MABADILIKO YA MITAZAMO YA WANAJAMII KATIKA SIASA
NA THUWAIBA HABIB
Ripoti ya mwaka 2021 iliyopewa jina la wanawake
bungeni iliyochapishwa na wanawake wa
wabunge dunia, ilionesha Rwanda ndio nchi inayoongoza duniani kwa kuwa na idadi
kubwa ya wanawake serikalini ambapo
63.8% ya wabunge na viti 13 vya uwaziri kati ya 32 vya mawaziri viliopo sasa
vimekaliwa na wanawake.
Idadi hiyo imemuhamashisha Mosi Haji Ushahidi
mkaazi wa kijiji cha Kikungwi kuona kuwa upo uwezo wanawake wengi kugombea nafasi
za uongozi na kuhamasisha wanawake wenziwe kuingia pia ili kufikia asilimia
kubwa ya kina mama wenye kuleta
maendeleo.
Mosi ni mama watoto watano ,56 amesema kwa kweli
huu sio tena wakati wa kurejeshwa nyuma wanawake kwa kutumia kasumba ya kuona
mwanamke hawezi kuongoza. Ni wakati wa kuendelea na safari ili wanawake wawe kama wanaume na kuwa na haki sawa ya kugombea uongozi
"Ni lazima wanawake
tuwe wamoja na kushikana mikono linapokuja suala na kugombea nafasi za Uongozi ."
Jambo muhimu ni wanajamii kutokubaguana kijinsia na
badala yake waende sawia katika uongozi wa nchi yetu.Hapa inafaa kukumbushana
kwamba mwanamke ni mwalimu, mtu mwenye ujasiri, hekima na busra na sio vyema
kudharau sifa hizi panapokuja suala la uongozi
"Kila mwanamke
anatakiwa kutodharau mwenziwe na kuwa pamoja kwa anacho kifanya kwani
tunaujasiri mkubwa katika masuala mbali mbali"
Mama huyu
aliwataka wanawake wenziwe kujiamini na kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa usahihi na vizuri wanapokwama
ukataka ushauri. na kujitoa kuwania nafasi
zilizopo katika siasa ifikapo 2025 njia
hiyo itawafanya watu wote waelewe uwepo wako.
‘’Ukiwa mtaani unapata maneno mengi yanayovunja
moyo ya kuwa hutoweza kuongoza muhimu ni kushikilia malengo yako tu’’,
aliongeza.
Katibu wa
wadi ya Bungi Wilaya ya Kusini Unguja Kassim Makame
Kombo, 42 amesema mimi ni miongoni mwa mwanaume ambaye nahamasisha wanawake
kuingia katika nafasi za uongozi na hata kuhakikisha nawasaidia katika kipindi
chao cha kampeni kwani nimegundua kuwa
wana uwezo mkubwa na niwapambania "Wanawake wana uwezo mkubwa wa
kutuongoza kwa hutumia juhudi kubwa kuhakikisha mafanikio yanapatikana"
Amesema sisi
wanaume tupo katika matabaka tofauti
baadhi yetu wanakuwa
ni wagumu kutoa fursa kwa wanawake
kuingia
katika siasa kutokana na sababu mbali mbali kama kufanyiwa udhalilishaji na mengine yanayoshusha heshima kwani vitu hivyo huweza fanyiwa mtu
yoyote muhimu kujielewa nini wanawataka tu.
"Wanaume tutowe
fursa kwa wanawake kugombea nafasi za uongozi kwa mtu yoyote awe mwanaume au
mwanamke anaweza kufanyiwa udhalilishaji kama haelewi ni anataka"
Katibu wa
Siasa Itikadi na Uenezi katika Wadi ya Kijitoupele, Riziki Abdallah Ali, amesema kwa mtazamo wake muda umefika wa kuwawezesha wanawake wengine
kuingia katika uongozi na hususa vijana wa kuanzia miaka 15 ili watoe mchango
wa kuijenga nchi.
Amesema kila mwanamke awe na uchungu na mwanamke mwenziwe kuhakikisha anashinda
katika uchaguzi ambao umetukabili mwakani kwa ni muhimu kupata watetezi wengi
wa kike ‘’Sasa woga wa wanawake kugombea umepungua na tunaahidi kujitokeza
kugombea nafasi mbali mbali katika uchaguzi wa mwaka 2025.alieleza riziki
Kwa kuwa wanajamii nyingi hufuata miongozo ya
dini na ndio nguzo ambayo wengi hutumia
katika kutolea maamuzi.
Mmoja wa wanazuoni maarufu wa elimu ya dini ya
Kiislamu, Profesa Issa Haji Zidi,
alipofafanua kwa undani kwamba
dini ya Kiislamu haijakataza mwanamke kuwa kiongozi wala kuwawekea
vikwazo.
"Dini ya kiislamu
hajakataza mwanamke kuwa kiongozi wa kumuwekea vikwazo bali inamtaka afuate
msingi ya dini katika uongozi wake"
Profesa Zidi ameeleza kwa undani kwamba katika enzi ya Mtume
Muhammad (SAW) walikuwepo wanawake waliokuwa viongozi katika vita na mambo
mengine na kote huko yalipatikana mafanikio chini ya uongozi wao.
"Wapo wanawake
walioweza kushiriki jatika vita jwa ajili ya kutetea dini ya kiislamu"
Alitoa mfano wa Bi Nasiba
binti Kaabu kuwa ni mmoja wa walinzi majasiri wa Mtume (SAW) katika vita vya Uhud na kuhakikisha mtume
anakuwa salama na alijeruhiwa takribani
mara 11.
Kwa mijibu wa ripoti ya sensa ya watu na makaazi ya
mwaka 2022 imeeleza kuwa Zanzibar ina watu 1,889,773 kati ya hao wanaumme ni
915 ,492 na wanawake ni 974 ,281 hii ina manisha kwamba wanawake ni asilimia 51.6ya wakaazi wote Zanzibar.
Asilimia
hiyo iliyokuwepo inatakiwa kushika
hatamu ya uongozi ifika 2025 kwani uwezekano huo upo endapo wanawake
watashirikiana na kuungana mikono katika kuhakikisha wanakuwa katika ngazi za
maamuzi.
Mkurugenzi wa wa chama cha waandishi wa habari wanawake Zanzibar _Tanzania Tamwa Dkt Mzuri Issa Ali amesema wanachukua
hatua za kuwasaidia wanawake kushiriki katika uongozi
Hii ni pamoja na kutoa elimu ya kujitambua,
kujielewa na kuthubutu kuwa wagombea huku wakizijuwa haki zao za kidemokrasia.
Na tunatoa elimu ya na namna ya kujilinda na rushwa
na kujuwa sheria za uchaguzi zinavyowalinda wanapokuwa katika harakati za
kugombea uongozi
Vijana
huunganishwa na wanasiasa wakongwe ili kupata uzoefu na kuhamasika kuchukua
nafasi za uongozi.
wanazopambana nazo ni pamoja na kuitaka jamii
ikubali mwanamke anao uwezo wa kuongoza
na kuachana na mila na desturi zinazomkwamisha mwanamke kupata nafasi ya
kuongoza wenzake
Kwa sasa tumepunguza matatizo yanayomkatisha tamaa
mwanamke asijitokeze mbele kugombea uongozi.Jambo muhimu ni kuondoa hofu na
kujichanganya na watu wote ili uwezo wao uonekane
"Tumeweza kupunguza
matatizo yanayokwamisha wanawake wasijitokeze kugombea jambo lilibaki ni wao
kuondoa hofu tu ili kushikilia nafasi hizo".
Aidha
Dira ya Zanzibar ya 2050 imeelezea jinsi gani masuala ya usawa wa jinsia juu ya
kuondoa unyanyasaji na kuimarisha mifumo ya uwezeshaji wanawake, ikiwa pamoja
na kuinua na kutoa nafasi za uongozi kwa wanawake.
Vile
vile imelenga kuongeza fursa na kuwawezesha katika vyombo vya kutoa maamuzi na
kwenye shughuli za uchumi, kijamii, siasa, ngazi za utawala na huduma za
sheria.
Naibu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na
Watoto Zanzibar, Anna Atanas Paul
amesema wizara hiyo itaendelea kuhamasisha wanawake kugombania nafasi mbali
mbali za uongozi wa kuchaguliwa ili ifikapo 2025 wafikie asilimia sawa 50
kwa 50.
Aidha amesema nafasi za viti maalumu kwa wanawake
ziondolewe badala yake nafasi hizo wapewe watu wenye mahitaji maalumu kwani
katika zama hizi wanawake wa Tanzania wameshathibitisha kwa vitendo kwamba
wanaweza kugombea majimboni na kushinda na kuongoza kwa ubora wa kiwango cha
juu.
"Chama Cha Mapinduzi na vyama vya
upinzani vimethibitisha kupitia chaguzi zilizopita kwamba wakiteuwa wanawake
kugombea wengi wao wanachaguliwa na kushinda", alieleza.
Katibu Uenezi Chama cha ACT
Wazalendo Halima Ibrahim Mohammed
ameeleza kuwa wanawake wamejitahidi kuchukua jitihada kubwa ya kushikana
mikono, kwa kuthibitisha hilo uchaguzi ujao wameandaa kampeni ya kumnyanyua
mwanamke, awemo katika ngazi za maamuzi, kamati kuu na halmashauri juu.
Uchaguzi wa mwaka 2020, mchakato wa kuwania nafasi
za uongozi majimboni kwa wanawake ulihamasika na kufikia takriban wanawake 400
waliojitokeza kwenye vyama mbalimbali vya siasa vyenye ushindani mkubwa,

Post a Comment