyie"amesema mgombea huyo.
Nae,
Mwenyekiti wa wanawake wa Chama hicho na mgombea wa ubunge Jimbo la Malindi,
Nadhra Ali Haji amelishukuru jeshi la polisi kwa kuimarisha ulinzi muda wote
wakati wanamsindikiza mgombea wao, kuchukua fomu ya uteuzi tume ya uchaguzi Zanzibar.
"Kwa
kweli jeshi la polisi limefanya kazi nzuri ya kuimarisha ulinzi kwa kila Chama
bila ya upendeleo na hivyo ndivyo inavyotakiwa" amesema.
Aidha
amewaomba wananchi wa Zanzibar kukipigia kura nyingi Chama hicho tarehe Oktober
29 ili kuhakikisha kinapata ushindi na kuwaletea maendeleo.
Nae, mgombea
ubunge Jimbo la Chumbuni Zanzibar, kwa tiketi ya Chama hicho Mafunda Faisal Ali
amewaomba wanachama wa Chama hicho,
kuendelea kutunza amani ya nchi kwani bila ya amani hakuna maendeleo.
" Ndugu
zangu tuendelee kutunza amani ya nchi yetu na
naowambeni sana kukipigia kura nyingi za ndiyo Chama chetu ili
tushirikiane kuleta maendeleo ya nchi yetu " amesema.
MWISHO

Post a Comment