SMZ NA SMT YASHIRIKIANA KUTEKELEZA HUDUMA YA USALAMA NA AFYA KAZINI.

 NA NIHIFADH  ABDULLAH,


 SMZ NA SMT YASHIRIKIANA KUTEKELEZA  HUDUMA YA USALAMA NA AFYA KAZINI.

Serikali ya Mapinduzi  Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kwa pamoja wanatekeleza masuala ya usalama na Afya kazini Kwa lengo la kuhakikisha kila mfanyakazi yupo katika mazingira rafiki yatakayowezesha kuleta maendeleo.

Kauli hiyo imetolewa na Kamishna wa Kazi wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Kazi Uchumi na Uwekezaji Zanzibar , Rashid khamis Othman wakati akifungua kikao kazi Cha siku moja kupitia rasimu ya sheria namba 8 ya mwaka 2005 katika ukumbi wa wizara hiyo Mwanakwerekwe Wilaya Magharib B Unguja.

Amesema lengo la kuipitia rasimu hiyo ni kuiboresha sheria ya idara ya usalama na afya kazini ili isimame kuwa wakala na ifanye kazi zake Kwa kujitegemea, Kwa lengo la maendeleo ya sasa na  baadae.

Ameeleza kuwa Shirika la Kazi Duniani  (ILO) limepitisha mkataba wa msingi wa Usalama wa Afya kazini na kuwa ni haki sio wajibu kutokana na  umuhimu wake, hivyo amewataka  washiriki wa Rasimu hiyo kutoa maoni yatakayoimarisha sheria hiyo.

"Niwaombe washiriki muipitie vyema rasimu hii kwani michango yenu ni muhimu kufikia adhma ya jambo letu na kuendana na kasi ya mabadiliko ya kupeleka mbele maendeleo ya vizazi vya Siasa na  baadae"alisema Kamishna 

Kwa upande wake Mkurugenzi Idara ya Usalama na Afya kazini Ame Faki Saleh, amesema  idara imepewa maelekezo ili iwe wakala lazima kurekebisha Sheria yake namba 8, ya mwaka 2005 hivyo wameamua kukusanya wadau wenye uzoefu wa usalama na afya kazini  kuipitia Kwa pamoja rasimu hiyo.

"Ili kuanzishwa  wakala  mbadala wa idara ,kwenye rasimu hii kumeengezwa vipengele mbalimbali vitakavyowezesha kuiendesha katika Kazi zake"alisema Ame

Amesema majadiliano hayo ya marekebisho ya sheria  yanakuja  kutokana na wakati kufika kutoka idara ya usalama na afya kazini kuifanya kuwa wakala rasmi Zanzibar.

 Kikao hicho kimeshirikisha ma afisa kutoka idara ya usalama wa Afya kazini na wadau mbalimbali kutoka Mashirika, Taasisi za Serikali na   binafsi ambao wanauzowefu wa Usalama na Afya kazini.

No comments

Powered by Blogger.