MAYELE AHUKUMIWA MIAKA 14 JELA KWA KOSA LA KULAWITI MTOTO WA KIUME MIAKA 12
NA MARYAM NASSOR
MAHAKAMA maalum ya makosa ya
Udhalilishaji mkoa Mahonda Imemuhukumu
Kijana Sharif Juma Hamad (33) maarufu kwa jina la 'MAYELE' wa Mzambarau
mbata Unguja, kutumikia kifungo cha
miaka 14 jela kwa kukutwa na hatia ya makosa mawili ya Udhalilishaji.
Akisoma hukumu hiyo,Hakimu Luciano makoe nyengo alisema
kuwa mshitakiwa huyo amekutwa na hatia hiyo baada ya Mahakama
kujiridhisha na Ushahidi uliyoletwa na Upande wa Mashtaka
uliyoongozwa na Mwendesha Mashtaka Hariri Yeshau Ali, na vielelezo
vilivyowasilishwa Mahakamani hapo,
Hakimu Luciano , alisema kuwa Mshitakiwa huyo anatiwa
hatiani kwa Makosa mawili aliyoshitakiwa
nayo, kosa la kwanza ni Kulawiti mtoto wa kiume
mwenye miaka 12, kwa kosa hilo atatumikia Kifungo cha maiaka 14 jela.
Kosa la pili, ni kutorosha mtoto wa kiume alie chini wa
uwangalizi wa wazazi wake kinyume na kifungu cha 113 (1) (b) cha sheria namba 6
ya mwaka 2018 sheria za Zanzibar. na
kosa hilo atatumikia kifungo cha miaka 10 jela .
Aidha, Hakimu Luciano alisema kuwa adhabu zote hizo ziende
sambamba hivyo mshitakiwa huyo atatumikia kifungo cha miaka 14 chuo cha
mafunzo.
kesi hiyo, yenye namba 18 ilifunguliwa tarehe 11/6/2024
na kusikilizwa mashahidi sita na upande wa utetezi kulikuwa na shahidi mmoja
ambae ni mshtakiwa.
Awali mshtakiwa huyo, alishtakiwa kwa makosa mawili kosa la
kwanza likiwa ni kulawiti mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 12 kinyume na kifungu cha 115(1) vya sheria ya adhabu namba 6 ya mwaka 2018 sheria za Zanzibar.
Na kosa la pili ni
kumtorosha mtoto wa kiume aliye chini ya
uangalizi wa wazazi wake, kutoka
nyumbani kwao mgambo na kumpeleka nyumbani kwa mshtakiwa huko huko mgambo bila ya ridhaa ya wazazi
wake na kufanya hivyo ni kosa kinyume na kifungu cha 113 (1) (b) cha sheria namba 6 ya
mwaka 2018 sheria za Zanzibar .
MWISHO
.jpeg)
Post a Comment