MKE NA MUUME WAPANDISHWA KIZIMBANI KWA KUPATIKANA NA MIRUNGI
NA MARYAM NASSOR
MAHAKAMA Kuu Zanzibar iliyopo Tunguu Unguja imewapandisha
kizimbani watuhumiwa wawili ambao ni mke
na mume kwa kesi ya kupatikana na dawa za kulevya aina ya mirungi vicha 35 vyenye uzito wa kilo 3.851 .
Watuhumiwa hao, ambao ni mke na mume ambao ni Nassor Aman Ismail(41) na Zeyana Khamis Mohamed(39)wote wakaanzi wa meli nne taveta Unguja.
Wakisomewa
shitaka lao hilo na mwendesha mashtaka kutoka Afisi ya mkurugenzi wa mashtaka
Zanzibar Dpp Ali Amour mbele ya Jaji wa Mahkama hiyo Mohamed Ali Mohamed, alidai kuwa watuhumiwa hao walipatikana na dawa zinazodaiwa kuwa ni za kulevya aina
ya mirungi wakiwa ndani ya nyumba yao wanayoishi.
Mara baada ya kusomewa shitaka lao watuhumiwa
hao, walikana shitaka lao hilo na kuiomba mahkama wapatiwe dhamana ombi ambalo lilikataliwa.
Awali
mahkamani hapo ilidaiwa na mwendesha mashtaka wa Serikali, kutenda kosa hilo
disemba 21 mwaka 2023 majira ya saa11:30
jioni huko maeneo ya meli nneTaveta
wilaya ya magharibi ‘B’ Unguja wote kwa pamoja wakiwa ndani ya nyumba yenye namba SH/TV/ZH/08
bila ya halali walipatikana na
vicha 35 vya majani ambayo yanadaiwa
kuwa ni dawa za kulevya aina ya mirungi
yenye uzito wa kilo 3.851 .
Wakili huyo
alidai kuwa, kufanya hivyo ni kosa kinyume na kifungu cha 21 (1) (d) cha sheria ya mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa
za kulevy a, sheria namba 8 ya mwaka
2012 sheria za Zanzibar.
Jaji wa mahkama hiyo, aliihairisha kesi hiyo
hadi august 28 mwaka huu kwa kuanza kusikilizwa kwa mashahidi.
Post a Comment