ASYA MOHAMED AJITOKEZA KUCHUKUWA FOMU YA UBUNGE JIMBO LA KIJINI MATEMWE
![]() |
| NDUGU ASYA MOHAMED MUHIDIN ACHUKUWA FOMU YA UBUNGE JIMBO LA KIJINI MATEMWE |
ZOEZI
la uchukuaji fomu za kuomba
kuteuliwa kugombea nafasi za
ubunge, uwakilishi na viti maalum
kupitia chama cha Mapinduzi ‘ CCM’
wilaya ya kaskazini ‘A’
Unguja linaendelea vizuri.
Mwandishi wa Habari hizi alifika katika Ofisi za Chama hicho wilaya ya kaskazini ‘A’ na kushuhudia wanachama wa chama hicho wakichukuwa fomu hizo.
Mtia nia Asya Mohamed Muhidin kutoka Jimbo la Kijini Matemwe mkoa wa kaskazini Unguja alifika Ofisi za chama hicho kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya Ubunge.
Akizungumza
na mwandishi wa Habari hizi, nje ya Ofisi ya chama hicho mtia nia huyo, alisema
ameamua kuchukua fomu hiyo ili kuunga nguvu za Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ya kuwaletea wananchi maendeleo.
Amesema
kuwa, amevutiwa sana na kasi ya Dk Samia
ya kuwaletea wananchi Maendeleo kwa
haraka na Rais mwanamke wa kwanza kuiongoza Tanzania.
“
Nimechukuwa fomu hii ya kugombea ubunge katika jimbo hili la kijini ili kusaidiana na Raisi wetu kuwaletea
wananchi maendeleo” amesema mtia
nia huyo.
Aidha
amesema kuwa, kila mwananchi ni shahidi
wa maendeleo yanayoendelea nchini kwa kipindi kifupi alichoongoza Rais huyo.
Akizungumzia
vipaumbele vyake, endapo vikao vya chama hicho vikirejesha jina
lake na kugombea jimbo hilo la kijini na kushinda kwenye uchaguzi
mkuu wa mwaka huu ni Pamoja na kuimarisha huduma za kijamii katika jimbo hilo, Pamoja na
Elimu na Afya.
Akizungumzia
kuhusu uzoefu wa kuongoza mtia nia huyo, amesema kuwa ana uzoefu wa kutosha wa
kuongoza kwani alishakuwa mbunge wa viti maalumu kwa kipindi cha miaka mitano.
“ Nina
uzoefu wa kutosha wa kuongoza na kuwatumikia wananchi kwani nilisha Jifunza mengi wakati nikiwa mbunge wa viti maalum” amesema .
MWISHO


Post a Comment