ZAMECO YAITAKA TUME YA UCHAGUZI ZNZ, KUZIFANYIA KAZI CHANGAMOTO ZA WANDISHI.
NA MARYAM
NASSOR
KAMATI ya waatalamu wa maswala ya Habari
Zanzibar ( ZAMECO) imeitaka
tume ya uchaguzi kuzifanyia kazi
changamoto za wandishi wa Habari
kuelekea uchaguzi mkuu 2025.
Tume ya uchaguzi nchini ( ZEC) ina jukumu la kuzifanyia kazi
changamoto mbali mbali za uchaguzi zinazojitokeza mara kwa mara hasa katika kipindi cha
uchaguzi ili kutoa uhuru kwa vyombo vya Habari kufanya kazi zao
kwa uhuru na utulivu.
Sheria ya
kufuta sheria ya uchaguzi namba. 11 ya mwaka 1984 na kutungwa sheria ya
uchaguzi ya mwaka 2017 na maswala mengine yanayohusiana nayo.
Katika
sheria hii, kuna kifungu cha 122 ambacho
kinakizana na uhuru wa vyombo vya Habari nchini, ambacho kifungu hicho kinasema
‘’
‘’ Mtu
yeyote ambaye, atachapisha, atatoa
chapisho au atasababisha kuchapishwa au kutolewa chapisho, au atabandika au atasababisha kubandikwa au
atasambaza au atasababisha kusambazwa
mabango au posta yanayohusiana na uchaguzi au kampeni za uchaguzi bila ya kuwa
na
(a) ruhusa ya tume au msimamizi wa uchaguzi kwa kadri
itakavyofaa.
(b)
Anuani
ya mchapishaji
Atakuwa
amefanya kosa na akipatikana na hatia atalipaa faini isiyozidi shilingi milioni
tano na isiyopungua shilingi laki tano au atatumikia kifungo kwa kipindi
kisichopungua miezi sita na kisichozidi mwaka mmoja au adhabu zote faini na
kifungo
Akizungumza
katika madhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya Habari duniani 2025 ,
huko katika ukumbi wa Rahaleo Mjini Unguja
Katibu wa Jumuiya ya Wandishi wa Habari Zanzibar ( ZPC)
Mwinyi mvua Nzukwi kwa niaba ya Mwenyekiti wa Club hiyo Abdalla Mfaume, amesema tume ya uchaguzi lazima izingalie changamoto za wandishi wa Habari
kwani wao wapo kwa ajili ya kuwahabarisha
wananchi.
Amesema
kuwa, jukumu la kukusanya na kutoa taarifa kwa wandishi wa Habari ni haki ya
msingi na kisheria, hivyo serikali ina wajibu ya kuwalinda wanahabari ili
kuweza kuihabarisha jamii bila ya kukumbana na changamoto zozote.
“ Jukumu la
kukusanya na kutoa taarifa kwa wandishi
wa Habari ni haki yao ya msingi na ipo kisheria hivyo Serikali ina
wajibu wa kutulinda ili kutimiza wajibu wetu wa kuihabarisha jamii”
anasema Nzukwi.
Aidha
amewataka wandishi wa Habari kufuata madili ya kazi zao, katika kipindi cha uchaguzi ili
kuepuka kusababisha kupotea
kwa amani katika kipindi cha
uchaguzi.
Salim Said ,
ni mwandishi mkongwe wa Habari visiwani
Zanzibar anasema uhuru wa Habari na haki ya kujieleza ni jambo
muhimu litakalo pelekea mabadiliko Chanya kwa taifa.
Anasema ,
ili haki hiyo iweze kupatikana kikamilifu ni vyema mamlaka za nchi
zikaifanyiakazi sheria zinazokizana na uhuru wa Habari na kuzirekebisha ili kuondoa changamoto zinazoikabili tasnia hiyo.
Anasema
kuwa, kuna sheria mbali mbali ambazo
haziko sawa kwa wandishi kuziripoti kutokana na kufungwa kwa sheria hizo kama sheria ya uchaguzi.
“ Ni
vyema mamlaka zikaiangalia upya sheria hizi ili kutoa uhuru wa vyombo
vya Habari nchini” anasema Salim.
Nae,
Mhadhiri wa Chuo kikuu cha Taifa
cha Zanzibar ( SUZA) ambae pia ni mjumbe wa chama cha Wandishi wa
Habari Wanawake Tanzania Zanzibar (
TAMWA ZNZ) Imane Os. Duwe amesisitiza
kuwa tume ya uchaguzi inapaswa kutoa mafunzo kwa wandishi wa Habari yatakayo
Saidia kuzifahamu sheria za uchaguzi na namna ya kuripoti tukio hilo bila ya
Kwenda kinyume na sheria hizo.
Anasema kuwa,
wandishi wengi hawana uwelewa wa kuripoti Habari za uchaguzi hususani
kuhusu matokeo hivyo ni vyema tume ya
uchaguzi kutoa elimu hiyo.
“Tume ya
uchaguzi ni vyema ikatowa mafunzo kwa wandishi wa Habari ili kutoa uwelewa wa kuziripoti Habari za uchaguzi” anasema
Imane.
Anasema kuwa, ni vyema tume ya
uchaguzi ikavifanyia kazi vifungu
vinavyowabana wandishi wa Habari ili
wakapata uhuru wa kuripoti Habari za uchaguzi wa mwaka huu.
“ Ni lazima sheria hiyo ibadilishwe
ili iwape nafasi wandishi wa Habari kuripoti kwa uwazi Habari za uchaguzi”
anasema Ali.
Nae, Afisa Programu wa Maswala ya
utetezi na Uchechemuzi kutoka Chama cha Wandishi wa Habari Wanawake Tanzania
Zanzibar ( TAMWA ZNZ) Zaina Abdalla Mzee
anasema wamekuwa wakichukuwa jitihada
mbali mbali za kuzisemea sheria zote zinazohusu
habari ambazo haziko huru.
“ Tumekuwa tukipaza sauti zetu kwa
muda mrefu sasa kupatikana sheria nzuri ambazo ni rafiki kwa wandishi na vyombo
vya Habari” anasema Zaina.
Hata hivyo, ameeleza mikakati
waliyojiwekea katika kupaza sauti zao juu ya mapungufu yaliyomo katika sheria
mbalimbali ikiwemo sheria ya uchaguzi na sheria ya Habari Zanzibar ambayo mpaka sasa haijulikani
ipo katika hatua ipi.
MWISHO

Post a Comment