“ SARATANI YA SHINGO YA MLANGO WA KIZAZI NI HATARI KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA UKIMWI’’
Maryam Nassor
SARATANI
ya shingo ya mlango wa kizazi ni aina ya
saratani inayotokea kwenye mlango wa kizazi (sehemu inayounganisha uke na mji
wa mimba).
Saratani hii
husababishwa kwa kiwango kikubwa na maambukizi ya muda mrefu ya virusi vya
Human Papillomavirus (HPV), hasa aina za HPV 16 na 18.
Watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi wako
katika hatari kubwa zaidi ya kupata saratani hii kutokana na mfumo wao wa kinga
ya mwilini kuwa dhaifu.
Kwa mujibu
wa ripoti ya Shirika la Afya Duniani (
WHO) ya mwaka 2020 inasema saratani ya shingo ya mlango wa kizazi ni ya
nne kwa kuathiri wanawake, ikiwa na wagonjwa zaidi ya 604,000 .
Takribani asilimia 90 ya vifo hutokea kila mwaka , hasa katika nchi zenye kipato cha chini na kati
kama Tanzania.
Takwimu za
WHO zinaonesha kuwa, kila mwaka Tanzania
inapata wagonjwa wapya 42,000 wa saratani
ya shingo ya mlango wa kizazi ambao wanafika katika vituo vya Afya.
Akizungumza
na mwandishi wa Makala hii, Daktari
dhamana kutoka Hospitali ya Wilaya ya
Kaskazini ‘A’ Unguja Kivunge Haji
Machano anasema ugonjwa wa saratani ya shingo ya mlango wa kizazi
huwapata sana watu wanaoishi na ugonjwa wa ukimwi ukilinganisha na watu wengine.
Ameeleza
kuwa, ugonjwa huo huwapata sana wanawake
wanao ishi na maradhi ya ukimwi
kutokana na kudhofika kwa kinga zao na kwa Bahati mbaya hufika Hospitali
wakiwa katika hatua ya pili na tatu
hivyo ni taabu kutibika.
Anasema
kuwa, watu wenye ugonjwa wa ukimwi
hupunguza uwezo
Wa mwili
kupambana na HPV kwa kuwa ndio kirusi kinachosababisha saratani ya shingo ya mlango wa
kizazi.
”Watu
wanaoishi na VVU wanapata maambukizi sugu ya HPV ambayo huwaengeza hatari ya
kuendelea hadi hatua ya saratani” anasema dk Haji.
Aidha anasema
kuwa, katika wilaya ya kaskazin ‘A’ Unguja ugonjwa huo huwa athiri
wanawake hasa wanaoishi na maradhi ya
Ukimwi.
Anasema
kuwa, saratani hutokea mapema zaidi kwa watu waishio na VVU kuliko watu wasio
uguwa ugonjwa huo, na matibabu yake huwa na changamoto zaidi kutokana na kinga
ya mwiili kupungua.
Halima Ali
shuhuda wa ugonjwa huo, anasema alikuwa
anatokwa na damu kila akishiriki tendo la ndoa na mume wake.
“ Nilikuwa
natokwa na damu usiku na mchana kila niliposhiriki tendo la ndoa , nilijua
nimerogwa na mke mwenzangu nilimaliza
waganga mpaka siku moja nikamuhadithia rafiki yangu na kunishauri nije
Hospitali ndipo nikafanya vipimo na kugundulika ni saratani” anasema
Anasema
kuwa, ni vyema jamii ikawa na utaratibu wa kuchunguza afya zao mara kwa mara
ili kubainika mapema na kupata matibabu
katika hatua za awali.
Naye,
mgonjwa mwengine Asha Ame ( si jina lake halisi) alikuwa ameketi kwenye kiti,huku kichwa chake akikiinamisha chini yeye ni mkaazi wa Nungwi mkoa wa Kaskazini
Unguja anasema baada ya kuanza matibabu harufu mbaya imekata
na sasa anaendelea vizuri.
Amesema ,”
Mimi nilikuwa natoka na uchafu wenye harufu katika sehemu zangu za siri ndipo
nikaja kufanya vipimo na nikagundulika ni saratani ya shingo ya mlango wa kizazi” ameendelea kusema kuwa ni vyema watu wakawa
na utaratibu wa kufanya uchunguzi mara kwa mara.
Anasema
kuwa, wanawake wanaoishi na virusi vya
Ukimwi wako hatarini zaidi hivyo aliwata
wanawake kuchunguza afya zao mapema ili kupata matibabu .
Daktari Umukulthumu Omar kutoka Hospitali ya
Mnazi mmoja anasema saratani ya shingo ya mlango wa kizazi inaweza kutibika
iwapo itagundulika mapema, na kufanya vipimo vya Pap Test ( Papanicolaous
Test) Pap – smear ni kipimo ambacho hutumika
kuchunguza mabadiliko ya chembe chembe zilizoko katika mlango wa kizazi ili kugundua mabadiliko na kuwahi kuyakabili.
“ Kinga kuna
chanjo. Lakini kinga pekee kabla hujaanza kujamiiana upewe chanjo ambayo
inatolewa kwa wasichana wadogo maskulini kote, tuhamasishe watu waelewe chanjo,
kwa hiyo tuwapeleke mabinti wakapate chanjo” anasema Dk Umu.
Wataalamu wa
Afya katika mataifa mbali mbali ikiwemo
Tanzania wamekuwa wakito elimu ya ugonjwa huo katika jamii na kuhamasisha wanawake kujitokeza kuchunguza afya zao. Ili
kujulikana mapema kama wana mabadiliko ya awali au viashiria vya saratani ya shingo ya mlango wa kizazi.
Mkakati wa
WHO ni kupunguza idadi ya wagonjwa wapya
kila mwaka hadi kufikia wanne au pungufu zaidi kwa kila wanawake elfu moja na
kuweka malengo matatu yatakayofikiwa
ifikapo mwaka 2030.
mwisho

Post a Comment