“ Mtindo wa maisha unavyoweka rihani maisha ya mama wajawazito”

 NA MARYAM NASSOR

Lishe bora   ni kitu muhimu kinachopaswa kuzingatiwa  na jamii ili kuwa na Watoto wenye afya na makuzi bora.

Hii ni kwasababu lishe  husaidia mwili kukua vyema, kujengeka  na kuimarisha kinga ya mwili  kupambana  na magonjwa.

Mtindo wa maisha  wenye afya  unaozingatia lishe bora, mazoezi na kuepuka vitu vinavyoweza  kuwa na madhara  ni miongoni mwa mambo muhimu anayotakiwa  kufuata mjamzito  ili aendelee vizuri.

Mambo hayo kama yatafuatwa yatamsaidia  mama na mtoto kuepuka hatari zisizo za lazima.

Imeelezwa kuwa  katika maisha ya sasa, mtindo wa maisha ni moja ya sababu zinazochangia hatari kubwa kwa wajawazito na vifo vya mama na mtoto.

Daktari bingwa wa magonjwa ya kina mama na Watoto kutoka Hospitali  kuu ya Mnazi mmoja Unguja,  Umulkulthum Omar anaeleza mtindo wa maisha  unavyoathiri afya za mama na mtoto.

Anasema,wajawazito wengi wanaohudhuria hospital wanakuwa na upungufu wa damu kutokana na vyakula wanavyokula.

“ utamkuta msichana  anakula chipsi na urojo  akija kuolewa akipata ujauzito hawezi kula, mwili wake unakuwa hauna  nguvu kwa kukosa virutubisho, kinachotokezea ni upungufu wa damu” anasema  Dk Umu.

Anasema kuwa, ni vyema jamii ikabadilika na kutumia vyakula vyenye virutubisho kutoka makundi yote ya vyakula ili kuwajenga Watoto kuwa na afya njema tokea wako wadogo.

“ Madaktari kipindi tunachokuwa hatulali na kukoroma ni kile kipindi cha mwezi wa Ramadhani, wajawazito wengi hupoteza maisha kwasababu ya kukosa damu” anasema Dk Umulkuruthum huku akishauri jamii ibadilishe mitindo yao ya maisha kwa kuona usasa ni kula vyakula ambavyo havina faida katika miili yao.

Ingawa Tanzania  imefanikiwa kupunguza vifo vya wajawazito vinavyotokana na matatizo ya uzazi kutoka wastani wa vifo 556 kwa kila vizazi hai 100,000  kwa mwaka 2015/16 hadi kufikia wastani wa vifo 104  kwa kila vizazi hai 100, 000   mwaka  2022.

 Lakini anashauri kuwa, ipo haja kwa jamii kubadili mitindo yao ya maisha kwa kula vyakula vyenye afya na ambavyo havina chumvi nyingi  na mafuta ili kuimarisha afya zao, ambavyo viko karibu na wao kama mboga mboga za majani.

Haitham Abdalla,  ni mama wa Watoto watatu anasema mara nyingi akihudhuria kliniki ya wajawzito huwa anaambiwa hana damu kwani anakuwa na kiwango cha damu tisa, hapo mimba ipo katika mwezi wa saba.

Anasema kuwa, akiwa mjamzito anatapika sana  na kupelekea kushindwa kula, na kila miezi ikienda mbele  damu inashuka na kushauriwa kutumia vidonge vya kuongeza damu mpaka ajifunguwe.

“ Nikiwa mjamzito kawaida sipendi kula na hata nikila huwa napenda niletewe urojo ndio unanipa hamu ya kula” anasema Haitham.

Nae, Abdalla Ali ni Baba wa Watoto wawili  mkaazi wa Mfenesini Unguja anasema, wanawake wengi wakiwa wajawazito hawapendi kula kutokana na hali zao lakini pia kujiendekeza.

Anasema kuwa, utamkuta mwanamke mjamzito hana damu lakini ukimpelekea vyakula vya damu kama  mboga mboga , maharage na matunda Havili, “ Anasema siwezi kula ni kweli lakini anatakiwa ajitahidi kula kwasababu hayuko pekee yake ana kiumbe tumboni ambacho kinahitaji kula kupitia mama yake” anasema.

Anasema kuwa, ni vyema wanawake wakiwa wasichana wapewe elimu ya lishe  bora, waaache kula vyakula ambavyo havina faida katika miili yao, kwani wao ni mama watarajiwa.

 Nae,  Fatma Haji mama wa Watoto watano , mkaazi wa Mkwajuni Wilaya ya Kaskazini ‘A’ Unguja anasema mara nyingi akiwa mjamzito huwa anakosa damu, kutokana na kukosa lishe bora.

Anasema kuwa,  baadhi ya wanaume hawazihudumii familia zao ipasavyo kwa kupeleka  vyakula vizuri majumbani .

“ Mimi mume wangu ni mchuuzi lakini Samaki wazuri hawaleti nyumbani, labda labda awe tayari kaanza kuharibika wateja wawe hawamtaki ndio amlete nyumbani kwa hali hiyo ndio maana tunakosa damu” anasema Maryam.

Anasema kuwa, ni vyema  wanaume wapewe elimu ya afya bora ili  isaidie kuleta vyakula vyenye afya majumbani .   

Kwa mujibu wa  ripoti ya Shirika la  Afya la Umoja wa Mataifa (WHO)linasema  kila siku wanawake 830 hufariki dunia kutokana na matatizo  wakati wa kujifungua na asilimia 99 ya vifo hutokea katika nchi zinazoendele.

Maryam  Ali Hassan  ni Mratibu wa  Afya ya Uzazi ya mama na mtoto wilaya ya  Kaskazini ‘B’ Unguja, anashauri wajawazito kuepuka kula vyakula ambavyo havina faida katika afya zao kama udongo na makaa na kula vyakula vyenye virutubisho kutoka katika makundi yote ya chakula.

“ Tunaendelea kutoa elimu kwa  jamii waone umuhimu wa kula vyakula vyenye Afya na virutubisho ili kulea mimba vyema na kujifungua salama” anasema.

Aidha amewasihi kina baba wawe karibu sana na wake zao kipindi cha ujauzito  na kuwahudumia kwa kuwapa vyakula vyenye afya ili kuepusha kuzaa Watoto wadumavu na kupunguza vifa vya mama na mtoto.

                        MWISHO NA MARYAM NASSOR

                        MWISHO

No comments

Powered by Blogger.