BARAZA LA MANISPAA KASKAZINI 'A' UNGUJA LAKUSANYA BILIONI 1.2 KATIKA KIPINDI CHA JULAI -JUNI 2023-2024.



KAIMU Mkurugenzi wa baraza la manispaa wilaya ya Kaskazini 'A' Unguja , Makame Saburi Machano amesema katika kipindi cha julai hadi juni 2023-2024  baraza, limejipanga kukusanya jumla ya Tzs 1,340,063,900,00 kutoka vyanzo vya ndani vya  mapato na kufanikiwa kukusanya  1,271,717,779.52 sawa na asilimia 95 ya makadirio yake.

Kaimu huyo, ameyasema hayo katika ukumbi wa mikutano wa baraza hilo, mara baada ya kumaliza utoaji wa taarifa ya utekelezaji  wa shughuli za baraza la manispaa wilaya ya kaskazini 'A' katika kipindi cha julai hadi juni Kwa mwaka wa fedha 2023-2024.

Amesema kuwa, mapato hayo yamepunguwa kwa shilingi 289, 672,674.69 ukilinganisha  na makusanyo ya shilingi 1,561,390,454.21 yaliyokusanya katika kipindi cha julai hadi juni 2022-2023.

 Aidha akizitaja sababu za kupungua mapato hayo, kaimu huyo alisema ni pamoja na kutokufanyika kwa malipo ya makusanyo ya ada za mabango, kupungua kwa mazoezi ya ufuatiliaji  wa mapato pamoja na kuchelewa kwa marejesho ya fedha za maliasili na mwamko mdogo  wa kurejesha kulipa tena ada za vitambulisho vya ujasiriamali.

Amesisitiza kuwa, baraza la manispaa limejipanga kutatua changamoto hizo, na wameandaa mikakati mizuri ya kufikia bilioni 2.6 mwaka 2024-2025.

Nae, mstahiki meya wa baraza hilo ndugu Machano Fadhil Machano, (BABLA) amesema kwa sasa wanamalengo zaidi ya kuimarisha  suala la usafi , kukusanya mapato na pamoja na kukamilisha miradi ya maendeleo katika wilaya hiyo kwa kuunga mkono juhudi za  Rais wa Zanzibar wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dkt Hussein Ali Mwinyi katika azma yake ya utekelezaji wa ilani ya CCM ya 2020-2025.



Fatma Makame Omar, Diwani wa wadi ya Kivunge,jimbo la kijini  na Twaha Hija Kheir Diwani wadi ya Chaani jimbo la Chaani ,wamesema  tathimini ya kikao hicho wamejipanga katika utekelezaji mkubwa wa miradi ya maendeleo katika wadi zao, ili kuleta maendeleo pamoja na kutatua changamoto zilizopo kwa utekelezaji  wa mikakati  yaliyopangwa katika vikao vyao, ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Rais  wa Zanzibar Dkt Hussein Mwinyi,katika Wilaya , Mkoa na Taifa kwa ujumla.

                           MWISHO


No comments

Powered by Blogger.