WANDISHI WA HABARI ZANZIBAR WATAKIWA KUENDELEA KUFANYA UCHECHEMUZI ILI KUPATA SHERIA MPYA YA HABARI
NA MARYAM NASSOR
WANDISHI wa habari nchini wametakiwa kuendelea kufanya uchechemuzi kuhusu Sheria za habari ambazo ni kandamizi,kwani juhudi hizo zimesaidia kuweka matumaini ya baadhi ya Sheria hizo kufanyiwa marekebisho.
Hayo yameelezwa na wadau wa habari katika kikao Cha tathimini ya utekelezaji wa program ya uchechemuzi wa Sheria za habari Zanzibar, huko katika ofisi za Tamwa Tunguu Unguja. Kikao hicho kilichowashirikisha wandishi wa habari na wadau mbali mbali wa habari.
Zaina Abdalla Mzee ni afisa program hiyo, kutoka TAMWA ZNZ,amesema program ya uchechemuzi ya mabadiliko ya Sheria za habari zinazokwaza uhuru wa habari Zanzibar, umeonesha kuleta mabadiliko ya maboresho ya baadhi ya vifungu vya Sheria za habari ambazo ni kandamizi.
Alisema kuwa,tayari TAMWA ZNZ Kwa kushirikiana na wadau mbali mbali wakiwemo kamati ya wataalamu wa maswala ya habari Zanzibar, ZAMECO wamefanya vikao vitano na taasisi za Serikali ambavyo zinahusika na utungaji wa Sheria Kwa ajili ya maboresho ya vifungu vya Sheria.
Aidha alisema kuwa, kupitia mradi huo jumla ya wandishi wa habari 25 Unguja na Pemba wamepatiwa mafunzo na kazi 161 zimeandikwa , hivyo aliwataka wandishi kudhidi kufanya uchechemuzi wa Sheria kandamizi za habari ili zifanyiwe marekebisho.
Akitoa maelezo ya tathimini ya vipindi, makala na habari Hairat Haji afisa program kutoka TAMWA ZNZ Kwa niaba ya mtaalam wa tathimini na ufuatiliaji alisema, habari , vipindi na makala ambavyo vimetolewa vimeonesha ni jinsi gani wandishi wamekuwa na uelewa wa kutosha juu ya vifungu vya Sheria ambavyo ni kikwazo kwao.
"Tumepokea makala nyingi na vipindi kutoka kwenye social media, magazeti na vipindi vya redio,Kwa kweli zimechambua Sheria na mapungufu pamoja na mapendekezo ya nini kifanyike ili kusiwe na vikwazo Kwa wandishi wa habari juu ya kutekeleza majukumu yao"alisema.
Nao baadhi ya wandishi wa habari waliochangia katika kikao hicho walisema, wataendelea kufanya uchechemuzi wa Sheria kandamizi ili zifanyiwe marekebisho.
"Tutazidi kufanya utetezi na uchechemuzi wa Sheria kandamizi zinazokwaza uhuru wa habari Zanzibar Kwani ni zaidi ya miaka 20 tokea wandishi wa habari,Wadai Sheria mpya Kwa Serikali na bado ombi lao Hilo halijapatiwa ufumbuzi"walisema.
TAMWA ZNZ, Kwakushirikiana na wadau mbali mbali wa habari wamefanya mapitio ya Sheria nane za habari zenye vifungu vinavyokwaza uhuru wa habari Zanzibar, ikiwemo Sheria ya usajili wa wakala wa habari, magazeti ya tume ya utangazaji Zanzibar no.7 ya mwaka 1997 iliyorekebishwa na Sheria no.1 ya mwaka 2010. Mwisho

Post a Comment