MTOTO WA KIKE ANAHAKI SAWA YA KUSHIRIKI MICHEZO ASIBAGULIWE

NA MARYAM NASSOR

Naibu Waziri   wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia,  Wazee na Watoto  Mhe Anna Atanas Paul ameitaka jamii kuelewa  kuwa mtoto wa kike ana haki za kushiriki michezo yote bila ya kudhalilishwa.

Ameyasema hayo  katika kilele cha maadhimisho ya  siku ya  kimataifa ya mtoto wa kike duniani, yalifanywa na wadau wa michezo kwa maendeleo Zanzibar ambao ni jumuiya ya wanasheria wanawake, Zanzibar (ZAFELA) kituo cha mijadala kwa vijana (CYD)na  chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania, Zanzibar (TAMWA,ZNZ) kwa kushirikiana na shirika la Ujeruman (GIZ)  huko katika viwanja vya mau zi dong  kikwajuni  ili kuhamasisha  ushiriki wa watoto wa kike na ustawi wa kijinsia katika michezo.

Amesema jinsia zote zina haki sawa ya kushiriki katika michezo na kutambua uwezo walionao na mchango wao una thamani sana katika jamii na kuhakikisha wanamlinda mtoto kike  akiwa katika mazingira yote kutokana na ukatili wa kijinsia.

Aidha amesema michezo itawasaidia watoto wa kike kujenga afya zao  za kimwili, kiakili, mashirikiano na kufurahi kwa pamoja.

"Michezo inamuwezesha mtoto kufaulu vizuri   iwapo hatopuuza masomo yake kwani kuondoa fikra mbaya"

Mhe Anna amesema  ipo haja ya kuwaongezea ujuzi watoto wa kike katika masuala ya uongozi na ushirikiano na kuwawezesha kuchukua nafasi  kubwa zaidi katika uongozi.



Mkurugenzi wakituo cha mijadala ya vijana CYD Hashim Pondeza  amesema tunahamasisha jamii kufahamu  kuwa mtoto wa kike apewe kipaumbele  kushiriki kwenye michezo mbali mbali kwani tutalinda usalama wao, mila na desturi zetu.

"Mtoto wa kike akishiriki michezo avae nguo za stara kama hijabu"

Kwa upande wake , Afisa Program kutoka chama cha waandishi wa habari wanawake Zanzibar, (TAMWA ZNZ) Asya Hakimu amesema michezo inamuhamasisha mtoto wa kike kutambua  viashiria vya udhalilishaji na kuweza kuviepuka.

Pia kupata uwezo wa kujiamini na kufanya mambo yake kwa ufanisi zaidi ambayo yatamletea mafanikio.


Nae Mwalimu wa skuli ya Bububu Bimkubwa  Abdurahman Ame amesema  michezo inawasaidia watoto wa kike kujichanganya na makundi tofauti na kupata kubadilishana mawazo pia hutoa fursa za ajira.

Nao wanafunzi walioshiriki mchezo wa netball zubeda said Ali na ibrahimu kamis haji kutoka kianga wamesema wanafurahi kushiki michezo wakiwa katika jinsia zote kwani wanazidi kupata uzoefu wa kucheza katika michezo ambayo walikuwa hawaichezi kama mpira wa miguu.

No comments

Powered by Blogger.