MTUHUMIWA ALIYEMUUA MKEWE AFIKISHWA MAHAKAMANI
NA MARYAM NASSOR ,
MTUHUMIWA wa kesi ya mauwaji, Khalfan Ali Abdallah( 26)
amepandishwa katika kizimba cha mahkama kuu Tunguu Zanzibar ,kwa tuhuma za kuua kwa makusudi
chanzo kikitajwa ni wivu wa mapenzi.
Akisomewa shitaka lake
hilo na mwendesha Mashtaka wa Serikali kutoka ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar, Ali
Amour Makame mshitakiwa huyo alikana shitaka hilo.
Awali, Mwendesha Mashtaka huyo alimueleza Jaji wa mahakama kuu Zanzibar kuwa, kesi hiyo ni mpya na ipo kwa ajili ya Mshitakiwa kusomewa Shitaka lake.
Mara baada ya kusomewa kosa lake, Mshitakiwa Khalfan Ali Abdallah alikana kufanya kosa hilo la kumuua mkewe kwa makusudi.
“Muheshimiwa jaji, upelelezi wa kesi hii tayari umekamilika, Mshitakiwa leo hii hana wakili na hajaieleza Mahakama yako kuwa atakuwa na wakili au la, na kwa mujibu wa Sheria ya mwenendo wa Makosa ya Jinai ambayo ni sheria namba 7 ya mwaka 2018, katika kifungu cha 198 na 199 , kosa analoshitakiwa nalo ni kubwa na sheria hiyo inalazimisha mshitakiwa awe na wakili atakaemuwakilisha, hivyo tunaomba kesi hii ihairishwe na kuipanga tarehe
nyengine ili kumpa muda mtuhumiwa
kutafuta au kutafutiwa wakili kwa ajili
ya kumsimamia kesi yake” alidai Mwendesha Mashtaka huyo.
Baada ya maelezo hayo,
Jaji wa mahakama kuu Zanzibar Ali Mohamed alimuuliza
mtuhumiwa huyo kuwa yuko tayari kwa ajili ya kuhairishiwa kesi yake hiyo na
kujibu ndio.
Kesi hiyo yenye namba 16/2024,kwa mara ya
kwanza ilisomwa mahakamani hapo juni 3 mwaka huu na kuhairishwa
mpaka tarehe 26 mwezi huu, kwa ajili ya kutajwa tena mahakamani hapo.
Awali ilidaiwa
mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka, kuwa mstakiwa huyo anadaiwa kumuua kwa makusudi mkewe wa ndoa kwa sababu ya wivu wa mapenzi.
Mshitakiwa huyo, alitenda
kosa hilo, huko Bwejuu mkoa wa kusini Unguja majira ya saa 10:00 usiku.
Ilidaiwa mahakamani hapo
kuwa, kutenda hivyo ni kosa kinyume na kifungu cha 179 na
180 chini ya Sheria namba 6 cha mwaka 2018 sheria za
Zanzibar.
Jaji, aliiahairisha kesi hiyo hadi juni 26 mwaka huu kwa hatua ya kutajwa,
MWISHO

Post a Comment