KUKOSEKANA KWA SHERIA NZURI NA RAFIKI KUNAVYOKWAZA WAANDISHI WA HABARI ZANZIBAR


NA ASIA MWALIM

BARAZA la Wawakilishi Zanzibar (BLW) ndio chombo kilichopewa mamlaka ya kutunga sheria na kuzirekebisha sheria ambazo zinaonekana kupitwa na wakati ikiwemo sheria kandamizi zinazonyima uhuru kwa baadhi ya makundi.

Zipo sheria ambazo Baraza la Wawakilishi limezipitisha lakini zinawapa ugumu wananchi kujikita katika fursa mbali mbali za kimaendeleo kutokana na mapungufu yanayojitokeza na hali halisi ya wakati tulionao. 

Mfano wa sheria hizo ni Sheria ya Makosa ya Mtandao ya namba 14 ya mwaka 2015 imebainika kuwa na mapungufu makubwa sana kwa wananchi katika mazingira yao ya kila siku.

Mapungufu hayo yanasababishwa na vikwazo ambavyo vinawanyima fursa watanzania kutumia fursa zilizoko katika sekta ya mawasiliano na habari kwa maendeleo ya taifa.

Katika sheria ya makosa ya mtandao ya namba 14 ya mwaka 2015 kifungu 22 kinaeleza kuwa mtu ambaye kwa makusudi na kinyume cha sheria ataharibu, atafuta, ataondoka, ataficha, atabadilisha au ataifanya data komputa kukosa maana kwa lengo la kuharibu ushahidi au kuchelewesha upelelezi atakuwa ametenda kosa na akitiwa hatiani atawajibika kulipa faini ya kiwango kisicho pungua milioni tatu au kutumikia kifungo kwa muda usiopungua mwaka mmoja au vyote. 

Kipengele hiki ni vyema kianishe katika mazingira gani kufuta data hizo ni kosa, kwani kuna matumizi ya data binafsi, matumizi ya data kwa taasisi za wanahabari kulingana na kazi za kusanifu, kuchakata taarifa.

Pamoja na maendeleo ya sekta ya habari na upatikanaji wa taarifa hata hivyo watanzania wengi hawaifahamu sheria hii inawahusu kwa namna gani lakini kwa lugha rahisi ni kua inamuathiri mtu yeyote anaetumia mtandao wa intaneti kwa kutumia kifaa chochote ikiwa komputa au kifaa chenye uwezo wa kufanya kazi kama komputa au simu ya mkononi, saa, televesheni na vinavyoendana na hivyo.

Malengo ya sheria hii ni kuanzisha makosa yanayohusiana na matumizi ya mfumo wa komputa na teknelojia ya habari na mawasiliano, kuweka utaratibu wa upelelezi, ukusanyaji na matumizi ya ushahidi wa kielektroniki na masuala mengine yanayohusiana na hayo.

Matumizi ya mitandao yote mikubwa kama,Tiktok, WhatsApp, Barua pepe, Instagram, Twitter,Facebook, blogu na data zote zilizo katika kifaa chochote cha kielektroniki yanaathiriwa kwa kiwango kikubwa cha sheria hii.

Aidha katika Kifungu cha 23 (1)cha sheria namba 14 ya mwaka 2015 ya makosa ya Mtandao kinaeleza kuwa mtu hataanzisha au kushajihisha mawasiliano yeyote ya kielektroniki kwenda kwa mtu yeyote kwa kutumia mfumo wa kumputa, kwa lengo la kurubuni, kulazimisha kutisha au kunyanyasa au kusababisha maudhui ya hisia.

Kifungu hicho cha sheria hakikuanisha maumivu ya kihisia kulingana na wataalamu wa saikolojia kipengele hiki ni tata kwa sababu maumivu ya kihisia yameegemezwa zaidi kwa tafsiri.

Kuna nchi tofauti za Afrika ikiwemo Ghana, Mozambiq, Mali pamoja na Kenya zinafanya vizuri katika masuala ya habari kutokana na sheria rafiki walizonazo na nchi hizo zinaamini kuwa upatikanaji wa uhuru wa habari nchi zao zitafika mbali kimaendeleo.

WADAU WA HABARI

Mkuu wa taaluma Chuo cha uandishi wa habari na Mawasiliano ya Umma Zanzibar Imane Duwe, anasema dunia ikisherehekea ukuaji wa teknologia kwenye eneo la habari, lazima waandishi wawe huru katika kazi zao.

Mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari Zanzibar ‘ZPC’ Abdalla Abudull-rahman Mfaume anasema vifungu ambavyo vinawapa wasi wasi waandishi wa habari, havina nafasi Zanzibar.

Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) Zanzibar Dk. Mzuri Issa anasema dunia ya sasa inahitaji kufanya mambo kwa kasi inayoendana na wakati uliopo na sio wananchi kuwekewa vikwazo kila kona.

Mmiliki wa Fp Media, Hijja Abdulrahman anasema vijana wengi wameekeza kwenye mitandao ya kijamii, hivyo waziri akiamka na kutoa maamuzi ya kufungia chombo cha habari itachangia umasikini nchini.

WANASIASA

Salim Bimani mwanasisa wa Zanzibar anasema sheria hizo hizo zinachagua watu wa kuwapa makosawengine wataingia hatiani na wengine hapana kutokana na mifumi mibaya inayotumika kwenye masuala ya uhuru wa kujieleza kupitia mitandao.

WAANDISHI WA HABARI

Mwinyimvua Abdi Nzukwi anasema sheria hiyo imepitwa na muda na mabadilko makubwa yametokwa kwenye teknelojia na mahitaji ya waandishi wa habari.

Anasema kwa sasa taasnia ya uandishi wa habari na waandishi wamekua katika masuala ya digital imechukua nafasi na kufanya utendaji wa kazi kuwa kwa haraka jambo ambalo ni vigumu mtu kutumia kufanya kazi zake.

“Sheria nyingi zinampa maelekeozo ya kazi muandishi na kumpa adhabu sio kumlinda, takriban sheria sita zinamzunguka na hazina ulinzi wa kmlinda na kumuendeleza kwa mujibu wa sheria”anasema.

Hatua hiyo inaminya uhuru wa habari na kuwakosesha wananchi kutoa maoni na kupokea kwa kuhofia usalama wake.

Kuomba serikali kushirikiana na taasisi za kihabari kuvunja vikwazo vilivyopo kwa waandishi wa habari ili kuondoa wasiwasi wa kuripoti habari wakati wa uchaguzi.

“wakati huu kabla ya uchaguzi serikali inapaswa kuchukua hatua na kuyaepuka matatizo hayo ikiwemo kupata sheria zinazokwenda na wakati” anasema.

Anasema matumizi ya teknelojia katika usambazaji na kutafuta habari dunia imefika mbali kwani zama hizi zimeenea maendeelo, na kueleza kuwa Zanzibar nayo ni lazima kutumika kwani inarahisisha utendaji wa kazi.

Jesse Mikofu kutoka Gaazei la Mwananchi anasema yeye ni muhanga kwenye masuala ya tekneloji kwani aliwahi kutumia kifaa aina ya simu ya mkononi kuchukua picha tu baadhi ya watendaji walichukizwa na jambo hilo.

Anasema licha ya kuwa sheria hizo sio rafiki ni vyema waandishi wa habari na jamii kiujumla kuwa makini katika matumizi ya mitndao ili kuwa salama wakati wote. 

JAMII

Mohammed Saleh Mohammed, Salma Said Khamis, Fatma Mohammed Abdallah wanasema yeye ni mtumizi mzuri wa mitandao lakini hana elimu yeyote inayohusu sheria ya makosa ya mtandao, na hafikirii kwamba vijana wanalitambua hilo.

Aidha vijana hao waliomba serikali kutoa elimu ya masuala ya sheria zianzosimamia mitandao ili kuepusha vijana kwenda kinyume na sheria.

“Mimi nasikia tu unyanyasaji wa kupitia mtandao lakini sijui una maana gani, maudhui ya kihisia pia hatuyajui ni vyema sheria hii iweze kufafanua zaidi”anasema fatma.

Naye Mkuu wa Kitengo cha habari, Uhusiano na Huduma kwa walipakodi kutoka Mamlaka ya Mapato Zanzibar ZRA Makame Khamis Mohammed, anasema mabadiliko ya sheria yanafanywa ili kuwa na sheria nzuri na rafiki kwa jamii ikiwemo masuala muhimu ya kodi na teknenolojia ili kupata sheria zinazokwenda na wakati.

Anasema sababu zinazoshawishi kufanya mabadiliko ya sheria ni pamoja hali ya uchumi wa nchi, mwenendo wa ufanyaji biashara,mabadiliko katika teknologia, changamoto katika utekelezaji wa sheria na serikali kusaidia wananchi wake kutokana na misamaha ya kodi mbalimbali.

WIZARA YA HABARI ZANZIBAR

Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo Zanzibar Tabia Maulid Mwita, anasema mchakato wa upatikanaji wa sheria bora na rafiki Zanzibar, umewiva maana mswada wa sheria ambayo imejali maoni ya wadau, itafikishwa Baraza la Wawakilishi.

MWISHO 

 

No comments

Powered by Blogger.