WANANCHI SHEHIA YA MAHONDA WAMETAKIWA KUUTUMIA MFUMO WA SEMA NA RAIS MWINYI ILI KUTATULIWA KERO ZAO
NA MARYAM NASSOR
WANANCHI wa shehia ya Mahonda
wametakiwa kutoa malalamiko yao katika mfumo wa sema na Rais Mwinyi ili
kutatuliwa matatizo yao yanayowakabili katika sehemu husika.
Akitoa elimu juu ya mfumo huo, naibu mkurugenzi idara ya mawasiliano anayeshuhulikia maswala ya umma kitengo cha sema na Rais Mwinyi, Haji Khamis Makame huko katika Shehia ya Mahonda wilaya ya kaskazini ‘B’ Unguja.
Amesema mfumo wa sema na Rais Mwinyi ni takwa la wananchi, ambalo walilitoa wakati Rais Mwinyi alipokuwa akiomba kura kwa wananchi mwaka 2020.
Alisema
kuwa, ndipo baada ya kushinda urais, akaamua kuanzisha kitengo hicho kwani hapo
awali wananchi wa Zanzibar walisema hawana sehemu maalum ya kupeleka malalamiko
yao yanayowakabili na kupatiwa ufumbuzi,
kwani wakipeleka kwa viongozi wa chini yanadharauliwa na hayafanyiwi kazi.
Aidha amesema kuwa, mfumo huo, umeanzishwa kwa lengo la kusikilizwa na kutatuliwa kero za wanachi
hivyo, ni vyema wakautumia ili kupatiwa ufumbuzi wa matatizo yao yanayowakabili.
Naibu mkurugenzi huyo, aliwatoa hofu wananchi wa shehia hiyo kuwa, mfumo huo unausiri na uhakika wa kutatuliwa changamoto za wananchi kwani tokea uwazishwe wamepokea malalamiko 17,000 na kuyafanyia kazi,na kila siku wanapokea malalamiko 25 kutoka kwa wananchi.
Nae, sheha wa shehia ya Mahonda, Ali Issa
Kinole aliwaasa wananchi wa shehia hiyo, kuendelea kutuma malalamiko yao katika
mfumo huo, ili utumike kama ilivyokusudiwa.
Nae
Mwananchi Haji Fadhil alisema kuwa,
wanamalalamiko mengi kwa wizara ya mambo
ya ndani ya nchi , kwani wanapoenda
kupeleka kesi kituo cha polisi wanaambiwa watie gari mafuta au
wakamkamate mwizi wenyewe wampeleke kituoni.
‘’ Tukienda
kituo cha Polisi kushtaki mfano kesi ya mwizi au ubakaji, tunaambiwa tutie gari
mafuta au tukamkamate muhalifu wenyewe tumpeleke kituoni, sasa hatujui kuwa huo
ndio utaratibu au laa’’ alisema.
Nae
mwananchi, Mussa Haji alisema kuwa jee
katika mfumo huo malalamiko ya wananchi
yanamfikia kweli Muheshimiwa Rais au laa.
Akijibu hoja za wananchi wa shehia hiyo, naibu
mkurugenzi huyo aliwatoa hofu, wananchi hao na kuwataka kuripoti malalamiko yao
katika mfumo huo, kwani yanashuhulikiwa na wahusika na kupatiwa ufumbuzi.
MWISHO
Post a Comment