MZEE WA MIAKA 50 APANDISHWA KIZIMBANI KWA KOSA LA KULAWITI MVULANA WA MIAKA 17
NA MARYAM NASSOR
MAHAKAMA ya
Mkoa Mahonda imempandisha kizimbani mzee
Alfred Barnabas Mbogo (50) wa Kinduni Unguja kwa kosa la kulawiti mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka (17).
Mara baada ya kufika Mahakamni hapo akitokea rumande mshtakiwa huyo,alisomewa
shitaka lake hilo na mwendesha mashtaka wa Serikali kutoka ofisi ya mkurugenzi
wa Mashtaka Zanzibar , Hariri Yeshau Ali mbele ya hakimu wa mahakama hiyo
Luciano Makoe Nyengo.
Mara baada
ya kusomewa shitaka lake hilo mtuhumiwa huyo, alikana kosa hilo .
Mwendesha mashtaka, alidai kuwa kesi hiyo leo
ipo kwa ajili ya kutajwa na upelelezi wa kesi hiyo imeshakamilika na kumuomba
hakimu wa mahakama hiyo kuihairisha na kuipanga siku nyengine kwa ajili ya
kuanza kusikilizwa kwa mashahidi.
‘’
Muheshimiwa hakimu leo kesi hii ipo kwa ajili ya kutajwa na Ushahidi wa kesi
hii umeshakamilika hivyo, tunaomba uipange siku nyengine kwa ajili ya kuanza
kusikilizwa kwa mashahidi’’ alidai Dpp huyo.
Awali
mahakamani hapo dpp Hariri alidai kuwa, mtuhumiwa huyo anashtakiwa kwa makosa
mawili kosa la kwanza ni kumlawiti kijana wa kiume miaka (17) kinyume na
kifungu cha 115(1) vya sheria ya adhabu
sheria namba 6 ya mwaka 2018 sheria za Zanzibar.
Na kosa la pili ni kutorosha mvulana ambapo ilidaiwa kuwa siku ya august
12 mwaka huu, majira ya saa moja usiku huko kinduni , wilaya ya Kaskazini ‘B’
Unguja bila ya halali alimchukuwa
mvulana wa miaka (17) kutoka nyumbani
kwao kinduni na kumpeleka kichakani , na kufanya hivyo ni kosa kinyume na
kifungu cha 133(1) (b) vya sheria ya
adhabu namba 6 ya mwaka 2018.
Hakimu wa
mahakama hiyo, alihairisha kesi hiyo hadi Septemba 9 mwaka huu kwa ajili ya
kuanza kusikilizwa kwa mashahidi.
MWISHO
.jpeg)
Post a Comment