KESI YA RAIA WA UGANDA ALIYEINGIZA KETE 38 ZA MADAWA YA KULEVYA ZNZ,IMEENDELEA KUHAIRISHWA MAHAKAMA KUU TUNGUU ZANZIBAR
NA MARYAM NASSOR
KESI ya raia wa Uganda anayekabiliwa na shitaka la kuingiza madawa ya
kulevya nchini aina ya Cocaine kete 38
zenye uzito wa gramu 454,208 kutoka
Entebbe Uganda kuja Zanzibar imeendelea kuairisha Mahkama kuu Tunguu Unguja baada ya shahidi wa
kesi hiyo kushindwa kufika Mahakamani hapo kwa dharura ya Ugonjwa.
Kesi hiyo, inayomkabili Jackie Ninsima (33) Raia huyo wa Uganda
mwenye passport namba BOOO65972
alisafiri kwa ndege ya Ethiopian
airline kutoka Uganda kuja Zanzibar kupitia Ethiopian
na kushikwa na polisi wa Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Amaan Abeid Karume akiwa na pipi 12 za madawa
ya kulevya na pipi nyengine akiwa
kazimeza na kuzitowa kwa njia ya haja
kubwa akiwa katika hospitali ya Mnazi mmoja.
Mara baada ya kufika Mahakamani hapo akitokea
Rumande, mshtakiwa huyo alisomewa shitaka lake hilo na mwendesha mashtaka
kutoka ofisi ya mkurugenzi wa mashtaka Zanzibar, DPP Ali Amour mbele ya Jaji wa mahkama hiyo, Mohamed Ali
Mohamed.
Amedai kuwa shahidi wa kesi hiyo hawajafika mahkamani hapo
kwa sababu ya ugonywa,na kumuomba jaji wa mahakama hiyo kuihairisha kesi hiyo.
‘’
Muheshimiwa Jaji leo shahidi ambae
tunamtegemea leo hajafika mahakamani hapa , hivyo tunaomba shauri hili
ulihairishe na kuipanga siku nyengine ajili ya kusikilizwa shahidi namba tatu, ambae
tulipanga tumsikilize leo’’alidai Dpp huyo.
Jaji wa
mahakama hiyo, Mohamed Ali Mohamed alikubali ombi hilo, na kumuliza
mshtakiwa huyo,kuwa yuko tayari kwa ajili ya kuhairishwa kesi hiyo na
kujibu ndio.
Awali mahakamani hapo, ilidaiwa kuwa
mshitakiwa huyo raia wa Uganda
anashtakiwa kwa kosa la kuingiza
dawa za kulevya Zanzibar aina ya
Cocaine kete 38 zenye uzito wa gramu 454,208 kutoka
Entebbe Uganda kuja Zanzibar na kufanya hivyo, ni kosa kinyume na kifungu
cha 21 (1) (a) cha sheria ya mamlaka ya kudhibiti na
kupambana na dawa za kulevya, sheria namba 8 ya mwaka 2021 sheria za Zanzibar.
Jaji wa
mahkama hiyo, aliihairisha Kesi hiyo hadi septemba 13 mwaka huu kwa ajili ya
kusikilizwa kwa shahidi namba tatu.
MWISHO
.jpeg)
Post a Comment