WAKULIMA KIJIJI CHA UZII, WANUFAIKA NA KILIMO MSETO

 

NA MARYAM NASSOR,

WAKULIMA KISIWA CHA UZII, WANUFAIKA NA KILIMO MSETO."


Uzii ni kisiwa kidogo kilichopo pembezoni mwa kisiwa Cha Unguja, Mkoa wa Kusini Unguja.

Kwa mujibu wa Ripoti ya sensa ya watu na makaazi ya Tanzania ya mwaka 2022, kisiwa Cha Uzii Kuna wakaazi wapatao 42,530.

Shughuli kubwa za kiuchumi Kwa wakaazi wa kisiwa hicho, ni kilimo na uvuvi, Ingawa Kwa sasa kutokana na mabadiliko ya tabianchi  wakaazi wa kisiwa hicho wanalazimika kulima kilimo mseto. 

Rukia Ibrahim Azani mkaazi katika kisiwa Cha Uzii, anasema  kutokana na mabadiliko ya tabianchi wanalazimika kulima kilimo mseto ili kupata faida lakini pia kukabiliana na  mabadiliko hayo . 

Amesema kuwa, hapo awali  walikuwa wanapata madhara makubwa ya kuharibikiwa na mazao yao kama, muhogo na ndizi kutokana na mabadiliko ya tabianchi.

Rukia anaeleza kuwa, kilimo hicho kimekuwa ni msaada tosha wa kujikwamua  na hali nguvu za kiuchumi Kijiji hapo.

"Kabla ya kupatiwa mafunzo ya kilimo mseto, Kila mwaka kipindi  Cha mvua , tulikuwa tunapata hasara ya mazao yetu, ila Kwa sasa Hali inaridhisha" amesema Bi Rukia. 

Amesema, kilimo mseto ni kizuri  kutokana na kuwa ni mchanganyiko wa mazao  ya matunda  na misitu na Mifugo.


"Kwa sasa wanawake wa Uzii, tunajishughulisha  na kilimo mseto,ambacho kinatusaidia kuendesha maisha yetu,Kwani  ndio shuhuli Kuu ya kiuchumi katika kisiwa chetu na Zaidi ya asilimia 55 ya wakaazi wa kisiwa hichi wanajishuhulisha na kilimo"amesema Rukia.

Mwantanga  Abubakar Haroub, ni mmoja  wa wakulima katika Kijiji hicho, anaeleza jinsi walivyofaidika na    kilimo mseto.

Amesema  kuwa, kilimo  hicho, kimekuwa ni msaada kwa wakulima, kwani watu wengi walikuwa wameacha kulima, kutokana na mabadiliko ya Tabianchi. 

"Hapo awali kabla ya kufikiwa na elimu ya kilimo mseto, tulikuwa tunaathiriwa Kwa kiasi kikubwa na mabadiliko ya tabianchi Kwa kuharibikiwa na mazao yetu" amesema Mwantanga.

Amesema kuwa, elimu waliyoipa kutoka   Taasisi ya community Forest Pemba (C FP)  ya kilimo mseto imewasaidia  kulima kilimo ambacho kina kabiliana na mabadiliko ya tabianchi. 

Othman Mwinyi Haji, ni sheha wa Shehia ya Uzii, amesema Kijiji hicho kimekuwa kikiathiriwa na mabadiliko ya tabianchi na baadhi ya wananchi wa kisiwa hicho kukosa chakula.

 

Amesema kuwa,  baada ya  kupatiwa mafunzo na mbegu kutoka Taasisi ya  (CFP)  wananchi wa Shehia hiyo ,wameanza  kulima kilimo mseto ili kujikwamua kiuchumi .

Aidha amesema kuwa, wananchi wa kijiji hicho walikuwa wameacha kulima kutokana na mazao yao,kuharibiwa na maji chumvi yanayoingia  kwenye mashambani yao.

"Tunashukuru sana Taasisi ya Community Forest Pemba, Kwa kutupa elimu ya kilimo mseto  ambacho ni mchanganyiko wa  miti ya matunda,  misitu na mifugo" amesema Sheha huyo.

Waziri wa nchi, Ofisi ya makamo wa Kwanza Zanzibar, Harusi  Saidi Suileiman alipokuwa akifungua kikao Cha kujadiliana  madhara ya mabadiliko ya tabianchi, amesema Zanzibar ni miongoni mwa nchi zilizoathiriwa na mabadiliko hayo.

Amesema,  kuwa mwaka 2012 Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Raia Zanzibar , ilifanya  utafiti kuhusu athari ya mabadiliko ya tabianchi kwa Uchumi wa Zanzibar na ilibaini, changamoto kubwa inayoikumba  Visiwa hivi. 

Changamoto hizo, ni ongezeko la joto, mabadiliko ya Mifumo ya mvua,kuongezeka Kwa upepo mkali, kupanda Kwa Kina Cha Bahari na maafa yanayotokana na Hali ya hewa.

"Tuzidi kushirikiana na Serikali yetu, katika kutoa Elimu Kwa wananchi ili kuona athari , hizo zinalindwa na kuwa na ustawi Mzuri Kwa taifa " amesema Harusi.

Mbaruk Musa Omar,ni Mkurugenzi wa Taasisi ya  Community Forest Pemba, amesema lengo la mradi huo, ni kuwafanya kina mama kuwa viongozi katika kukabiliana  na mabadiliko ya tabianchi, kwa kutunza mazingira, na kulima kilimo mseto.

Mkurugenzi huyo, amesema kuwa katika Kijiji Cha Uzi wakulima walikuwa wameacha kulima kutokana na madhara ya mabadiliko ya tabianchi lakini kwa sasa hali imekuwa inaridhisha.

"Tumeona tuupeleke mradi  huu ,Kijiji Cha Uzii kutokana na watu walikuwa wameacha kulima kwasababu ya mabadiliko ya tabianchi "amesema Mkurugenzi huyo.

Amesema kuwa, Mabadiliko ya tabianchi ni janga la Ulimwengu si la Zanzibar pekee yake, hivyo ni vyema wakashirikiana na Serikali katika kukabiliana na mabadiliko hayo.

Aidha amesema kuwa, kupitia mradi wa ZanziAdapt wanataka wanawake ndio, wawe viongozi katika kulima kilimo, ili kukabiliana na Mabadiliko ya tabianchi lakini pia kuinua vipato vyao.

''Wanawake tunataka wawe mstari wa mbele, katika kulima kilimo mseto kwani ni kizuri kinaweza kukabiliana na Mabadiliko ya tabianchi, lakiini pia mutapata mapato kuendesha  maisha yenu'' amesema Mkurugenzi huyo.

Shabani Peter, ni Ofisa wa teknolojia  ya Uzalishaji wa mradi wa ZanzAdapt, amesema mradi huo umefadhiliwa na Global Affair Canada, na umetoa elimu  na  mafunzo ya kilimo ,Kwa wanawake  zaidi ya asilimia  80, wa Unguja na Pemba, kuhusu kilimo mseto , mabadiliko ya tabianchi na kumfanya mwanamke awe kiongozi katika kukabiliana nayo.

Mradi huo, unatekelezwa Kwa kushirikiana na Shirika la Misitu Duniani (C F I), Chama Cha Wandishi wa Habari Wanawake Tanzania Zanzibar, (TAMWA ZNZ)  na Taasisi ya Community Forest Pemba,(CFP).

 


No comments

Powered by Blogger.