RAISI wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi, awataka wazanzibar kuliwekea mkazo suala la maadili mema.
NA MARYAM NASSOR
RAISI wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi, amewataka wazanzibar kuhakikisha wanaendelea kuliwekea mkazo suala zima la maadili mema,ili kupata jamii Bora na yenye kuthaminika.
Ameyasema hayo, makamo wa pili wa Raisi wa Zanzibar,Hemed Suleiman Abdullah huko Mahonda, Mkoa wa Kaskazini Unguja alipokuwa akimuwakilisha Raisi wa Zanzibar katika tamasha la 29 la utamaduni wa mzanzibar.
Amesema kuwa, Serikali ya mapinduzi Zanzibar kupitia wizara ya Habari Vijana, utamaduni na michezo itaendelea kuweka mazingira Bora ya kuendeleza sanaa na utamaduni wa mzanzibar.
Aidha, alisema kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, imeanza ujenzi wa nyumba za sanaa mwanakwerekwe Unguja, Kwa lengo la kuviendeleza vipaji vya wasanii na wajasiriamali wanaotengeneza bidhaa za utamaduni.
Amesema kuwa, Jengo Hilo likikamilika litakuwa na madarasa ya kufundishia sanaa mbali mbali na vitu vya utamaduni, ambavyo vitatumika kuitangaza Zanzibar nje ya nchi sambamba na kutoa fursa za ajira Kwa wahitimu wa mafunzo hayo .
Waziri wa habari vijana utamaduni na michezo, Tabia Maulid Mwita, amewapongeza viongozi wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Kwa kulifanikisha tamasha Hilo, kuwa la kipekee kwa kuwashirikisha watu wa rika zote.
Amesema kuwa, mara nyinyi tamasha Hilo huzinduliwa maneno ya mjini lakini mwaka huu wameona walipeleke mkoa huo, lakini tokea waaze matamasha hayo hajawahi kushuhudia tamasha zuri kama la mwaka huu.
"Tokea tuanze kuandaa matamasha haya, sijawahi kushuhudia tamasha lililofana kama hili ahsantee sana Wana kaskazini" alisema.
Nae mkuu wa wilaya ya Kaskazini 'B' Unguja Ame Seif Said akitoa salamu za mkoa huo, Kwa niaba ya mkuu wa Mkoa, amesema mkoa huo upo vizuri na umetekeleza ilani ya chama Cha Mapinduzi Kwa asilimia 100.
Amesema kuwa, mkoa huo umepiga hatua kimaendeleo kwani una mahoteli 260 kati ya hizo 22 ni hoteli zenye hadhi ya nyota Tano na kutoa ajira Kwa vijana wa Mkoa huo.
Aidha alisema kuwa, Kwa upande wa mindombinu ya barabara walipanga kujenga kilomita 147 za barabara mpaka 2025 na tayari wameshajenga kilomita 62 na Kwa upande wa mindombinu ya elimu wamejenga skuli Tano za ghorofa.
Tamasha Hilo la utamaduni ni la 29 na mwaka huu limezinduliwa mkoa wa kaskazini Unguja na tarehe 20- 26 litafanyika maneno ya Dole Unguja
Post a Comment