MWENYEKITI WA ACT WAZALENDO TAIFA AMESEMA, MAMLAKA YA KUENDESHA NCHI NI YA WANANCHI WENYEWE
NA MARYAM NASSOR,
MAKAMO wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, ambae pia ni
mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo taifa, Othman Massoud Othman amesema
mamlaka ya kuendesha nchi ni ya wananchi ambapo nguvu na uwezo wa Serikali
kufuata katiba, unatokana na wananchi
wenyewe.
Amesema hayo huko katika hotel ya Golden Tulip
Kiembesamaki Unguja alipokuwa akiwatangaza mawaziri wa kisekta 16(Mawaziri Kivuli) manaibu waziri pamoja na wizara zao.
Alisema kuwa,
lengo la kuteuwa mawaziri hao ni kuangalia utendaji wa Serikali , kisera na
kisheria juu ya kuwaletea wananchii maendeleo kwa kuishauri Serikali.
Amesema kuwa, hatua hiyo imekuja kutokana na maagizo ya halmashauri kuu ya chama
hicho,kuamua kuanzisha mabaraza hayo,
kutokana na uzoefu waliyoupata katika
baraza kivuli la mawaziri kule Tanzania bara na kuona ipo haja kuamua kuanzisha
hapa Zanzibar baada ya kushauriana na wenzake.
Aidha mwenyekiti huyo, amesema kuwa kifungu cha 10
cha katiba ya chama chao kimeweka
bayana malengo muhimu ya kisiasa na
nchi, miongoni mwa malengo hayo ni kuondoa kabisa vitendo vya rushwa na
utumiaji mbaya wa cheo kwa viongozi waliyokuwepo madarakani.
Alieleza kuwa, ibara ya 7 ya katiba ya chama cha Act Wazalendo inaeleza
malengo na madhumuni ya chama hicho, ambayo inakiambia chama kupigania
takribani malengo yote, yaliyoainishwa katika katiba ya Zanzibar katika kazi
zake za kuwa sauti kwa wananchi.
Nao baadhi ya Mawaziri na manaibu wao,walioteuliwa ni pamoja na
Profesa Ibrahim Fakih waziri wa Fedha na Halfan Amour Mohamed waziri wa
katiba na sheria, wameishuku kamati kuu ya Act Wazalendo kwa kuwapa fursa hiyo, na kuwahidi hakika wataitendea haki kwa kuwatumikia
wananchi.
Nao baadhi ya
wandishi wa habari waliopata nafasi ya kuuliza maswali walihoji, ni kwanini
wamemteuwa waziri mmoja mwanamke au hakuna wanawake wenye uwezo wa kuongoza katika chama hicho .
Akijibu maswali ya wandishi wa habari, mwenyekiti wa
chama hicho Othma Massoud Othaman alisema, wamezingatia uwiano wa jinsia kwa
kuteuwa manaibu mawaziri wengi wanawake.
MWISHO

Post a Comment