Mbunge wa Viti Maalum Zanzibar aunga Mkono Juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan
NA MARYAM NASSOR
MBUNGE wa viti maalum Zanzibar Bi Asya Mwadini Mohammed, amewataka wananchi wa Jimbo la Kijini Matemwe Mkoa wa Kaskazini Unguja, kuokoa maisha yao kwa kutumia nishati safi ya kupikia ambayo, itawaepusha na Athari katika mfumo wa upumuaji na kutunza mazingira.
Ameyasema hayo, huko Kijini Matemwe alipokuwa akigawa Majiko ya gesi ya kupikia kwa wananchi wa jimbo hilo, yenye lengo la kumuunga mkono jitihada za Raisi Samia Suluhu Hassan,katika kampen yake ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia.
Amesema Kuwa, matumizi ya nishati safi ya kupikia, itawasaidia wanawake kutumia muda mwingi katika kufanya shughuli za kiuchumi na maendeleo, kutokana na Kuwa matumizi ya gesi ni rahisi na yaana ukoamuda.
Amewataka wananchi hao, kuanza kutumia nishati safi ya kupikia kwa ujumla, kwani yataondoa uharibifu wa mazingira ambapo, Jamii itaachana na ukataji wa miti ovyo, na kumuondolea mwanamke adhaa ya kutumia muda mwingi katika kutafuta Kuni.
"Matumizi ya nishati safi ya kupikia, yatawasaidia kutumi muda mwingi katika kufanya shughuli za kiuchumi, kwani matumizi ya majiko ya haya ni rahisi na yanaokoa muda"alisema.
Aidha mbunge huyo, aliwataka wananchi hao kuwa mabalozi wazuri katika kumuunga mkono Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Samia Suluhu Hassan ,katika kampeni yake ya matumizi ya nishati safi ya kupikia.
Nae, mwananchi wa shehia iyo, Patima Mwepo Juma amemshukuru mbunge huyo kwa kuwajali afya zao,na kuwapa majiko hayo ya gesi ya kupikia na kuahidi kuanzia sasa watakuwa balozi wazuri wa kuhamasisha matumizi ya nishati safi.
"Kwa kweli mimi sijawahi kutumia nishati safi ya gesi kwa kupikia, lakin kuanzia Leo nitaanza kupikia" amesema.
Mwananchi Khadija Simai Makame, amemshukuru mbunge huyo kwa kuwapa majiko hayo ya gesi, na kuwapa elimu ya matumizi ya majiko hayo.
Awali mbunge huyo, mara baada ya kuwapa majiko hayo wananchi hao,aliwapa elimu ya matumizi sahihi ya majiko hayo ya gesi.
Zaidi ya majiko hamsini yametolewa na mbunge huyo, ikiwa ni muendelezo wake katika mkakatiti wa matumizi ya nishati safi ya kupikia, iliyozinduliwa na Raisi Samia Suluhu Hassan Mei 8, 2024 ikilenga kuepuka athari za kuni na mkaa, unaoambatana na utunzaji wa mazingira.




Post a Comment