TAMWA YAWATAKA WANDISHI KURIPOTI HABARI ZA TABIANCHI






NA MARYAM NASSOR

Mkurugenzi wa chama cha waandishi wa habari  wanawake Tanzania,ZNZ(TAMWA ZNZ ) Dkt. Mzuri Issa Ali amewataka wanawake kutumia vyombo vya habari kuzitangaza kazi zao , hususan kazi zinazohusu  mabadiliko ya Tabia nchi .

Ameyasema hayo huko  Tunguu Unguja, alipokuwa akizungumza na wandishi wa habari na wadau mbali mbali,katika kikao cha kuandaa muongozo  wa namna gani waandishi watashirikiana  na jamii katika kuripoti habari za mabadiliko ya Tabia nchi.

Amesema muongozo huo utasaidia kuleta mabadiliko makubwa nchini hivyo ni vyema waandishi kuitumia elimu hiyo ili kuhakikisha mabadiliko ya  Tabia nchi yanabadilika kwa kiwango kikubwa.

"Nivyema kuufanyia kazi muongozo huu mliopatiwa kuleta mabadiliko ya tabia ya nchi kwa jamii zilizotuzunguka"alisema.

Akizungumzia kuhusu masuala ya kijinsia katika mabadiliko ya hali ya nchi aliwataka wanawake kufanya kazi kwa kujiamini sambamba na kuondoa hofu wakati wanapotoa taarifa husika kwa vyombo vya habari.

Aidha alisema kuwa, wanawake wanafanya kazi kubwa katika jamii lakini  kazi zao hazijulikani.

Kwaupande wake mkufunzi wa muongozo huo Shifaa Said Hassan amewataka waandishi hao pamoja na wadau wa sekta mbali mbali kufanyia kazi muongozo.

Alisema kuwa, muongozo huo ukitumiwa ipasavyo,  utasaidia kuleta mabadiliko katika jamii na taifa Kwa ujumla.

Dk Salim Suleiman Ali, mhadhiri kutoka chuo kikuu Cha Zanzibar (SUZA) akichangia mada katika kikao hicho, alisema  muongozo wa kuwasaidia wanawake kutumia vyombo vya habari ni mzuri, lakini pia wanawake hao wafundishwe jinsi ya kuweka kumbukumbu  vizuri katika vikundi vyao.

"Wanawake wengi waliokuwemo katika vikundi hawajui kutunza kumbukumbu , hivyo ni vyema wakapewa na elimu hiyo" alisema.

Nae, mshiriki katika  kikao hicho Najat Omar mwandishi kutoka The Chanzo,  alisema ni vyema wanawake hao kuunda magrupu ya mitandao ya kijamii ili kuwasaidia kutuma matukio yanayotokea katika jamii ili wandishi wa habari iwe rahisi kuyaripoti.

No comments

Powered by Blogger.