ULINZI WA WANDISHI WA HABARI KIPINDI CHA UCHAGUZI BADO NI KITENDAWILI
NA MARYAM NASSOR
PAMOJA na
kufanya kazi kubwa ya kuhabarisha umma, waandishi wa Habari ulimwenguni kote wanakabiliwa na mashambulizi
yanayo hatarisha maisha na usalama wao.
Tafiti
zilizofanywa na shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni “UNESCO” zimebaini kuwa kati ya mwaka 2016 na 2020, zaidi ya wandishi wa
Habari 1,200 wameuwawa kwa kuripoti
Habari za umma.
Utafiti huo,
umeonesha kuwa kati ya vifo 10 ni
kisa kimoja tu ndio muhusika au wahusika
wanaadhibiwa au kufikishwa mahakamani .
Katibu Mkuu
Umoja wa Mataifa Antonio Guterres anasema
nafasi adhimu ya wanahabari kutumia nafasi yao, kuwezesha demokrasia na
kuwajibisha mamlaka iko hatarini kwa sababu ya kufichuwa kwao ukweli.
Akizungumza
na mwandishi wa Makala hii, Jesse Mikofu mwandishi wa Habari Mwandamizi kutoka
gazeti la Nipashe Zanzibar amesema waandishi wa Habari wanafanya kazi kwa ajili
ya umma , ni Daraja kati ya jamii na
Serikali hivyo wanahitaji ulinzi.
Amesema kuwa , kuna umuhimu mkubwa kwa Waandishi wa habari
wanapokuwa salama, kwani wanaweza
kufanya kazi zao kwa uhuru bila hofu ya kulengwa na makundi yenye maslahi
binafsi.
Aidha amesema kuwa, waandishi
wanatakiwa kujilinda wenyewe kabla hujafikwa na tatizo lolote kwani,hakuna
chenye thamani dhidi ya maisha yako.
“ Mimi binafsi nilishawahi kukutana
na misuko suko kadhaa nilishawahi kuwekwa ndani, wakati nafuatilia
Habari ya vitambulisho kule bara na
hapa Zanzibar pia wakati nikitimiza majukumu yangu, nilishawahi
kupigwa na hata kupoteza vifaa vyangu ”
anasema Jesse.
Nae,
mwandishi wa Habari kutoka sauti ya DW Zanzibar Salma Saidi amesema waandishi
wa Habari hawako salama duniani kote kwa sababu ya kazi zao za kuisemea jamii
na kuiwajibisha Serikali .
Amesema kuwa, Waandishi wa habari
wana jukumu muhimu katika mchakato wa kidemokrasia, hasa katika vipindi vya
uchaguzi. Wanatoa taarifa kwa umma, kufichua ukweli, na kuhakikisha kuwa
wananchi wanapata habari sahihi ili kufanya maamuzi yaliyo na msingi.
“Lakini ukitaka kujua kama hakuna uhuru wa Habari basi mfuate mwandishi
umwambie tufuatilie Habari Fulani hakuna aliye tayari kwa hofu ya maisha yake”
amesema Salma.
Aidha amesema kuwa, kuna umuhimu mkubwa wa ulinzi kwa wandishi wa
habari ,kwani changamoto nyingi, huwakumbwa
hasa kipindi cha uchaguzi ikiwa ni pamoja na vitisho, mashambulizi, na
ukandamizaji kutoka kwa wadau mbalimbali wa kisiasa.
Aidha amesema kuwa ,Waandishi wa habari wanapokuwa salama, wanaweza
kufanya kazi zao kwa uhuru bila hofu ya kulengwa na makundi yenye maslahi
binafsi. Hili linahakikisha kuwa habari zinazotolewa hazijachakachuliwa kwa
lengo la kupotosha umma.
Nae, mwandishi wa Habari
mkongwe Kisiwani Zanzibar Salim Said
Salim amesema Katika historia ya chaguzi nyingi duniani , waandishi wa habari wamekuwa
wahanga wa vitisho, utekaji nyara, na hata mauaji. Ulinzi wa kutosha unasaidia
kupunguza matukio haya, hivyo kuwawezesha kutekeleza majukumu yao kwa amani.
Amesema kuwa, Waandishi wa habari
ni miongoni mwa wale wanaowajibisha wanasiasa kwa kuhakikisha kuwa wanatimiza
ahadi zao na wanaheshimu misingi ya demokrasia. Bila ulinzi wa kutosha,
wanasiasa na taasisi zenye nguvu huweza kuwanyamazisha waandishi kwa vitisho.
“ Waandishi
wa Habari wanapolengwa , jamii kwa ujumla ndio inalipia gharama kwani wao wapo kwa ajili
ya kuiwakilisha jamii”
Aidha
amesema kuwa, jukumu muhimu la waandishi wa Habari ni kufichuwa
ukweli, lakini ukweli huo huja na gharama , hivyo ni vyema wapewe ulinzi na mamlaka husika ili kutimiza wajibu wao.
Jabir
Idrissa ni mmoja wa wajumbe wa kamati ya
Maswala ya Habari Zanzibar ( ZAMECO)
anasema upo umuhimu mkubwa wa ulinzi kwa wandishi wa Habari, kwani
wanafanya kazi kubwa ya kuihabarisha jamii na kuchochea maendeleo.
Amesema
kuwa, bila ya wandishi wa Habari wazalendo kwa nchi yao,basi maendeleo hayawezi
kupatikana.
“Habari
zinazotegemea ukweli na uchambuzi hutegemea
ulinzi na usalama wa wandishi wa
Habari wanaofanya kazi zao kwa uhuru, bila woga na upendeleo” anasema Jabir.
Akizungumzia umuhimu wa ulinzi, kwa waandishi wa Habari
hususani kipindi cha uchaguzi , Shadida Mohamed kutoka Ofisi ya Watetezi wa
Haki za Binaadamu Tanzania Zanzibar ( THRDC) anasema wandishi wa Habari wanafanya kazi kubwa hasa
kipindi cha uchaguzi, ni vyema ukaangaliwa usalama wao kwanza.
Amesema
kuwa, wandishi wa Habari ni kiungo muhimu katika jamii na Serikali kwa ujumla,
bila ya wandishi wa Habari hatuwezi kupata taarifa zenye ukweli na uwazi.
Nae, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni ‘UNESCO’ Audrey Azoulay amesema kutokana na hali hiyo dhidi ya vyombo vya Habari, Mataifa yana jukumu la kuwalinda wana Habari na kuhakikisha watekelezaji wa uhalifu dhidi ya Wandishi wa Habari wana wajibishwa.
Mwisho
Post a Comment