Millioni 150,000 zatumika katika ununuzi wa vifaa vya Miundombinu ya Maji.
NAMARYAM
NASSOR,
Jumla ya shilingi million 150,000 za kitanzania zimetumika kununua vifaa vya mindombinu ya maji, Kwa wanufaika wa kilimo mseto, ili kulima na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Akikabidhi vifaa hivyo, Kwa wanufaika wa mradi ,Mgeni rasmi katika hafla hiyo ya ugawaji huko katika kisiwa Cha Uzii Ng'ambwa, Mkuu wa mkoa wa Kusini Unguja, Ayoub Mohamed Mahmoud, alivitaja vijiji hivyo , ni Uzii Ng'ambwa, Bungi na Unguja Ukuu.
Mkuu wa Mkoa huyo,amewataka wanufaika wa mradi wa ZanzAdapt kuvitunza
vifaa hivyo, ili vitumike kama ilivyokusudiwa.
Aidha , amewashukuru Jumuiya ya Community Forest Pemba(CFP) Kwa kujitoa kuwasaidia wananchi wa Kisiwa hicho na kuwataka Taasisi nyengine kuiga moyo wa kuzalendo walionao.
" Napenda kuishukuru Kwa dhati, Jumuiya ya Community
Forest Pemba Kwa kusaidia kutekeleza sera za Wizara ya Kilimo " amesema .
Nae, Mkurugenzi wa Jumuiya hiyo, Mbarouk Mussa Omar,
amewataka wananchi wa kisiwa Cha Uzii , Ng'ambwa, Bungi na Unguja Ukuu kuvitumia vifaa hivyo, kama ilivyokusudiwa.
Amesema kuwa, lengo la mradi wa ZanzAdapt ni kuwawezesha
wanawake Kwa kuwapa mafunzo na Miche ya
miti mbali mbali, ili kulima na kuinua vipato vyao kiuchumi.
Amesema kuwa, kutokana na Mabadiliko ya Tabianchi walikuwa , hawapati kitu kwenye kilimo kutokana na kuingiliwa na maji ya chumvi katika mashamba yao.
Mradi huo,wa Mabadiliko ya Tabianchi (ZanzAdapt)
unatekelezwa na Shirika la Misitu Duniani (CFI) chama Cha Wandishi wa Habari
Wanawake Tanzania Zanzibar (TAMWA ZNZ) na Jumuiya ya Community Forest Pemba
(CFP) na unatekelezwa katika shehia nane
Kwa Unguja na Pemba.
Post a Comment